MALAIKA WANNE WAZUIAO PEPO NNE ZA NCHI 

Siku za Mwisho No Comments

MALAIKA WANNE WAZUIAO PEPO NNE ZA NCHI 

Majira yaliyopo mbele yetu, si rafiki kabisa ndugu yangu, bali ni majira ya vita. Fahamu kuwa hii dunia haitaisha katika amani..Vipo vita vikubwa na vibaya vinavyokuja mbele yetu… Hilo haliepukiki kwasababu biblia ilishatabiri.

Leo hii tunasikia tetesi za vita katika mataifa makubwa, kila taifa linataka kuonyesha ubabe kwa lingine, lakini kwanini hatuoni vita vyeyewe vikipiganwa, ni kwasababu bado siku yenyewe haijafika.

Tukisoma katika kitabu cha Ufunuo sura ya 9 tunaona kuna malaika wanne waliowekwa katika ule mto mkubwa Frati kuzuia pepo nne zisivume juu ya nchi mpaka wakati uwadie.

Ufunuo 9:13 “Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao MALAIKA WANNE waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa WAMEWEKWA TAYARI KWA ILE SAA NA SIKU NA MWEZI NA MWAKA, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.

17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.

20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

Katika mstari wa 14 tunaona ikitolewa amri ya kufunguliwa kwa malaika hao waliokuwa wamefungwa katika Mto Frati. Na hawa lengo la kuzuiwa katika Mto Frati ni ili wasilete madhara waliyoamriwa kuleta kabla ya wakati kufika, kwamba wakati ukifika waue theluthi ya wanadamu wanaoishi juu ya nchi…Ili tujue hawa malaika ni wapi…turudi nyuma kidogo kwenye ufunuo Mlango wa 7.

Ufunuo 7: 1 “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,

3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao”.

Malaika hao wanne waliokuwa wamezuiwa kwenye mto Frati ndio hawa hawa ambao walionekana wamesimama kwenye pepo nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, Na pepo hizi nne ni upepo wa KI-SIASA, upepo wa KI-DINI, KI-UCHUMI na KI-JESHI. Hizo ndio pepo 4 za nchi.

Malaika hawa waliwekwa kuzuia vita vikuu vya Harmagedoni visitokee juu ya nchi.. Kwahiyo walikuwa wanazuia shughuli zozote za kipepo zisifanye kazi juu ya siasa ya dunia, uchumi wadunia, dini ya dunia wala jeshi la dunia, lakini sasa wakati huu, wataruhusu shetani aingie kuvuruga siasa ya dunia, uchumi, dini pamoja na jeshi…Yale mapepo yaliyotoka kuzimu yatawaingia wanasiasa wa dunia, sasa kuanzia wakati huu kutakuwa hakuna kuelewana duniani, kutakuwa hakuna kuvumiliana tena…mipango ya vita itawekwa, na amani itavurugika kwa kiwango kikubwa sana…Na ndio maana unajiuliza kwanini Leo mataifa makubwa yanagombana lakini hayapigani, nikwasababu malaika hawa wameamuriwa wazuie machafuko, lakini wakati utafika hakutakuwa na kuzuiwa tena, vitendo vitafuata.

Biblia inasema zaidi ya wanajeshi milioni 200 (elfu ishirini mara elfu kumi), watahusika katika mapambano ya vita hiyo ya Harmagedoni. (Kwa ufafanuzi zaidi tuandikie ujumbe inbox).

Hebu fikiria mwenyewe, haya mabomu ya nyuklia ambayo yanatengenezwa kila siku ni ya nini? Ni kwa ajili ya vita ya kumaliza hii dunia.

Kristo yupo mlangoni, umefanya uteule wako na wito wako imara sawasawa na 2 Petro 1:10?. Kama sivyo jitazame mara mbili, kisha chagua mwisho mwema, mambo haya sio hadithi tu za kale ni mambo ambayo yatakuja kutokea dhahiri mbele ya macho ya watu wengi.

Na sio miaka mingi ijayo, bali ni katika kizazi hiki yatatokea, kwani maandalizi yapo tayari.. kinachozuia tu mwisho mambo yote ni kanisa. Lakini moja ya siku hizi parapanda italia na wateule wa Mungu watanyakuliwa, na baada ya hapo wewe utakayebaki utashudia haya yote yakitokea, na hakika utajuta sana kwani wakati huo hata ukilia na kutubu toba ya kweli hautakusaidia, maana mlango wa neema utakuwa umeshafungwa.

Kilichobaki ni kupokea tu chapa ya mpinga-kristo na kisha kupitia dhiki kuu, kufa na kwenda kutupwa katika ziwa la moto.

Leo hii, Bwana anakupa tena nafasi nyingine..amua kuacha maovu yote na kumgeukia Bwana Yesu kwa kumaanisha kabisa kabisa.

Muda umekwisha, parapanda ipo karibu sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *