Mavazi ya kikahaba ni mavazi ya aina gani?

Biblia kwa kina, Maswali ya Biblia No Comments

Mavazi ya kikahaba ni mavazi ya aina gani?

Mithali 7:7 “Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,

[8]Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,

[9]Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani.

[10]Na tazama, mwanamke akamkuta, ANA MAVAZI YA KIKAHABA, mwerevu wa moyo;

[11]Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake.

[12]Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia”.

Mavazi ya kikahaba ni mavazi yanayovaliwa na makahaba kwa lengo la kuwavutia wateja wao.

Mfano wa mavazi hayo ni yale yanayoacha baadhi ya viungo vya mwili wazi na yale yanayochora umbile la mwili.

>Kwamaana hiyo, mavazi yote yanayobana mwili kuanzia juu mpaka chini (modo) ni mavazi ya kikahaba.

>Mavazi yanayochora maumbile ya mtu (tumbo, maziwa, makalio) ni mavazi ya kikahaba!

>Mavazi ya nusu uchi (vimini), mavazi ya mgongo wazi, kifua wazi, tumbo wazi yote hayo ni mavazi ya kikahaba.

>Gauni za kubana na sketi fupi ya kuonyesha mapaja, na suruali aina yoyote kwa mwanamke ni mavazi ya kikahaba.

Hivyo mwanamke wa kikiristo hapaswi kuvaa mavazi ya namna hiyo wala kuwauzia wengine.

Mwanamke wa kikiristo aliyeookoka kweli kweli, anaye ukiri uchaji wa Mungu anapaswa avae mavazi ya kustiri mwili wake wote kuanzia juu mpaka chini.

1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.

Je! wewe unayesoma habari hii, je mavazi yako yanaendana na ukristo au ni yale ya kikahaba?

Hebu jiangalie mwenyewe kisha chukua hatua ya kubadilika mara moja kwasababu watu watendao mambo ya jinsi hiyo (ukahaba & uzinzi)) hawataurithi ufalme wa Mungu bali sehemu yao ni jehanumu ya moto, biblia ndivyo inavyosema. (Ufunuo 21:8 & Wagalatia 5:19).

Amua kuchoma moto mavazi yote ya kikahaba na acha ukahaba mpokee Yesu ishi maisha ya utakatifu kama mwanamke/mwanamume anaye ukiri uchaji wa Mungu.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *