
MIMI NDIMI NJIA, KWELI NA UZIMA.
Yohana 14:4 “Nami niendako mwaijua njia.
[5]Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.
Shalom karibu tujifunze Neno la uzima.
Tukitaka kufika mahali Fulani au mji Fulani, ni wazi kuwa zitakuwepo njia nyingi za kufika mahali pale, zitakuwepo njia za Lami, au za vumbi, au vichochoro au hata njia ya maporini.
Zozote kati ya hizo njia zinaweza kutufikisha pale tunapotaka kwenda, isipokuwa zinatofautiana wepesi au ugumu. Njia nyingine zitakuwa ni nyepesi na rahisi, kwamfano zile za lami, vile vile njia nyingine zitakuwa ngumu, kwa mfano za vumbi au zile za mikato ya maporini.
Lakini kwa vyovyote vile mojawapo ya njia hizo zitatufikisha kule tunakotaka kwenda.
Lakini kwa habari ya kufika mbinguni HAIKO HIVYO!. Hakuna njia nyingi nyingi ambazo zinaweza kutufikisha mahali pamoja, kwamba tuchague yoyote kati ya hizo na mwishowe zitatufikisha mbinguni.
Bwana Yesu alisema wazi kuwa Njia ya kufika mbinguni NI MOJA TU..Na njia hiyo ni Yeye mwenyewe!.
“Alisema mtu hawezi kufika mbinguni isipokuwa kwa njia yake yeye”.
Ikiwa na maana kuwa hakuna njia nyingine ya mkato ya kutufikisha sisi mbinguni.
Unaweza kuwa na dini nzuri, lakini fahamu kuwa dini yako kama msingi wake sio Yesu Kristo basi huwezi kufika mbinguni, unaweza kuwa na dhehebu zuri lakini dhehebu lako kama msingi wake sio YESU basi siku ya mwisho hutamwona Mungu.
Unaweza kuwa na Imani nzuri, inayokufundisha kufanya mazuri, lakini imani yako hiyo kama inamkataa Yesu, au haimkiri Yesu basi siku ya Mwisho hutaweza kufika mbinguni, kwasababu hakuna njia nyingi za kufika kwa Mungu, njia ni Moja tu!!
“Unaweza kumwuliza mtu, je! Umempokea Yesu, atakuambia La! Sijampokea na wala simwamini.. lakini nina Imani, na ukizidi kumwuliza kama una uhakika wa kufika mbinguni siku ile ya mwisho?, anajibu kwa kusema Ndio!.. Ukizidi kumwuliza kwa namna gani?..atakujibu kwasababu anafanya matendo mazuri!, na zaidi sana njia ni nyingi ila Mungu ni Yule yule.”
Sasa mtu huyu ni kweli ana mawazo mazuri, lakini pasipo kujua kanuni za Mungu si kanuni za wanadamu..Sisi tuna machaguzi mengi ya kufika mahali Fulani, lakini Mungu ameweka njia moja tu!, na Jawabu moja tu la Maisha, na jawabu hilo ni Yesu!.
Matendo mazuri bila Yesu ni sawa na kufanya biashara bila leseni, ni sawa na kuendesha gari bila leseni, jambo ambalo ni kosa!.
Vile vile katika matendo yako mema unayoyafanya mweke kwanza Yesu kuwa Msingi, maana yake mwamini yeye na mkiri yeye, na kwa kufanya hivyo hata matendo yako Mungu atayaangalia na siku ya mwisho utafika mbinguni na kupata thawabu.
Usidanganywe na shetani kuwa zipo njia nyingi za kufika mbinguni. Njia ni Moja tu!, nayo ni YESU, siku zote usilisahau hilo!.
Je leo tayari umeshampokea Yesu na kuokoka?
Kama bado usingoje kesho kwasababu biblia inasema saa ya Wokovu ni sasa na wakati uliokubalika ni sasa (2Wakorintho 6:2).
Usiseme kesho nitatubu, au kesho nitampokea Yesu, mpokee Yesu leo kwasababu hajui dakika tano mbele ni nini kitatokea. Hivyo ili uwe salama kiroho na kimwili, mfanye Yesu tumaini lako kuanzia sasa.
Na baada ya kuokoka hakikisha unapata ubatizo sahihi, kama bado hujabatizwa, na ubatizo sahihi ni ule wa maji tele na kwa jina la Yesu (Yohana 3:23 na Matendo 2:38).
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.