Naamini nisaidie kutokuamini kwangu.
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe karibu katika tafakari ya neno la Mungu.
Andiko hilo tunalipata katika kitabu cha Marko 9:19-23 habari ambayo tunaifahamu wote kama wewe ni Msomaji wa biblia na kuna jambo kubwa hapo tutajifunza siku ya leo.
Katika habari hiyo tunasoma juu ya kijana aliyekuwa na pepo bubu tangu utotoni na likikuwa likimtesa kwa namna mbali mbali mwisho baba yake na mtoto alikutana na wanafunzi wa Yesu Kristo wakajaribu kumtoa pepo lakini haikuwezekana Yesu Kristo anakuja na kuuanza kuuliza taarifa zake na mwisho anamuamuru pepo hiyo Mtoke na ikawa hivyo.
Jambo ambalo nataka tuliangalie hapa juu ya mzazi wa huyo mtoto kwa nini akizungumza kauli kama hiyo? Na sisi tunajifunza nini katika habari hiyo. Tusome..
Marko 9:24“Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.”
Kwa nini anasema “….Naamini,nisaidie kutokuamini kwangu.”
Ukisoma kwenye biblia ya kiingereza inasema..
Mark 9:24[24]At once the father of the boy gave [an eager, piercing, inarticulate] cry with tears, and he said, Lord, I believe! [Constantly] help my weakness of faith!
Maana yake..
Marko 9:24
[24]Mara babaye yule kijana akalia kwa machozi, akasema, Naamini, Bwana! [Daima] nisaidie udhaifu wangu wa imani!
Ukirudi hapo juu linatumika neno “Constantly” maana yake ni kitu kisichobadilika kama vile jua linavyochomoza kutoka mashariki kwenda magharibi hakuna siku litachomoza kutoka Kaskazini kwenda kusini. Sasa ni kwa namna gani anasema hivyo jibu tumelipata hapo ni kwa sababu ya udhaifu wa imani aliyokuwa nayo juu ya jambo hilo.
Sasa nini maana ya imani? Biblia imetupa majibu..
Waebrania 11:1″Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
Kumbe imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo!!.
Sasa naomba usome kwa makini sana hapa hii itakusaidia na Mungu wa mbinguni akusaidie kuyaelewa haya.
Wakristo wengi sana wanatatizo hili na mimi nimewahi kuwa mmoja wapo.. unajikuta unaamini jambo lakini unakuwa na mashaka juu ya hilo jambo kama kweli litatokea?
Yaani unaamini kwa kipindi fulani kifupi lakini ndani yako unaanza kuona shaka itawezekana kweli? Si kwamba hujaamini moyoni mwako la umeamini lakini kuna mashaka fulani yanajitokeza.. Ndio kilichomtokea hata baba yake na huyo kijana mwanzo aliamini lakini akawa na shaka ndani yake kama kweli kijana wake atapona.
Sasa weka hili akili vizuri mtu wa Mungu..
“Imani si asimilia miamoja kuamini kikamilifu” kwa maana nyingine ni hivi.. unaposema unaamini si katika asilimia zote 100% bila mashaka la!. Yaani inatokea tu unaamini asilimia zote bila kuona aina yoyote ya shaka ndani yako.
Siku zote imani na mashaka huambatana kwa pamoja(huja kwa pamoja).. namaanisha imani ni uchaguzi wa kweli ambao mtu anaamua ndani yake.. hivyo Imani na mashaka vinapokuja kwa pamoja ni jukumu langu mimi na wewe kuchagua.. ukichagua kuamini hicho kitu kitatokea.. ukichagua kuwa na mashaka jambo hilo halitatokea.
Na hakuna mwanadamu yeyote asiyekuwa na mashaka labda huyo si mwanadamu.. mashaka siku zote yapo kwa kila mmoja mmoja wetu Sasa ni sisi kushindana na hali hiyo ya kuwa na mashaka ndani yetu shindana mpaka uone hauna mashaka tena ndani yako juu ya jambo hilo unalolitamani kulipata kutoka kwa Mungu. Hivyo usisumbuke na pale mashaka yanapokuja juu ya kile ulichoamini jukumu lako ni kuhakikisha mashaka hayatawali ndani yako.Inawezekana kabisa..
Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi baada ya kuuambia yasipatikane matunda na ukanyauka wakati alipokuwa njiani wanafunzi wake walishangaa baada ya tendo lile lakini aliwaambia..
Mathayo 21:21“Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka.”
Unaona hapo? Bwana Yesu aliwaambia “mkiwa na imani,Msipokuwa na shaka…”
Hivyo imani siku zote unapotaka kuamini kitu fulani lazima pia mashaka yanakuwepo Sasa ni sisi kuhakikisha hatutawalilwi na mashaka ya namna yoyote bali tunaamini ni kawaida ya mwanadamu akili zetu(Fahamu zetu na mitazamo yetu) inakwenda kinyume kabisa na mambo ya rohoni.
Sasa ni kwa namna gani tutayashinda mashaka.
1.Kusoma biblia.
Unapokuwa ni Msomaji wa maandiko neno la Kristo linakaa ndani yako. Na neno la Kristo ni hai hivyo linapokaa ndani yako linakupa hakikisho/linakujengea imani.(Waebrania 4:12).
2.kuwa muombaji.
Unapokuwa muombaji kila siku kwa masafa marefu huku ukitumia neno la Mungu utaona mabadiliko makubwa mno utajikuta unashida hali ya kuwa na mashaka ndani yako.. maombi ni sehemu ambayo tunajengwa na kuimarishwa zaidi imani kupitia maombi inajengeka zaidi maana kupitia maombi ufahamu wetu unazidi kukua na Mungu anasema na watu sana zaidi katika maombi.
Tunakosa kumsikia Mungu kwenye maombi na tunaona ni ya kawaida tu ni kwa sababu tunakosa umakini tunapokuwa katika maombi.
Yapo mambo mengi sana yanayoweza kutusaidia lakini kwa uchache anza na haya na hakika utaona mabadiliko makubwa sana ndani yako.
Nimekuombea na nina imani unakwenda kuwa mtu mwingine.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.