NAWEZAJE KUSHINDA MAJARIBU?

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Majaribu ni mtaji..,” kwetu sisi Wakristo majaribu ni mtaji yanayotuongezea daraja kubwa sana pale tunapofanikiwa kuyashinda..

Na bahati mbaya au nzuri siku zote unapokuwa katika jaribu ni ngumu sana kujua kama uko kwenye majaribu.  Na hata unapofahamu upo katika majaribu ni vigumu kujua jaribu lile linakuimarisha ama kusudi lake kubwa haswa ni nini.

Na jukumu lako yakupasa ushinde uendelee mbele… Sasa kwa namna gani unaweza kushinda?

Siku zote mleta majaribu ni Shetani na lengo lake shetani anapoleta majaribu sio kwamba akuimalishe uzidi kupanda daraja kubwa mbele za Mungu.  Lengo lake kubwa ni wewe kukuangusha katika imani na yuko makini sana na siriazi na kitu anachokifanya.

Maana hafurahii wewe unapoendelea kudumu katika imani. Na kama kwa Mkristo ulieokoka kweli kweli na kuamuna kumfuata Yesu Kristo ni lazima utamuona Shetani dhahiri kabisa. Lakini ikiwa hujaamua kweli kusimama na Kristo kamwe hutayaona utakuwa unasikia tu.

Sasa anaweza kukuletea majaribu katika maeneo mbali mbali katika afya yako/magonjwa,uchumi wako,ajali,Mafarakano katika familia/ndoa,mikosi,Vishawishi ili utende dhambi ujiweke mbali na Mungu nk lengo ni kukuangusha. Yote haya yanampata mtu alieamua kumfata Kristo kweli.

YESU Kristo aliwaambia pia wanafunzi wake kuwa “Majaribu hayana budi kuja” maana yake ni sehemu ya maisha ya mwamini alieamua kumfata kweli kweli Kristo.

Lakini aliwaambia pia namna ya kuyashida wao ni KUOMBA/MAOMBI.

wakati Yesu anakaribia kwenda msalabani karibu katika injili zote alikuwa anawaasa sana wanafunzi wake waombe alikuwa anamaana kubwa sana alijua hawataweza kuyashinda majaribu bila maombi..

Mathayo 26:40 ” Akawajia wale wanafunzi wake, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, je! hamkuweza kukesha pamoja nami hata SAA MOJA?.

41Kesheni, MWOMBE, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

Utaona Bwana Yesu anakuja kuwamsha wanafunzi wake waombe(jambo ambalo kabla hajakaribia kwenda msalabani hakuwa anawaambia maana hakukuwa na jaribu lolote kwao)

Sasa Bwana aliona ni nini kitakachotokea mbele na ndio maana akawaambia wanafunzi wake waamke waombe lakini hawakumsikia. Yesu mwenyewe aliomba ikiwezekana kikombe kile kimuepuke lakini haikuwezekana..lakini tunaona katika maombi yale jaribu halikuondoshwa kabisa ila tunaona Mungu anampa nguvu ya kukistahimili kikombe kile na ndio maana tunaona malaika wanamtokea na kumtia nguvu mahali alipokuwa akiomba.

Lakini tunaona Baada ya Yesu kustahimili pale wanafunzi wake hawakuweza kabisa kustahili kwa sababu hawakuomba hivyo jaribu lilipokuja walishindwa. Tunamuona mtume Petro baada ya kujalibiwa na mwovu alimkana Bwana Yesu mara tatu (hakufanya vile kwa bahati mbaya alikwa anamaanisha kweli).

Lakini wangelikesha na Bwana kweli kweli katika kuomba wangeweza kushinda maana Mungu angeliwapa nguvu ya kustahimili jaribu lile kama vile Bwana Yesu alivyopewa nguvu hiyo.

Jambo hili linaendelea hata sasa kwa Mkristo yoyote aliesimama fahamu unapolala ndugu yangu Shetani halali anazidi kuoanga majeshi yake ili akuangushe kabisa. Kama majaribu yalimpata Mwokozi wetu Yesu Kristo ambae alikuwa muombaji na mfungaji na Mhubiri,nabii,Mwalimu(karama zote na nguvu alikuwa nazo) yalimpata vipi kuhusu mti mkavu mimi na wewe? Ikiwa aliomba BABA amwepushe na majaribu imekupasaje wewe na mimi ndugu?

Jambo hili aliwafundisha hata wanafunzi wake pale wanapomwomba Bwana, waombe awaepushe na majaribu (fahamu tu siku zote huwezi kuepushwa na Jaribu lisikipate ila utapewa nguvu ya kulishinda.). Anawambia wawe wakiomba “USITUTIE MAJARIBUNI BALI UTUEPUSHE NA YULE MWOVU”. ni maombi ambayo unapaswa uyaombe kila siku kama mwamini.

Na ni vyema zaidi kutambua maeneo muhimu ambayo ibilisi anayatumia kukuangusha au kukudhoofisha kiimani ili usiendelee mbele ni muhimu kuyafahamu ndugu yangu. Atatumia marafiki zako,Familia yako au watu wako wa karibu sana. Ili ushindwe kusoma neno, ushindwe kuomba uwe ni Mkristo usiekuwa na ulinzi wa maombi.

Huna budi kuomba sana ili Bwana Yesu awalinde watu hao ili asiwatumie katika kukuangusha ama kukudhoofisha kiimani. Ilikwa Ibilisi aliweza kumtumia Yuda aliekuwa karibu na Bwana Yesu vipi hukusu hao watu wako wa karibu?

Anaweza pia kutumia maboss wako au wafanyakazi wenzako ili kukuangusha na kukukosesha nguvu ya kusonga mbele inakuoa kuwa makini. Unapoomba hivi unaruhusu Mungu aachilie neema ya kukuwezesha kushinda jaribu lolote litakalokuja hutatikisika kamwe.

Kama Danieli aliweza kuepukana na kumezwa na simba ni kwa sababu alikuwa ni muombaji Danieli na alikuwa anatembea katika njia ya haki. Siku zote ukitaka utembee katika mapenzi ya Mungu ni lazima uwe muombaji. 

Kinyume chake usipokuwa mwombaji ni lazima Shetani atakushinda tu hata ujitumainishe vipi utapigwa ndugu. Ili uweze kushinda kuwa ni mtu wa kuomba kila siku ingia magotini omba sana katika Roho.

Si kwamba Petro alikuwa na mpango wa kumkana Bwana atakapoingia kwenye matatizo la!. Petro alikuwa radhi kufa na Bwana lakini kwa nini alimkana? Kwa sababu hakuwa na hiyo nguvu ya kustahimili mwisho wa siku akamkana Bwana Yesu.  Nguvu hii ya kustahimili jaribu inapatiakana katika maombi tu zaidi ya hapo hakuna na haiwezekani..

Hivyo kama Mkristo hakikisha kwa siku nzima yote unaomba hata kwa kiwango kile cha chini kabisa yaani SAA 1. ndio kiwango cha chini sana.

Lakini kama ni Mkristo inapita wiki nzima au siku nzima hujaomba hata saa1 uko kwenye hatari kubwa sana ya kuanguka ikiwa kweli umedhamiria kumfata Kristo utaanza kuona ugumu na shida ya kuwa Mkristo. Ukristo wako hautakuwa na furaha.  Kwa sababu huombi.. Shetani atakujaribu na kukutumia kila aina ya mishale utajitajidi kukwepa mwisho utakupata tu.

Usikubali siku nzima uko busy na mambo ya kidunia tu yaani Kazi harafu inapita siku yote hujaongeza kitu kingine katika roho yako kwa kuomba ndugu ni hatari mno.

Hutaweza kushinda Vishawishi vinavyokuzunguka hapo kazini kwako vya kuzini,kuiba,kula rushwa nk kama usipokuwa muombaji.

Yakobo 4: 1″ Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?.2Mwatamani wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu KWA KUWA HAMWOMBI.

Hivyo anza kupanga ratiba zako vizuri pata muda wa kuomba utaona unaepushwa na majaribu mengi sana mengine hata hutajua ila ni kwa sababu uliomba Bwana atakuepusha na mengi sana.

Lisaa1 ni dogo sana katika maombi kama ukizama kweli na kugugusa katika kila maeneo katika maisha yako ukiba ukuwaji wako wa kiroho,Ukiombea familia yako nk ni muda mchache.

Usiombe maombi ya kuvalia viatu ya dakika 5 , 10, 20.

Anza kuomba kuanzia leo maombi ni kujizoesha. Hakuna mtu aliepewa karama ya kuomba hii ni kwa wote..

Unataka kusimama na kumshinda ibilisi?, na kufurahia wokovu wako? KUWA MUOMBAJI.

ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *