NI SIRI IPI ILIYOMFANYA  ESTA AKUBALIKE KULIKO MABIKIRA WENGINE?.

Mwanamke No Comments

NI SIRI IPI ILIYOMFANYA  ESTA AKUBALIKE KULIKO MABIKIRA WENGINE?.

(Masomo maalumu kwa wanawake)

Wengi wanadhani ubikira ndicho kigezo cha juu ya kupata kibali… Nataka nikuambie sivyo!.. walijitokeza mabikra wengi mbele ya Mfalme Ahasuero, lakini ni mmoja tu aliyechaguliwa..

Biblia haimtaji Esta kama alikuwa ni mwanamke mzuri kuliko wote waliohudhuria, hapana biblia inasema alikuwa na Uso mwema tu, wala hakutokea katika familia ya kitajiri kama wenzake, wala hakuwa na elimu kama wale wengine pengine ingekuwa chachu ya kumfanya mfalme avutiwe naye lakini vyote hivyo hakuwa navyo. Bali kuna jambo lingine liliomfanya mfalme avutiwe naye.

Sasa ni kigezo gani cha juu kilichompa Esta umalkia??….Turejee maandiko tutapata majibu..

Esta 2:15 “Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, YEYE HAKUTAKA KITU, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.

16 Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake.

17 MFALME AKAMPENDA ESTA KULIKO WANAWAKE WOTE, NAYE AKAPATA NEEMA NA KIBALI MACHONI PAKE KULIKO MABIKIRA WOTE; BASI AKAMTIA TAJI YA KIFALME KICHWANI PAKE, AKAMFANYA AWE MALKIA BADALA YA VASHTI”.

Kama wewe ni mwanamke na unatamani kupata kibali cha ndoa, au kupata mtu sahihi wa atakayekupenda, basi kuwa kama Esta, ambaye alikuwa na tabia ya kutokupenda-penda vitu!…

Esta hakuwa na tabia ya kupenda-penda vitu (kwa ufupi hakuwa na tamaa) na wala hakuwa na mambo mengi!!.. aliingia kwa mfalme yeye kama yeye, katika uhalisia wake!.. wakati wengine walitaka waingie kwa mfalme na marashi yao, na mitindo yao, na wapambe wao, ili wakubalike, Esta yeye hakutaka hayo yote, aliona ni ulimbukeni, aliingia yeye kama yeye, isipokuwa vitu vichache ambaye yule msimamizi aliyeitwa Hegai alimshauri.

Hata leo ni hivyo hivyo, Biblia bado ni Neno la Mungu lililo hai, kupitia hilo tunajifunza kanuni nyingi.. kama wewe ni binti!, au mwanamke!.. ukitaka kibali na Neema.. basi KUWA WEWE!!!… Usianze kujibadili maungo yako, wala sura yako kwa kujipodoa, au sauti, au chochote kile katika mwili wako ambacho umeumbwa katika ualisi wake, vile vile usiwe mtu wa tamaa ya vitu (kila unachokiona unakitamani)..

Ukiwa mtu wa namna hiyo ni rahisi sana kupata kibali.

Lakini kumbuka kibali kinatoka kwa Mungu, na hivyo hatua ya kwanza ya kupata kibali kwa Mungu ni kuokoka yaani kuzaliwa mara ya pili. Na baada ya hapo kuishi maisha ya utakatifu.

Kwa kawaida binti wa Yesu aliyeokoka kweli kweli hawezi kutafuta kibali ya kukubaliwa na mwanaume kwa kujipamba mwili wake kama mabinti wa kidunia, hapana bali atakuwa mtulivu na mwenye heshima na kutunza mwili wake. Kwani anafahamu tumaini la maisha yake yote lipo kwa Bwana, na hivyo atamletea mwanaume anayemfaa kwa wakati wake.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *