Nini maana ya kusali kwa kupayuka payuka?

Maswali ya Biblia No Comments

 

Nini maana ya kusali kwa kupayuka payuka?

Shalom Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo kwa njia ya swali hili.

Maandiko Matakatifu yanatwambia…

Mhubiri 5:2 “….. kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo MANENO YAKO na yawe MACHACHE.”

Sasa Swali letu linatoka hapa ni maneno aliyoyasema Mwokozi wetu mwenyewe..

Mathayo 6:7
“Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya MANENO YAO KUWA MENGI.

8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. “

Ukisoma biblia ya kiingereza inatoa maelezo vizuri juu ya mstari huu..

Matthew 6:7
[7]And when you pray, do not heap up phrases (multiply words, repeating the same ones over and over) as the Gentiles do, for they think they will be heard for their much speaking. [I Kings 18:25-29.]

Unaona hapo anasema “Repeating the same ones over and over” maana yake kurudia kitu kile kile kimoja mara nyingi nyingi sasa hii sio sahihi kabisa kimaandiko na ni makosa mbele za Mungu. kwani tunamfanya Mungu kama kiziwi kwamba hasiki tunapomwomba, ilihali si hivyo.

Neno “kupayuka-payuka” kama ilivyotumika hapo inamaanisha “kurudia-rudia” maneno katika sala, na si kupaza sauti kama wanavyodhani wengi, Bali ni Agizo kama lile tulilosoma kutoka kitabu Cha muhubiri hapo juu, kuwa maneno yetu yawe machache.

Kuhusu Suala la kupaza sauti, usiri au faragha katika Maombi linaongelewa vyema katika mistari ya juu..

Mathayo 6:5-6
5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.

6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”

 

Tunakatazwa kusali kwa kupaza sauti ili kujionesha mbele za watu [unafiki], Bali tufanye kwa Siri maana Baba yetu anaketi sirini; Agizo hili halikatazi kupaza sauti, ila tunapaswa kufanya hivyo tumliliapo Mungu kwa ukweli kabisa na si ili kujionesha mbele za watu.

Kuhusu kurudia rudia maneno tunaweza kuona mifano mingi kama kusali rozari, hufanyika kwa Sala ndefu lakini kibiblia sio sahihi! maana Mungu anazijua haja zetu kabla hatujamwomba.

Ni kosa kufanya hivyo mbele za Mungu maana ni tamaduni za kipagani [gentiles]; sisi tunapaswa tupeleke hoja za msingi mbele za Mungu Kisha tushukuru na kumaliza, kuliko kuomba kwa muda mrefu kwa kudhani kuna fidia juu ya Wingi wa maneno yasiyo maana katika Sala! Kuwa huru na hoja za maana zenye mapenzi ya Mungu, naye Atasikia!

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *