Nini maana ya mna hila nyingi moyoni mwa mtu; lakini shauri la Bwana ndilo litakalo simama.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Yesu Kristo.

Bwana wetu Yesu Kristo anamaanisha kuwa ndani ya moyo wa mwanadamu kuna mawazo mengi ya tamaa ambayo mwisho wa siku hizo tamaa hupelekea upotevu kwamfano mtu atatamani anunue nyumba au awe na mali nyingi ili aweze kuwatendea vibaya wale waliomtendea vibaya wakati Bado hajapata mali na wakati mwingine atahitaji atende ubaya na kuwatesa hata ambao hawajamkosea ilimradi nafsi ya mtu huyo ijiinue na wengine huenda mbali zaidi kwa kutaka kusujudiwa na watu kutokana na mali walizonazo.

Mungu akiona mawazo haya ndani ya moyo wa mwanadamu huwa  anayabatilisha ili lisimame wazo lake pekee ambalo linafaida kwa mtu huyo na mwingine kwakuwa Mungu wetu ni pendo hivyo asingependa kuona mtu yeyote anapotea na kupoteza wengine kwa sababu ya mali hivyo atazuia ubaya usitendeke. Neno la Bwana linasema

Yakobo 4:2 “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!

3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”

Hivyo tunavyopeleka maombi yetu kwa Bwana inatupasa tuwaze mema mioyoni mwetu huku tukiwa na utayari wa kunitumia vile tunavyoviomba kwa Bwana kwa faida ya ufalme wa Mungu na watu wengine ili Mungu anapotupatia aione Imani na yale mema tutakayoyafanya baada ya kupokea tuliyoyaomba kwa Bwana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *