Shalom.
Swali: Mafarisayo walipomwambia Yesu kuwa alitoa Pepo kwa beelzebuli, JE? Alimaanisha Nini alipowauliza JE watoto huwatoa kwa nani?
Tusome..
Mathayo 12:24 “Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.
25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.
26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?
27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, JE! WANA WENU HUWATOA KWA NANI? KWA SABABU HIYO HAO NDIO WATAKAOWAHUKUMU.
28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia”.
Neema ya Mungu ilikuwapo tangu zamani [Agano la kale] lakini haikuwa imefunuliwa, kwa wazi kama ilivyofunuliwa kwetu leo kupitia Yesu Kristo.
Mfano ukisoma Yohana 5, kulikuwako birika Mashuhuri lililoitwa Bethzatha huko Yerusalemu. Ambapo Mungu alikuwa akituma malaika wake, kuyatibua Yale maji na Kisha yule mtu wa kwanza kuingia humo aliponywa na kufunguliwa muda huo huo(matatizo, magonjwa n.k). Tunamwona yule aliyesumbuliwa na Pepo la udhaifu kwa miaka 38, tunatambua ya kuwa lilikuwa ni Pepo la udhaifu kwa maana mwishoni Bwana anamwambia aifanye dhambi tena yasije yakamkuta yaliyo mabaya zaidi kama yale katika Luka 11:24. Hivyo mtu yule angeingia tu kwenye yale maji angefunguliwa.
Huo ni mfano wa njia alizotumia Mungu kuwafungua dhidi ya mapepo wayahudi, zilikuwapo na nyingine nyingi, uthibitisho mwingine ni kuhusu wale wapunga Pepo (matendo 19:13), ambao walikurupuka kulitaja jina la Yesu bila kujua mamlaka iliyo nyuma yake,wakafanya kwa njia zao na wakaharibikiwa!
Tukirudi katika swali letu, mafarisayo walishangaa jinsi Yesu alivyokuwa akiamuru kwa neno moja tu Miujiza inatendeka [uponyaji, kufufua wafu n.k] jambo ambalo ni tofauti na walivyokuwa walifanya wao, ndipo wakang’amua ya kuwa alitumia nguvu za Pepo. Tunaweza kusema kwa lugha rahisi, akawauliza kama Mimi nilitoa kwa beelzebuli JE wanafunzi wenu walitoa kwa nani? Kama ni kwa msaada wa Mungu wa Ibrahim, kwanini mnahitimisha Mimi natoa kwa Beelzebuli? JE Pepo anawezaje kutoa Pepo?Hamjui ya kuwa hao [wanafunzi wao] ndio watakaowahukumu.
Nasi tunapaswa kuwa makini sana, panapofanyika uponyaji wa watu tusiwe wepesi kukimbilia kuhitimisha kuwa zile ni Nguvu za Giza! Maana si Kila anayefanya hivyo ni mchawi au anatumia nguvu za Giza, kwa kuhukumu namna hiyo tutakuwa tunajiweka hatiani wenyewe.
Amen
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.