Nini maana ya nasaba?

Maswali ya Biblia No Comments

Tusome

1 Mambo ya Nyakati 9:1

[1]Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.

Nasaba maana yake ni orodha au mfufulizo wa majina ya watu, ambayo yanakuwa yamejumuisha orodha ya watu watu wote walio katika ukoo mmoja.

Jambo hili pia tunaliona katika kitabu cha mathayo, ambacho kilielezea ukoo wa Yesu kwanzia mwanzo hadi mwisho, tusome

Mathayo 1:1-7

[1]Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.

[2]Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

[3]Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;

[4]Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;

[5]Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;

[6]Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;

[7]Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

Hiyo ndiyo nasaba ya ukoo wa Yesu, Ni nini tunajifunza katika jambo hili

Nasi tunaokoka tunakuwa Moja kwa Moja tunatambulika tu uzao wa Yesu, lakini nasi pia tunapomzalia Mungu matunda nasi tunatengeneza nasaba yetu, ambayo inahifadhiwa huko Mbinguni.

Ni jukumu la Kila mwamini kumzakia Mungu matunda

Yohana 15:1-2

[1]Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

[2]Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *