Jabari ni mtu shujaa asiyeshindwa na jambo lolote pia ni mtu anayejiamini kwa asilimia kubwa sana katika kila alifanyalo na ni mtu hodari sana katika jambo hilo jema au baya alifanyalo.
Tusome maandiko ili tupate kujifunza zaidi.
Isaya 49:24 “Je! Aliye hodari aweza kunyang’anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka?
25 Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye JABARI wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu”.
Pia turejee maandiko haya ya Yesu Kristo yanayoelezea kuhusu mtu hodari ili tupate kujifunza zaidi.
Mathayo 12:29
[29]Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.Luka 11:21
[21]Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama;
Hebu tuone aina za jabali na maana zake kibiblia ili tujifunze zaidi sawa sawa na Bwana anavyotaka tujifunze.
1. Jabari katika kutenda maovu na kumtegemea vitu vya mwilini badala ya kumtumaini Yesu Kristo.
2. Jabari katika kutenda mema yanayompendeza Mungu inayoambatana na kumtegemea Mungu.
Jabari katika kutenda maovu imeelezwa kwa mifano ya watu waliobobea katika kutenda maovu yaliyopitiliza ni hawa wafuatao.
Zaburi 52:1Kwa nini kujisifia uovu, EWE JABARI? Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.
5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
6 Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; 7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. ALIUTUMAINIA WINGI WA MALI ZAKE, NA KUJIFANYA HODARI KWA MADHARA YAKE.
8 Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Jabari katika kutenda mema kama ilivyo ainishwa hapa katika neno la Bwana ambao pia ni jabali katika kuishindania Imani.
Waebrania 11:33 “ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,
34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, WALIKUWA HODARI KATIKA VITA, walikimbiza majeshi ya wageni.
35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;
36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.
39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;
40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.
Mpendwa hivyo inatupasa kuwa majabari katika kutenda mema na pia kuwa kuishindania Imani ambayo ndiyo msingi wetu huku tukiuzidisha upendo amba ndiyo amri kuu tuliyopewa na Bwana Yesu na njia pekee ya kuweka kuwa majabari katika mema ni kwa njia ya kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako, kusoma neno na kuwa ni muombaji.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.