Piga hatua Fikia katika kiwango hiki

Biblia kwa kina No Comments

 

Piga hatua Fikia katika kiwango hiki

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kama mkristo kuna viwango ambavyo unapaswa kuvifikia viko viwango vya namna mbali mbali ambavyo unapaswa kuvifikia lakini kwa leo tutaangalia kiwango au hatua ambayo wewe kwako ni ya muhimu sana kuifikia na kama hujafikia bado utaonekana ni mtoto mdogo/mchanga katika ufalme na kama utakua nim toto mdogo katika ufalme basi jua kabisa huwezi kuuteka ufalme wa Mungu.

1.Kutokuangushwa/kufata madhaifu wa kiongozi wako.

Ni jambo ambalo linaonekana kuwa ni dogo au haliwezekaniki lakini ukweli ni kwamba wako wakristo wengi sana wanaangushwa na kurudi nyuma kwa sababu ya madhaifu flani ambayo kingozi huenda yameonekana kwake na bila kufahamu kama yeye pia ni mwanadamu kuna mahali atakosea. Tutaangalia ni kwa namna gani katika hili.

Ukweli ni kwamba kuna mambo yanaweza kuonekana kwa kiongozi na watu imara tu waliokua/Matured/waliosimama imara ndio wanaweza kuendelea kusimama lakini Pamoja na kuomba juu yake lakini kwa watu ambao ni wachanga/Watoto wadogo katika ufalme wa Mungu hao badala ya kusimama kumuombea kiongozi wao wanakuwa ni watu wa kwanza kuanza kumtangaza na kumsema vibaya lakini hawaishii hapo tu bali pia na wao wanaingia katika mstari huo huo tena.

Umewahi kusikia kauli hii kwa mshirika mwenzako anasema “kama mchungaji amefanya hivyo mimi ni nani?” ukisikia kauli ya namna hii kwa mshirika mwenzako jua kabisa yeye ni mtoto unaezungumza nae au kama ni wewe basi jua kuna hatua ambazo unahitaji kuzifikia.

utakuta ni mmshirika lakini hata anapooona wenzake wameanguka mahali fulani ama wanamadhaifu fulani badala ajifunze kupitia wao ili yeye naye asiwe kama wao lakini awekeze muda mwingi katika kuwaombea mtu huyo nae anafata nyendo zilezile kwa kusema “kila mtu anafanya hata na mimi nikifanya ni sawa tu”

anashindwa kujitofautisha na kuwa msingi wa wa kuwaombeawengine na zaidi anaanza kusambaza kwa wengine ukijiona ni Mkristo uko namna kama hii ndugu yangu wewe ni mtoto na kama utaendelea kukaa hapo hutakua na wala hutaona uhalisia wa Mungu akijidhirisha katika maisha yako.

Kristo anatamani tufikie hatua ambayo sisi tunaweza kusimama kwa ajili ya watu wanaotuchunga kama kuna mahali adui wamempa nafasi katika utumishi basi sisi tusiwe wepesi wa sisi kuanza kuwasema na kufikia hatua ambayo sisi tunatumia udhaifu ule walionao na sisi kujifariji kwa wao wamekosa vile basi na sisi tunaweza tukafanya hivyo jambo ambalo sio sahihi kabisa.

Mwanandishi wa kitabu cha Waebrania anawaandikia waebrania juu ya wao kuwaombea ili wazidi pia kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote maana yake wasifanyike kuwa chanzo cha watu wengine kuanguka kwa sababu ya mahali fukani ambapo hapajakaa sawa.

Na ndio maana katika nyaraka nyingi Paulo anazungumzia juu ya tabia au kiongozi ni namna gani anavyopaswa kuenenda.

Waebrania 13:18 “Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.”

Pia kama kiongozi pia unawajibu wa kuhakikisha pia huwi kikwazo au chanzo cha watu wengine kuanguka au kupita katika makosa yako kwa sababu wamekuona umefanya kitu Fulani kuwa na mwenendo bora ili hata wale wachanga wanapokuona nao watamani kuwa kama wewe. Ikiwa ni kionozi wa vijana, askofu,mchungaji,shemasi, mzee wa kanisa nk uongozi ni dhamana na watu wengi wanaimarika kupitia wewe lakini wtu wengi wanaanguka pia kwa kupitia wewe hapo kama mwenendo wako ukiwa sio mzuri.

1 Timotheo 4:12 “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;”

Ukisoma pia…

2 Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”

Hivyo kama kiongozi una wajibu huo na wewe mshirikika una wajibu wa kuwaombea viongozi wako na sio kuwasema na kuwatangaza kila mahali na kutumia udhaifu wao na wewe kufanya hivyo kwa kisingizio kwamba “kama kiongozi kafanya hivyo ama yuko vile mimi ni nani?”

Jenga tabia ya kusimama na kuomba na kuhakikisha viongozi wako wanakua salama maana wanawindwa na adui zaidi ya unavyofikiri maana adui amewekeza nguvu kubwa kwao akijua kabisa akifanikisha kuwaangusha wao Kundi kubwa litaanguka pia.

Muombe Mungu akupe neema ya kusimama imara

naranatha

mawasiliano:0613079530

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *