ROHO YA YEZEBELI IMEBEBA KIBURI

Biblia kwa kina No Comments

ROHO YA YEZEBELI IMEBEBA KIBURI.

Tabia nyingine ya hii roho ya Yezebeli ukiacha uzinzi, uchawi na unabii wa uongo, tabia nyingine aliyobeba ni kiburi.

Roho ya YEZEBELI ina tabia ya kushindana na Roho ya kweli ya Mungu.. Ndio maana utaona Malkia Yezebeli katika Uzinzi wake, na uchawi wake na unabii wake wa uongo, hakuwahi kamwe kupatana na Nabii Eliya, wala kujinyenyekeza kwake..zaidi sana utaona Yezebeli baada ya kusikia ishara Eliya aliyoifanya ya kushusha moto na kuwaua manaabii wake wa baali, aliapa kumlipa kisasi Eliya, na wala hakumwogopa hata Mungu. (Ni roho ya kiburi).

Roho hii ikishakita mizizi ndani ya mtu, inamfanya kuwa na kiburi, na mkatili hususani katika watumishi wa kweli wa Mungu, na inakuwa inamfanya mtu kuichukia njia ya kweli na watumishi wa Mungu wa kweli.

Angalia leo wanawake wanaojipamba kwa mapambo ya Yezebeli, utaona hiyo roho ya kiburi imewavaa, utaona wakihubiriwa waache mapambo hayo ya kipepo..wanashindana na Neno la Mungu, wanaipinga njia ya kweli…sio jambo la kawaida ni roho ya kiburi tayari imewavaa.

Dada/mama jivue roho ya UYEZEBELI.. Mvae BWANA YESU (Warumi 13:14). Hizi ni siku za Mwisho na Bwana YESU anarudi.

Unajivua roho hii ya shetani kwa kuamua kuondoa mapambo yote katika mwili wako kuanzia kichwani mpaka miguuni… yaani unaondoa hizo nywele bandia ulizoweka kichwani/wigi na unafumua nywele zako ambazo umesuka unaacha kama ilivyo, lakini pia unavua mabangili, hereni, vipini, wanja, mekaups, lipsticks, kucha bandia/rangi bandia ulizopaka kwenye kucha za miguuni na mikononi.

kwanini ubadilishe rangi ya kucha uliyopewa, kwanini ubadilishe ngozi yako uliyopewa, kwanini ubadilishe nywele zako na kusokotasokota, kwanini utoboe toboe masikio na pua zako ambao umeumbiwa pasipo tobo lolote.. huoni kuwa unashindana na Muumba wako.(kiburi) Na biblia inasema katika..

Isaya 45:9 “Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?”

Hivyo, hebu amua kuvua roho ya Yezebeli kwa kuondoa hayo mapambo na mavazi yote ya kikahaba (vimini, suruali aina yoyote iwe pana au ya kubana, magauni ya kubana, nguo zinazochora maungo yako au zile zinazoacha maziwa/kifua wazi, mgongo wazi hayo ni mavazi ya kikahaba..ni mavazi ya Yezebeli mwanamke kahaba, kwahiyo amua kubadilika na kuwa mkristo wa kweli.

Mkristo wa kweli ni yule aliyejikana nafsi na kuacha kufuata mitindo na kanuni ya ulimwengu huu.

Tafuta magauni marefu yasiyobana na ubaki na muonekano wako ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani waliokuwa wanaukiri uchaji wa Mungu.

1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

1Petro 3:3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

Lakini kama usipotaka kusikia, ukaendelea kufuata njia ya ulimwengu na kukubaliana na kanuni za ulimwengu huu na roho ya Yezebeli ambayo inaendesha ulimwengu na kuchafua kanisa la Mungu basi fahamu leo mapema kuwa Jehanumu ipo kwa watu wa jinsi hiyo…na muda wowote unaweza ukajikuta upo huko na kule utakuwa katika majuto ya milele utakumbuka jinsi ulivyokuwa unahubiriwa ubadilike lakini utakuwa umechelewa.

Muda wa kutubu na kuamua kubadilika ni leo…usiangalie wingi wa watu wanaoipinga njia ya kweli, kwa maana njia iendayo uzimani ni nyembamba na ni wachache ndio wanaiona (Mathayo7:13-14).

Maran atha (Bwana Yesu anarudi).

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *