Sifa kuu ya kanisa la Kristo
Shalom: Jina la Bwana Yesu Kristo libarkiwe.
Leo tutaangalia sifa kuu tano za kanisa la Kristo ambazo kanisa la Mungu liwapo mahali popote linapaswa liwe nazo.
Hii ina maana kuwa kila unapoingia ndani ya kanisa la Kristo mahali popote ni lazima ukutane na sifa hizi tano vinginevyo hilo sio kanisa la Kristo bali ni sinagogi la shetani.
Kumbuka kanisa la Kristo sio dhehebu fulani au kikundi fulani cha wanaharakati, bali ni watu wa Mungu (watakatifu) walioitwa na kuoshwa dhambi zao, na hivyo wanamwabudu Mungu katika Roho na kweli na sio katika mapokeo na liturujia.
1: Mionekano ya wanawake.
Wanawake kufunika vichwa.
Ndani ya kanisa la Kristo, wanawake wanapaswa washike maagizo ya Kristo yote ikiwemo kufunika vichwa wakati wowote wa ibada kwa ajili ya ishara ya kutawaliwa na waume zao na kwa ajili pia ya malaika.
1 Wakorintho 11:5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
[6]Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
[10]Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
Hivyo ukiingia kwenye kanisa lolote la Kristo, sharti ukute wanawake wamefunika vichwa vyao, tofauti na hapo hilo sio kanisa..haijalishi lina watu wengi kiasi gani.
. Wanawake wawe wamejistiri ipasavyo.
Wanawake wa kikirsto wanapaswa kujistiri kwa mavazi ya heshima na ya adabu kama wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
1 Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Hivyo ukiingia ndani ya kanisa lolote ukakuta wanawake wamevaa mavazi ya aibu, mfano nguo fupi, suruali, na zile zinazochora maumbile/zinazobana au kuacha baadhi ya sehemu za mwili wazi, ujue hilo sio kanisa bali ni nyumba ya makahaba… kwasababu hayo ni mavazi ya kikihaba (Mithali 7:10).
Mwanamke wa kikirsto iwe ni kanisani au nyumbani..sharti avae gauni au sketi ndefu mpaka visigino na isiyobana, na nguo isiyoenyesha maziwa yake au mgongo wake..huko ndiko kujistiri.
. Wanawake wa kikirsto hawapaswi kujipamba kwa nje.
1 Petro 3:2 Wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.
[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
Mwanamke wa kikirsto kutotumia mapambo ya kidunia kama hereni, bangili, vipini, mekaup, lipustiks, wanja, wigi, kusuka, kucha bandia, na rangi ya kucha sio sheria bali ni agizo la Kristo kwa kanisa lake duniani kote.
Na kanisa la Kristo mahali popote lilipo, wanawake wanapaswa wawe wanalitii hilo agizo la kutojipamba kabisa..tofauti na hapo bado hilo kanisa linakunyanzi na Kristo haliwezi kulichukua.. maana anakuja kuchukua kanisa lisilokuwa na mawaa wala kunyanzi (Waefeso 5:27)
2: Uongozi madhabahuni.
Kanisa la kweli la Kristo..linapaswa lisimamiwe na Askofu jinsia ya kiume na mchungaji jinsia ya kiume kulingana na utaratibu ambao Roho Mtakatifu aliiweka ndani ya kanisa.
1 Wakorintho 14:34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
Hii haimanishi mwanamke asiwe na wajibu wowote ndani ya kanisa, hapana anaweza akafanya kazi zingine tu nyingi kulingana na huduma aliyopewa na Bwana, lakini huduma inayohusisha kufundisha na kumtawala mwanamume..hapaswi kujihusishanayo, hata kama anajiona kuwa anaweza kufanya hivyo, anapaswa atii Neno la Mungu na wala sio msukumo wake.
Katika siku hizi za mwisho, shetani anawadanganya sana wengi kuwa mwanamke anaweza akawa sawa na mwanamume, hivyo mwanamke kuwa mchungaji ni sawa, kanisa la Kristo halina huo utaratibu..bali linaongozwa na Roho Mtakatifu katika ukamilifu wote wa maandiko.
Kwahiyo kanisa linaloongozwa na wanawake wanaojihita ni wachungaji, hilo sio kanisa la Kristo bali ni mahekalu ya mpinga Kristo, hata kama miujiza mingi inatendeka na watu wanashukiwa na nguvu za Mungu..na kupona, hayo hayawezi kubatilisha Neno la Mungu..na ndio maana wengi watakataliwa siku ile.
1 Timotheo 2:11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
3 Ubatizo sahihi.
Ubatizo sahihi kulingana na biblia, ni ule wa kuzamishwa ndani ya maji mwili mzima, kama Bwana Yesu alipotoa kielelezo akafunga safari kutoka Galilaya zaidi ya kilometa mia mpaka Yordani ili akabatizwe kwa kuzamishwa kabisa ndani ya maji. (Mathayo3:13-16), na pia tunaona Yohana Mbatizaji akibatiza kule Aiononi kwasababu huko kulikuwa na maji tele,
Yohana 3:23 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.”
Angeweza tu kutumia maji ya karai au kidumu kimoja kingetosha kuwanyunyizia hao watu.. lakini ubatizo kama ilivyo tafsiri yake ni kuzamisha na wala sio kunyunyiza..na huo ndio ubatizo sahihi wa kibiblia huo mwingine unatoka kwa aduni.
Na sio tu kuzamishwa basi, bali ni kwa kutamkiwa jina la Bwana Yesu Kristo na sio majina mengine…vinginevyo huo ubatizo ni batili.
Kanisa la kwanza .. watu wote waliosikia injili na kutubu dhambi zao, walibatizwa kwa JINA LA YESU KRISTO. Soma matendo 2:38, Matendo 10:48, Matendo 19:5.
Jina la Yesu Kristo ndio jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu..soma biblia vizuri kwa uongozo wa Roho Mtakatifu.
Usikubali kuchukuliwa na upepo wa kila namna, na hila za ibilisi,
Kwahiyo hizo ndizo sifa kuu tatu za kanisa la Kristo, ambayo wewe mtu unayeishi Afrika..ukienda Amerika,au Ulaya au Asia ni lazima ulikute kanisa la Kristo likiwa na hizo sifa na zingine nyingi ambazo zinaendana na biblia.
Je! Kanisa ulilopo lina hizo sifa? Kama jibu ni hapana, basi huwenda shida ipo kwako au mahali uliko..yamkini hilo ni sinagogi la shetani, au ni wewe pengine umemzimisha Roho Mtakatifu au hujawahi kumpokea kabisa.
Hivyo nakusihi kabla hujatafuta kanisa sahihi, tafuta kwanza kujazwa Roho Mtakatifu, ambao unakuja kwa wewe kudhamiria kutubu dhambi zote na kuacha ulimwengu yaani kujikana nafsi kabisa na kukubali kumfuata Kristo bila kujalisha gharama yotote..na hapo ndipo utaweza kufuta Roho Mtakatifu aingie ndani yako na kukuongoza katika njia ya kweli.
Kumbuka biblia inasema mtu awaye yoye asipokuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake. Kasome Warumi 8:9
Tunaishi ukiongoni mwa siku za mwisho, Bwana Yesu yupo milangoni kurudi.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.