Bwana alimaanisha nini aliposema ”viuno vyenu viwe vimefungwa na taa zenu ziwe zinawaka?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana alimaanisha nini aliposema ”viuno vyenu viwe vimefungwa na taa zenu ziwe zinawaka?

Jibu: Tusome

Luka 12:35 “VIUNO VYENU NA VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA.

[36]nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.

[37]Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

[38]Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.

Ili tuelewae vizuri turudi katika Agano la kale, Je umewahi kutafakari ile habari ya wana wa Israeli wakati wanatoka Misri, Kwa kuwa hatuna muda wa kuelezea matukio yote lakini tunafahamu siku ile ya mwisho ya wao kukaa katika nchi ya Misri Mungu aliwapa maagizo, na ikumbukwe kuwa hawakutoka nchi ya Misri MCHANA, hapana bali ilikuwa ni USIKU wa manane kwasababu ndio uliokuwa mpango wa Mungu watoke usiku.

Aliwapa maagizo na maagizo na mojawapo ya maagizo hayo ilikuwa ni KUFUNGWA MKANDA VIUNONI na KUVALIWA kwa VIATU. Tunafahamu mtu akienda kulala ni lazima azilege nguo zake, atoe mikanda kisha azime taa na alale. Lakini kama nguo zako bado zimebanwa na mkanda pamoja na viatu ni wazi kuwa mtu huyo yupo katika mazingira ya kutoka muda wowote.

Hata wewe, kama una safari ambayo unaamkia alfajiri, ni lazima utajiweka sawa usiku, utajipanga kwa ajili ya safari ya kesho..si ndiyo.

Huwezi kuamka na kuanza kutafuta soksi mahali zilipo, au kama ni kuandaa nguo, nauli, viatu, na vitu vya muhimu vinavyoitajika kwenye safari, ni lazima tu utandaa kabla ya muda wa safari, vinginevyo utaachwa na usafiri.

Lakini wana wa Israeli walipoambiwa wajiweke tayari kwaajili ya safari ya kesho, hawakujua uzito wa wao kuambiwa hivyo, mpaka tunavyosoma pale Farao na wamisri wote wakiwafukuza wenyewe kutoka Misri pamoja na zawadi nyingi usiku ule ule, hapo ndipo walipotambua kuwa kumbe! KUVAA KULE NDIO ILIKUWA NI KUONDOKA! Wengine waliwaza mbona! imekuwa Ghafla ghafla tu, hili jambo si lingesubiria walau asubuhi tu, tuanze kuweka vitu vyetu vizuri, tuwaage majirani zetu, tuwafuate wadeni wetu watulipe kwanza?, tukavune ngano zetu tupate chakula cha kusafiria? Nk. Lakini mbona jambo hili Mungu kaliharakisha mapema hivi?….Tunasoma usiku ule ule safari ilianza (Kutoka 12), lakini jaribu kifikiria kama mwisraeli mmoja asingetiii yale maagizo na kwenda kuamua kujifungia ndani kwake na kuvua nguo zake na kulala, unadhani atakapoamka ni jambo gani atakutana nalo?, WENZAKE HAWAPO!!. Na ndivyo itakavyokuwa katika siku hizi za mwisho Bwana alisema.

Luka 12:35 VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka;

36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.

37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.”

Kwahiyo, Bwana aliposema ‘viuno vyenu viwe vimefungwa” alimaanisha tuwe tayari kwa ajili ya ile siku ya kuondoka hapa duniani na kwenda kwenye karamu yake aliyoenda kuiandaa. Kumbuka andiko hili linahusu tu bibi arusi safi wa Kristo basi!. Ndio anambiwa awe tayari, awe amejifunga vazi la bibi arusi (utakatifu).

Ndugu siku ya kuondoka kwa wana wa Mungu hapa duniani hakutakuwa kwa kukutazamia kama wengi wanavyodhani. Utakuwa ni wakati usiofaa kwa wengi hata katikati ya watumishi wake waaminifu.

Bwana alipotupa maagizo kwamba TUKESHE, TAA ZETU ZIWE ZINAWAKA na VIUNO VYETU VIWE VIMEFUNGWA. Alijua kabisa itakuwa ni wakati wa usiku wa manane ndio muda utakuwa wa kurudi kwake . Na sasa ndio tupo hicho kipindi ambapo dunia ipo katika kilele cha giza kuu kuliko hata vizazi vyote vya nyuma vilivyotutangulia. Maovu yameongezeka kuliko hata kipindi cha Sodoma, ushoga unahalalishwa hata mahali patakatifu. Hizo ndio dalili madhubuti kuonyesha kwamba tupo katika giza nene la usiku wa manane.

Lakini kumbuka pia Bwana wetu yupo karibu kurudi kutoka katika arusi ya faragha aliyoalikwa na BABA yake mbinguni. Na watakaokwenda naye ni wale tu ambao TAA zao zinawaka na VIUNO vyao vimefungwa, yaani wale ambao kila siku macho yao yapo mbinguni. Biblia inasema “jifungeni KWELI kiunoni” na kweli ni NENO LA MUNGU (Waefeso 6:14). Hivyo wale wote wataokadumu katika msingi ya Neno la Mungu wakielekeza macho yao mbinguni bila kujali mambo yanayopita ya ulimwengu, kadhalika pia wale ambao TAA zao zinawaka, kumbuka ili taa iwake inahitaji mafuta, na mafuta ni ROHO MTAKATIFU, Hivyo wale ambao waliotajazwa Roho na kila wakati wanaufanya uteule wao na wito wao imara bila kumzimisha Roho wa Mungu ndani yao, hao ndio siku ile BWANA atakapogonga watamsikia na kuingia kwenye Karamu aliyoiandaa yeye mwenyewe. Na pia ili taa iwake lazima kuwe na giza, taa haiwezi kuwashwa wakati wa mchana, hivyo wakati huu ambapo dunia imejaa matendo ya giza, ndio wakati wa kuzifanya taa zetu ziwake

Lakini wengine wote waliosalia, wapendao matendo ya giza hawatajua lolote, itakapopambazuka tu ndipo watakapogundua kuwa wenzao hawapo, na ndiko kutakako kuwa na kilio na kusaga meno. Katika dhiki kuu, na katika siku ile ya BWANA.

Ni kwanini leo maisha yako yasiuhakisi wokovu?, Ni kwanini bado upo usingizini?. Na uzingizi hauna nguvu mchana,JE! Unao huhakika hata Bwana akija leo, utakuwa mwepesi kumsikia akigonga mlango wa moyo wako?, Mambo ya ulimwengu huu yanakusonga?, Unawatazama wanadamu? Hao watakusaidia nini endapo umesikia unyakuo umekupita, ? na wewe umebaki? ujana wako, mali zako na nguvu zako zitakuwa msaada gani kwako katika siku hiyo?

BWANA ANASEMA..

Waefeso 5:14 “……AMKA, WEWE USINZIAYE, UFUFUKE KATIKA WAFU, Na Kristo atakuangaza.

15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16 MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU.”

Kama haujatubu ndugu fanya hivyo sasa, huu si wakati wa kuishi maisha ya kubahatisha, UKOMBOE WAKATI! nenda ukabatizwe katika ubatizo ulio sahihi wa maji mengi katika jina la YESU KRISTO haraka baada ya kutubu dhambi zako ili upate ondoleo la dhambi (Matendo 2:38) …Kumbuka kuzaliwa mara ya pili ni kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho, na kuishi maisha matakatifu katika Kristo, na si vinginevyo. Ikiwa bado hujapitia hatua hizo zote hapo bado hujazaliwa mara ya pili. Na Bwana alisema mtu wa namna hiyo hawezi kuuona ufalme wa mbinguni (Yohana 3:5).

Fanya bidii utubu na Bwana atakuangazia neema yake.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *