SIFA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU....

Sifa ni kitendo cha kumshuhudia Mungu, au kuyasimulia matendo makuu ambayo ameyafanya au aliyonayo, na sifa huwa inaambata na mguso wa ndani unaomfanya mtu arukeruke, acheze, afurahie, aimbe, ashangalie, apige kilele kwa nguvu, kwa hayo aliyoyaona kwa Mungu wake…

Kwamfano tunapoona jinsi, mbingu na nchi, jua na mwezi, na milima na bahari, vilivyoumbwa kwa uweza na ukuu wa ajabu, hapo tunapata sababu ya kumshuhudia Mungu, au kumtangaza kwa namna zote aidha kwa kumwimbia, kushangalia kwa sauti ya juu,

Au labda ulikuwa na shida Fulani labda ugonjwa, ukaponywa, au hitaji la kazi, nyumba, chakula ukapatiwa na yeye. Hapo ndipo unapopata sababu ya kuyatangaza maajabu yake, kwa kumwimbia kwa nguvu sana. Hizo ndio sifa.

Mungu anasema.

Zaburi 68:32 “Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo”.

Zaburi 117:1 “Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidini.

Zaburi 147:1 “Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu, Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri”.

Biblia inatuambia viumbe vyote na uumbaji wote, vinamsifu Mungu. Kwanini na sisi tusimwimbie yeye sifa zetu?.  Embu tazama pumzi uliyopewa bure, embu tazama mapigo ya moyo yanayodundishwa ndani yako bila tozo lolote, embu tafakari jua unaloangaziwa na Yehova. Kwanini usimsifu yeye?

Bwana anaketi juu ya sifa.. (Zaburi 22:3), Na yeye pekee ndiye anayestahili kuabudiwa.

Hivyo wote wamsifuo kwa Roho na Kweli, yeye yupo juu yao. Katika sifa kuta za Yeriko zilianguka, , \vifungo vya Gereza vililegezwa Paulo na Sila walipokuwa gerezani, katika sifa maadui waliuliwa bila vita yoyote kipindi cha Mfalme Yehoshafati.  Nasi pia tukiwa watu wa sifa, ni maombi tosha ya kutuweka huru na kutufungua.

Bwana atupe macho ya kuliona hilo.

Shalom.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *