Tafuta kukaa uweponi mwa Mungu daima.
Shalom! Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Uwepo wa Mungu upo pamoja nasi siku zote na kila mtu alieokoka anao uwepo wa Mungu kwa sababu anae Roho wa Mungu ndani yake.
Lakini si kila Mkristo anakaa ndani ya uwepo wa Mungu, uwepo wa Mungu tunautafasiri kwa namna tofauti kabisa na jinsi ulivyo, watu wengi wanafikiri uwepo wa Mungu ni hali fulani ambayo ni ya kitofauti sana yaani mtu akishaingia kwenye uwepo wa Mungu basi inavyotafasirika labda mpaka mazingira nk vinavadilika au anakuwa sehemu nyingine labda kama Paulo alivyochukuliwa mpaka mbingu ya tatu basi hapo alikuwa uweponi mwa Mungu au alikua katika Roho nk.
” Uwepo wa Mungu ni pale unapofanya shughuli za ufalme au jambo lolote linalomhusisha Mungu moja kwa moja hapo unaruhusu Mbingu kushirikiana na wewe”
Twende pamoja utaelewa zaidi unapoendelea kusoma..
Lakini sivyo kwa namba moja tunaweza kusema hizo ni sehemu moja wapo za kuwa uweponi mwa Mungu lakini ukweli ni kwamba ni zaidi ya hapo.
Watu wengi wanatamani kukaa uweponi mwa Mungu lakini wanaishia kutamani tu! Na hakuna kitu kingine zaidi na wanakua hivyo miaka nenda rudi.. wakifikiri kwamba ipo siku tu watajikuta wanakaa au wapo katika uwepo wa Mungu na watamfurahia Mungu lakini sivyo kabisa kama utaendelea kukaa hivyo daima hutaweza kuona utaishia kutamani tu.
Sasa mwandishi wa Zaburi nyingi yaani Daudi kuna jambo analizungumza hapa..! Ambalo natamani tujifunze na kuangalia maisha kwa uchache ya Daudi.
Zaburi 27:4
“ Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta , Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.”
Soma hapo maneno ya kwanza hapo anasema “ Neno Moja nimelitaka kwa Bwana…” unaona hapo? Kwamba kuna jambo moja amelitaka kutoka kwa Mungu! Lakini hajaishia kusema hivyo tu basi lakini angalia anaendelea kusema…. “.. ndilo nitakalolitafuta ,” unaona? Ndilo nitakalolitafuta, maana yake hajaishia kutaka tu lakini imembidi pia atafute jambo hilo nalo ni lipi??
…” Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.”
Akae nyumbani mwa Mungu siku zote za maisha yake na anasema na kutafakari hekaluni mwake kumbuka ( wakati Daudi anazungumza jambo hili Hekalu lilikua bado halijajengwa kabisa maana alikuja kulinga Sulemani baada ya baba yake Daudi kufa)
Hivyo hekalu linalozungumziwa hapo alikuwa anamaanisha uweponi mwa Mungu kwa kiingereza wameandika”God’s Presence..”
Kwa kutafakari neno la Mungu. Anasema autazame uzuri wa uso wa Mungu hamaanishi kwamba Daudi alikua anaangalia uso wa Mungu kabisa hivi kama Musa la!, bali alikua ni mtu ambae anauona uzuri wa Mungu kwa kukaa na kulitafakari neno kwa muda mrefu.
Vivyo hivyo watu wengi wanatamani na kuomba sana kwamba “ Mungu jidhihirishe kwangu nataka nikuone,nikuelewe,nikufate nk”
Ndugu yangu Mungu ameshajidhirisha tayari katika Neno lake na hawezi kujidhihirisha nje na neno lake( Wanaotafakari na kutendea kazi neno ndiowanaoona Mungu akijidhirisha kwao).. maana yake kumuelewa Mungu inahitaji utafakari Neno lake na upate kilichoko nyuma ya hayo maandishi unayoyasoma yaani ufunuo kupitia Roho Mtakatifu.
Sasa kukaa uweponi mwa Mungu Daudi alifanya hivyo na alikua analazimika kuacha shughuli zake(kusitisha mambo yake kwa Muda ili kupata kuwa karibu na Mungu au kuingia uweponi mwa Mungu).
Ijapokuwa Daudi alikua ni mfalme,mtu wa vita wanazuoni wanasema Daudi alipigana zaidi ya vita 66 mpaka 100 na hakuna vita aliyoshindwa lakini vita vilivyo rekodiwa na biblia ni 12 hadi 15.
Pamoja na yote haya daudi alikuwa ni mtu ambae anatafuta sana kukaa uweponi mwa Mungu na alifanikiwa kwa sehemu kubwa sana..
Zaburi 119:164
“ Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yako.”
Mara sababa haimaanishi moja kwa moja kwamba alikuwa kila siku anamsifu Mungu mara saba la!(anahesabu ya kwanza mpaka saba) Bali jambo hili linaonyesha kuwa Daudi kila siku alitenga nyakati nyingi kumtukuza na kumtafakari Bwana. (Huku ndio kukaa uweponi mwa Mungu)
Ili kuelewa hili Tusome tena Zaburi moja…
Zaburi 55:17
“ Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.”
Tunaona maisha ya Daudi hapa bidii aliyokuwa nayo kuonyesha Asubuhi,Mchana na jioni alikuaa na nyakati nyingi za kumtafakari Mungu na kumtukuza Mungu.
Hii haimaanishi Daudi hakuwa na kazi nyingi alikuwa nazo nyingi kuliko mimi na wewe kama Danieli nae alikuwa na tabia hii Mara tatu kwa siku.
Daudi aliona neno la Mungu, sheria zake na haki zake kuwa za thamani, na hilo lilimpelekea kumsifu Mungu kila wakati. Lakini kupitia kukaa uweponi mwa Mungu..
Kukaa uweponi mwa Mungu ni kusoma neno(kutafakari, kumsifu Mungu sio lazima ucheze hata unapokua kazini kwako haikuzuii kumsifu Mungu, kumtafakari Mungu) pamoja na maombi na wala kukaa uweponi sio kuomba Mungu naomba nikae uweponi mwako halafu hufanyi haya mambo hutaona uzuri wa Mungu kamwe.
Je! Unatenga muda hata wa lisaa,masaa mawili mpaka manne kwa muda wote wa saa 24 kupata nafasi ya kumshukuru Mungu, kumtafakari Mungu nk baada ya shughuli za kutwa nzima? Au ukitoka kazini unausikiliza Mawili unakwabia “ umechoka sana huwezi kwa leo pumzika kidogo”
Biblia imetumia watu ambao walikua na majukumu makubwa(si ambao walikua hawana kazi, tafuta watu wote kwenye maandiko waliofanya mambo makubwa na Mungu) walikua ni watu wa majukumu mengi katika ngazi za kitaifa(ufalme) na walihakikisha wanapata Muda wa kusoma Neno,kuomba,kumtafakari Mungu nk mimi na wewe tunataka tuwe kama hawa watu…
Mungu atutumie kama wakina Paulo,Musa,Mitume nk lakini tutafakari je tunalipa gharama ya kuhakikisha tunakaa uweponi mwa Mungu angalau hata kwa masaa2 ndani ya masaa 24? Kama sivyo tujitafakari upya na kuhakikisha tunatengeneza mahusiano ya karibu na Mungu kuhakikisha tunapata muda wa kusema nae kila siku kwa muda wa masaa 3 hadi 6 kwa nyakati tofauti tofauti tumia masaa 18 au 20 kwa siku hayo yanayobaki mpe Yesu..
Yeye ndio chanzo cha uhai wetu, ndio chakula chetu,ndio uzima wetu, tafakari kwa siku nzima hauko karibu na uzima wa mwili wako ambacho ni chakula mwili utakua katika hali gani?
Mwili ili uendelee kuwa na nguvu umetengenzwa kwa namna ya kula kila wakati(kila siku) ili nguvu ziendelee na ndivyo ilivyo hata mtu wa ndani chanzo chake ni Mungu ili endelee kuwa na nguvu zaidi ni lazima akae karibu na chanzo cha uhai na uzima wake ambae ni Mungu, kupitia maombi,Neno nk.
Bwana Yesu akubariki sana.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.