Tafuta kwa bidii kuwa na nguvu za rohoni.
Shalom, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Ili Mkristo aweze kuleta mabadiliko kwake yeye,kwa jamii inayomzunguka na katika ufalme wa Mungu katika mambo ya Muhimu sana anatakiwa kuwa nayo basi ni kuwa na nguvu nyingi za rohoni.
Nguvu za rohoni ndio zinazoweza kubadilisha na kuamua mambo katika ulimwengu huu wa damu wa damu na nyama.
“ Ulimwengu wa roho una nguvu kushinda ulimwengu huu tuliopo, ule hauna mipaka na ni zaidi ya upeo wetu ikiwa mwanamini atafanikiwa kuelewa na kuweza kupata access basi hawi Mkristo wa kawaida tena”_
Mtu mwenye nguvu nyingi za rohoni anaweza kuleta mabadiliko na kuamua nini kitokee kutokana na mamlaka aliyonayo.
Wakristo wengi wanafikiri na kuishi katika mtazamo kwamba nguvu za rohoni au mabadiliko/ukuaji wa kiroho unakuja tu baada ya kipindi fulani, jambo ambalo si kweli. Nguvu za rohoni zinatafutwa tena kwa bidii si kwa ulegevu lazima ukubali kujitoa ili kufanikiwa kuwa nazo haziji tu la!.
Nguvu za rohoni ni nini? _Ni mamlaka ya Ki-Mungu ndani ya mwamini yanayomuwezesha mwamini kutawala/kumiliki katika ulimwengu wa roho na kuleta matokeo katika ulimwengu huu wa damu na nyama._
Mabadiko yanasema sisi ni watawala/tumepewa kumiliki ni kweli kabisa jambo hili lakini pasipo nguvu hatuwezi kutawala tutakuwa na majina ya kutawala kweli lakini ndani yake hakuna nguvu na mtawala siku zote lazima awe na nguvu ili aweze kumiliki mahali fulani. Pasipo nguvu ni sawa na bure.
Nguvu za rohoni sio zawadi au unapokea tu kama neema ya wokovu(tumepewa hivi vyote kwa neema lakini inahitajika bidii kutawala haihitajiki nguvu wala bidii kumuamini Yesu na kupata msamaha wa dhambi ni bure hakuna gharama yoyote tunalipa.)
Na ukweli nguvu hizi ziko ndani ya kila mwamini lakini ili ziweze kuleta mabadiliko inahitajika kuingia gharama ili kuziona katika uhalisia zipo kanununi na kuzifata kanuni hizo kuna gharama ni sawa na kufata kanuni za asili za kidunia zina gharama zake).
Maandiko yamesema ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu..
Mathayo 11:12
“ Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”
Maana yake wanyonge wataendelea kuwa ombaomba tu(kuuteka ufalme wa Mungu ni kufanya mbingu ikuhudumie)
Hebu tafakari ikiwa ufalme wa Mungu anaetupenda na kutujali na aliekufa kwa ajili yetu kwa nini isingekuwa free tu kuuteka ufalme wake? Vipi kuhusu ulimwengu wa giza ulio kinyume na sisi?(hii inamaanisha ukiweza kuuteka ufalme wa Mungu usiotetemeshwa basi unaweza kuuteka ufalme wa giza kwa sababu ufalme wa giza hauna nguvu kama ufalme wa Mungu.)
Tutaagalia mifano ya watu wachache waliofanikiwa kuwa na nguvu za rohoni wapo wengi tutaangalia wawili tu.
1.Yohana Mbatizaji.
Kama hufahamu Yohana Mbatizaji hakufanya muujiza wowote, biblia haija rekodi mahali popote, hakuponya wagonjwa, hakutoa pepo nk na injili yake ilikuwa ni kugeuza mioyo ya watu kumuelekea Kristo (tafakari kumgeuza mtu pasipo kuona huyo mtu muujiza wowote kwako hasa mambo ya rohoni?)
Sasa Mtu huyu alikuwa na nguvu nyingi rohoni “ _nguvu za rohoni ni zaidi ya kutoa pepo na kuponya wagonjwa au kuona maono nk”_
Mathayo 11:11
“Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.”
Maana yake hakukuwa na mtu aliekuwa na nguvu nyingi kama huyu tangu agano la Kale mpaka katika kuzaliwa kwake.
Umewahi kufikiri ni kwa nini watu walikuwa wanamfata jangwani na sio yeye ndio alikuwa anawafata mijini na visiting? Ni kwa sababu ya nguvu iliyokuwa ndani yake huyu mtu ilikuwa inawavuta watu kumfata kule aliko na meneno aliyokuwa anazungumza yalikuwa na nguvu ndani yake yaani yalikuwa ni maneno kama tunayosema mimi na wewe juu ya injili lakini nyuma ya maneno yale kulikuwa na nguvu isiyokuwa ya kawaida.
Inayowafanya watu kuugua watu kugeuka kutoka katika dhambi watu wanalia na kujuta na kutubu kwa kumaanisha kugeuka kutoka dhambini.
“ Watu hawageuki kwa wingi wa maneno au upangiliaji wa maneno mzuri la! Bali ni nguvu iliyo ndani ya yale maneno unayosema Neno la la Mkristo anaekemea pepo litoke kwa jina la Yesu aliejaa Roho ni tofauti kabisa na neno hilo hilo linalotamkwa na mtu ambae hajajawa roho maana mtu aliejaa roho neno lake linakuwa na mamlaka na nguvu Nyuma yake inayofanya pepo nk vitoke’_
Na maneno hayo yanaenda kuleta uzima…
Yohana 6:63
“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”
Na kilichopelekea huyu mtu kuwa hivi ni kukaa majangwani yaani(kuomba,kufunga kusoma torati)
2.Eliya
Mtu huyu(kama mimi na wewe) aliweza kuzuia mvua isinyeshe kwa miaka mitatu na nusu na kuruhusu ije tena uwezo huo ulikuwa ndani yake.
“Mungu hakuzuia mvua ni Eliya ndio aliyefanya hivyo… wala Mungu hakushusha moto kwa wale watu waliotumwa kumkamata ni Eliya kwa sababu ya nguvu iliyokuwa ndani yake”
1 Wafalme 17:1
“Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.”
Unaona hapo? “ILA KWA NENO LANGU”
Unaweza fikiri ni tukio lilitokea siku moja kuzuia mvua Eliya aliamua tu hivyo akajifungia akaomba basi ikawa kama unafikiri hivyo Jaribu kujifungia na wewe uzuie kitu fulani uone.
Haikutokea ghafula tu ikawa hivyo lakini yalikuwa ni matokeo ya nguvu ambazo alizitengeneza kwa kipindi kirefu Eliya
wapo watu wengi ndani ya maandiko na nje ya maandiko ambao walifanya mambo makubwa kwa sababu walijua kanuni ya kupata nguvu na kuwa watawala katika ulimwengu wa roho. Na baada ya kujua hivyo walitafuta kwa bidii sana.
Na tabia za watu hawa walikuwa ni Waombaji,wafungaji,walidhamiria Kutoka ndani na wakakubali kulipa gharama wakafanikiwa, walijitenga na maovu wakaruhusu nguvu kudhirika ndani yao.
Ni kama wakina Bill graham hawakufanya miujiza na walikua wanasimama kutoa mahubiri ndani ya dakika 30 zikizidi sana 50 na baada ya hapo akiita watu kuokoka mamia ya watu walimgeukia Kristo.
Lipa gharama kubali hakuna mabadiliko pasipo kufunga,pasipo maombi pasipo neno hayapo.
Ukristo sio dini Ukristo ni maisha halisi kabisa ambayo lazima watu waone mabadiliko.
Ubarikiwe sana.
@Nuru ya upendo.
Mawasiliano:0613079530
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.