ukuta uliopakwa chokaa ni nini sawasawa na matendo 23:3?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Kabla ya kwenda kutazama maana halisi ya mstari huu ni vizuri tukajua kwanza zamani makaburi yalikuwa ni ya aina gani.

Makaburi ya zamani yalikuwa ni ya tofauti kidogo na ya sasa.
Kama tunavyojua Makaburi ya kipindi hiki ni Makaburi yanayochimbwa kwenda chini kaa urefu usiopungua futi 6. Na yakishachimbwa ikiwa mtu amekufa basi anawekwa kwenye jeneza kisha litashushwa kwa kamba mpaka mwisho na litafunikwa kwa mchanga.  Na baada ya kipindi fulani linaweza jengewa kwa vigae au simenti.

Lakini Makaburi ya zamani yenyewe yalikuwa ni pango yanakuwa na mlango ambayo yanafunguliwa watu waliokufa wanawekwa humo kisha linafungwa na kwa nje linapakwa chokaa/linarembwa kwa kupakwa rangi mbali mbali mojawapo ni chokaa. Linakuwa linavutia na kupendeza kwa nje.

Bwana Yesu pia aliwahi kutumia mfano huu alipokuwa akiwaambia haswa Mafarisayo akatolea mfano wa makaburi yaliyopambwa kwa chokaa na yanavutia sana kana kwamba kitu kilichoko ndani ni kizuri sana na ni cha thamani kubwa sana ilihali huko ndani Kuna mifupa tu.


Sasa mfano huo ulikuwa mahususi zaidi ukilenga kutoa mfano wa watu ambao kwa nje wanaonekana ni watauwa, yaani watakatifu lakini kumbe wamejaa unafiki ndani yao wala kile wanachokionyesha nje ni mbali kabisa na kile kilichoko ndani.

Wanaonekana ni watumishi wa Mungu, waimbaji kwaya,mashemasi,wahasibu wa kanisa, wazee wa kanisa kwa nje wanaonekana ni wema sana na wanamcha Mungu Lakini kumbe kwa ndani ni wanafiki.na ndio maana Bwana Yesu anasema Ole wao.

Mathayo 23;27 ‘Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na MAKABURI YALIYOPAKWA CHOKAA, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa MIFUPA YA WAFU, na uchafu wote.

28 Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani MMEJAA UNAFIKI NA MAASI’.

Unaona hapo!, alikuwa akiwaambia Mafarisayo na Waandishi walikuwa wamejaa unafiki walikuwa wanajionyesha kwa watu kuwa wao ni watakatifu na wanaokubali na Mungu wala hawana waa lolote lakini kumbe ni wanafiki.

Hizi ni tabia zilizokuwa ziko kwa watu hawa katika nyakati zile.

Sasa vivyo hivyo hata katika nyakati hizi za Mwisho jambo hili lipo tena kwa kasi kubwa sana sana. Tunaonekana kwa nje na watu sisis ni watakatifu sana na wakati mwingine tunasifiwa na watu hata wanaotuzunguka lakini ndani yetu tumejaa unafiki, tumejqa maseng’enyo,wivu,hasira, husuda,uzinzi,wizi,uporaji, unywaji wa pombe, kujichua,kuangalia picha za uchi,nk na kila uchafu kwa kila namna tumejaa nao.


2 Timotheo 3:5
“wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. ”

Unaona hapo! Ni wenye mfano lakini si wenyewe wanafanania kwa nje lakini kwa ndani ni tofauti kabisa.

Tito 1:16
“Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. ”

Maandiko pia yanasema…..

1Wathesalonike 5:22 “jitengeni na ubaya wa kila namna.

23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.

Tufanye bidii katika kujitenga na kila ainanya ubaya wa kila namna ili siku ile tutakaposimama mbele zake basi tusiwe na mawaa.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *