Unatambua uko katika nyakati gani
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Wakristo wengi wanaishi pasipo kutambua wapo katika nyakati gani au majira gani!, kiasi kwamba wamejisahau na wengine hawajui kabisa wanaishi katika nyakati za hatari kiasi gani!, dalili nyingi za kurudi kwa Bwana Yesu zimeshaonekana nyakati zile zilizotabiliwa zimeshaonekana tayari. Tupo katika wakati ambao si rafiki kwetu tena.
Wakristo wengi wanapumbazwa na mambo ya ulimwengu huu kiasi kwamba hawajui hata nyakati wanazoishi. Udanganyifu wa mali nk vimewapumbaza Wakristo wengi wamewekeza nguvu kubwa katika mambo ya ulimwengu huu kuliko mambo ya Rohoni.. (si vibaya lakini kipaumbele yasiwe mambo yanayopita bali yadumuyo)
Maandiko yanasema tuyatafakari yaliyo juu lakini Wakristo wa nyakati hizi hawayatafakari tena yaliyo juu kule aliko Kristo bali wanayatafari ya chini.
Ni maombi yangu Roho Mtakatifu akufunulie jambo hili kupitia somo hili fupi.
Nyakati tunazoishi ni nyakati za Mwisho na Bwana Yesu yupo karibu kurudi sasa tunajuaje kwamba hizi nyakati tunazoishi ni nyakati za Mwisho? Maandiko yenyewe yameweka wazi.
Yoeli 2:28“Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;”
Mungu kupitia kinywa cha nabii Yoeli alizungumza jambo hili katika siku za mwisho atamimina Roho yake juu ya wote wenye mwili ikiwa na maana si Waisraeli peke yao tu bali kwa watu wote ikiwemo sisi watu wa mataifa na tunaona moja wapo ni kina Kornelio pamoja na sisi tu mashahidi wa mambo haya kuwa ni kweli.
Sasa siku za mwisho zilianza tu pale Yesu Kristo anapaa kwenda na mbinguni na baada ya siku kumi(10) tunaona siku za mwisho zinaanzia siku ile ya Pentecoste pale Roho Mtakatifu alipowashukia wale mitume Mia na ishiri (120) walipokuwa wakidumu katika maombi..
Na jambo hilo mtume Petro analisema baada ya Roho Mtakatifu kushuka juu yao maandio yanasema..
Matendo ya Mitume 2
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Unaona hapo katika Mstari wa 17? Anasema itakuwa katika siku za mwisho maana yake siku za mwisho zilianza kuhesabika tangu kipindi cha Mitume na ndio maana mitume walikuwa wanahubiri injili na kukubali kuwa takataka kwa kupigwa nk wakijua wanakipindi kifupi sana Bwana Yesu atarudi kuwachukua..
Walikubali adha na mateso ya kila namna kwa sababu walitambua nyakati na majira mpaka sasa tunaposoma nyaraka za mitume ni kana kwamba zimeandikwa jana tu maana mambo waliyotabiri tunayaona wazi wazi katika kipindi hiki.
Waliishi kwa kuyatafakari yaliyo juu wala si yaliyo chini.. ndugu ikiwa ndege wanatambua majira na nyakati ni ajabu kuwa wewe hufahamu majira na nyakati na siku ile ikujie kama mwivi..
Yeremia 8:7“Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana.”
Maandiko yanatutaka sisi tulio wa mchana tuwe na kiasi..
1 Wathesalonike 5
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.
Mstari wa sita anasema tusilale usingizi maana yake kuna kulala usingizi tukajikuta tunatembea kama watu wa ulimwengu huu. Tuwe ni watu wa kujizuia na kuwa na kiasi.
Leo hii Wakristo wengi hawana kiasi hata katika mambo yasiyowajenga wao wako.. utakuta Mkristo yuko bize na mipira, tamthilia,vichekesho lakini hana muda na biblia akisoma kidogo analala anasingizia mashambulizi hajijengei nidhamu na mambo ya rohoni wala Hajaii Roho,Maombi mpaka asukumwe sukumwe..
Pasipo kujaa Roho Mtakatifu ndugu yangu huwezi kuishi maisha ya yanayo mfanania Kristo utakuwa unaenda unarudi.. wekeza muda wako katika Kusoma biblia,kuomba,kuwahubiria wengine nk utaona unaanza kuona wepesi kutembea katika roho na kuyatimiza mapenzi ya Mungu.
Nimekuombea katika jina la Yesu Kristo akufungue macho na uishi katika maisha haya ukiyafikiri ya juu aliko Kristo wala si ya chini tena. Mpe Roho Mtakatifu nafasi na yuko pamoja na wewe wala usiogope.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.