Nakusalimu katika Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo.
Ziko ibada kuu tatu ambazo watu wengi sana katika nyakati hizi za Mwisho watu wanaziabudu pasipo hata kufahamu. Maana ibilisi amewafumba macho wasiweze kutambua. Tutazianisha hapa na kuzitazama kwa undani zaidi kwa neema za Bwana.
- SANAMU ZILIZOCHONGWA KWA MFANO WA MTU.
2.SANAMU-WATU.
3.SANAMU-VITU.
Aina kuu hizi tatu zinaabudiwa na idadi kubwa sana Duniani. Wengine ni Wakristo kabisa lakini hawafahamu kuwa wanaabudu sanamu jambo ambalo ni machukizo makubwa mbele za Bwana.
1.SANAMU ZILIZOCHONGWA KWA MFANO WA MTU.
Hizi ni aina za sanamu zinazochongwa na watu(yaani kazi ya mikono ya Mwanadamu) kwa lengo hasa la kuabudiwa/kuzifanyia ibada na kuziona kama Mungu kwao.
Ni sanamu ambazo zina mfano wa mtu kabisa na sifa zake zimeanishwa vyema katika maandiko kuwa zina masikio lakini hazisikii,zina midomo lakini hazineni,zina macho lakini hazioni,zina pua lakini hazinusi,zina mikono lakini hazishiki,zina miguu lakini hazitembei nk. Kifupi zina milango yote mitano ta fahamu na yote haifanyi kazi.
Pia wanaoziabudu wanafananishwa hivyo kiroho
Zaburi 115:4 “Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu.
5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,
6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu,
7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake.
8 Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia”
Ni sanamu zinazoabudiwa na wimbi kubwa la watu wanaojiita kuwa ni Wakristo zinawekwa kwenye makanisa(Sanamu ya Maria,Yesu,Yusufu nk)watu wanakwenda kuzifanyia ibada na kusema shida zao kana kwamba zinasikia lakini sivyo..
Pia jamii ya wahindi,Wabasha nk nao wanazo hizi wanaziabudu lakini ukweli ni kwamba hazisikii wala haziwezi kufanya lolote ni sawa sawa na mungu wa Wafilisti Dagon ambae alivunjika shingo na miguu na kichwa baada ya sanduku la Mungu alie hai kuwekwa pale. Kuonesha ule ulikuwa ni udongo tu..
Na jambo hilo ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu. Sawa sawa na maandiko katika kitabu cha Kutoka 20:4-6.
2.SANAMU WATU.
Ni sanamu ambayo ni tofauti kidogo na ile ya kwanza tofauti hii inapumua/ina uhai ndani yake. Ile ya kwanza imetengenezwa kwa udongo/kwa Fedha nk. Vivyo hivyo nayo sanamu hii(Wanadamu) ina macho ya kuona lakini haioni,ina masikio lakini haisikii,ina pua lakini hainusi,ina akili lakini haitambui na kufahamu nk. Kama maandiko yanavyosema.
Ezekieli 12: 1 “Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, WATU AMBAO WANA MACHO YA KUONA, ILA HAWAONI, WANA MASIKIO YA KUSIKIA, ILA HAWASIKII; kwa maana ni nyumba iliyoasi”.
Hivyo mwanadamu Yeyote ambae hajamuamini Yesu Kristo huyo katika roho anatambulikana kama sanamu maana anamasikio lakini hasikii(haelewi Neno La Mungu) anamdomo lakini haneni/kusema mambo ya Ki-Mungu ana pua lakini hanusi mambo ya Rohoni na kujua tuko katika nyakati za Mwisho. Nk
Hivyo sanamu si tu zinazochongwa lakini pia hata mtu ambae hajamwamini Yesu Kristo ni sanamu. Mwisho litavunjika kama Dagoni sanamu ya Wafilisti.
Hivyo ikiwa hujamfuata Yesu wewe na viungo vyako vyote ni sanamu..
MODOMO wako ni Sanamu unanena maneno yasiyofaa(Matusi na uzinzi nk) bado unaubadilishia kila siku rangi leo nyekundu kesho brown nk.
KICHWA chako mi sanamu maana kila siku unakitumikia na kuwaza unakiwekea mtindo gani wa nywele ili kipendeze unaweka rasta., unanyoa viduku kama vile ulizaliwa mavyo unaona bila hivyo huwezi nk.
MIKONO NA MIGUU YAKO ni sanamu unaishikisha mambo yasiyofaa na unaweka makucha ya bandika(ili upendezeshe mungu wako)
TUMBO lako ni sanamu/mungu wako unalitumikia kwa kuliwekea mambo mabaya kama pombe,nk ili uliburudishe nk.
Maandiko yanasema..
Wafilipi 3:19 “mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Lakini pia inasema biblia.
Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”.
Hivyo haijalishi unasema unamuamini Yesu ikiwa bado unahangaika na mwili wako kuuwekea mapambo na fashion za kidunia unaabudu sanamu acha mara moja kaa katika hali yako ya kiasili..
Ndio maana ukienda kanisani hujaweka rasta na kucha badia nk unaona kama hauko sawa kwa sababu mungu wako hujamupendezesha ili kuvuta attention ya watu.
3.SANAMU-VITU.
Hizi ni sanamu ambazo hazina muonekano unaofanana na Mwanadamu lakini zinaabudiwa sana pia na Wakristo wengi na wapagani.
Mfano wa sanamu hizi ni Vipawa(karama)Fedha,vipaji(talent)kazi,nyumba,gari nk.
Na mambo mengine kama haya Mwanadamu anapokuwa navyo na hajampa Yesu Kristo maisha yake hajamuamini. Huyo ni muabudu sanamu.
Hata wewe uliyeokoka ikiw unaviona hivi ndio vya thamani kwako na ukivipoteza vinaharibu mahusiano yako na Mungu wewe ni muabudu sanamu.
Hivyo hakuna mwanadamu ambae yuko katika kati yaani hayupo kwa Mungu wala kwa Shetani hayupo ikiwa wewe si wa Shetani basi wewe ni wa Mungu na ikiwa wewe si wa Mungu basi wewe ni wa shetani uwe hutaki au unataka ndio ilivyo. Amua leo kujitoa maisha yako kwa Yesu Kristo kweli kweli kabisa.
Umempa Yesu Kristo maisha yako??
Maana maandiko yanasema kuwa waabudu sanamu wote sehemu yao ni katika ziwa lile liwakalo moto liepuke kwa kumwamini Yesu Kristo.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, NA HAO WAABUDUO SANAMU, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Thanks for this very informative article! For anyone looking for a detailed step-by-step guide on creating a Binance account, here’s a helpful resource I found: How to Register an Account on Binance. Hope it’s useful!