Shalom na Maranatha Maana yake ni nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe ndugu katika Kristo Yesu.

Maneno haya mawili yanatumika sana kwa Watakatifu wengi, na huenda huwa unayasikia mara kwa mara lakini huenda hujui nini maana yake.

Maana hata mimi nilikuwa nikiyasikia kwa muda mrefu lakini sikuwa najua maana yake hapo kabla.

Sasa leo tutakwenda kujifunza maana ya maneno haya mawili.

Shalom Ni neno la kiiebrania “šālōm”   maana yake ni Amani!, hivyo neno Shalom maana yake ni Amani. Baina ya Mtu na Mtu ama baina ya Mungu na Mtu, ama kati ya taifa na taifa lingine.

Waamuzi 6:22 “Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso.23 Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.24 Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri”.

Mungu wetu pia jina lake ni YEHOVA-SHALOM yaani Mungu wa Amani.(God of piece).

Pia ukisoma.

Waebrania 13:21″ MUNGU WA AMANI  awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.”

Ukisima pia 1 Wathesalonike 5:23, Wafilipi 4:9  Isaya 9:6.  utaliona jambo hilo likizungumziwa kuwa Mungu wetu ni Mungu wa Amani.

Hivyo kama jinsi Mungu wetu yaani Bwana wetu Yesu Kristo alivyo wa Amani nasi pia hatuna budi kuwa ni watu wa Amani,  wasiotaka Mashindano ya namna yoyote ile, na sio tunasalimiana Shalom,Shalom ya mdomoni tu lakini Moyoni tumejaa visasi, wivu nk.

Maana kama alivyo mkamilifu na sisi inatupasa kuwa vivyo hivyo.

Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Hivyo na sisi pia tunatakiwa kuwa kama Baba yetu.

Pia tunasisitizwa kuitafuta sana Amani na haipatikani kwingineko ila kwake Kristo Yesu tukikubali kuongozwa  na Roho wake Mtakatifu.

1Petro 3:10 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani,aifuate sana“.

Maana ya MARANATHA ni nini?

Ni Neno la kiiebrania lenye maana ya “Bwana wetu anakuja” kwa kiingereza “OH LORD COME”.

Tunalisoma hilo katika.

1 Wakorintho 16:23

Maranatha!.

Tafadhali washirikishe na wengine na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na namba hii +255 789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *