Beelzebuli ni nani?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom Bwana Bwana Yesu apewe sifa.

Beelzebuli katika Agano la Kale alikuwa ni mungu wa Wafilisti(Philistine) kwa sasa inajulikana kama Palestina. Pale Mfalme Ahazia alipoanguka kutoka juu kule Samaria akaugua sana hivyo akatuma wajumbe waende wakamuulize kwa Beelzebuli mungu wa Ekroni kwamba je atapona ugonjwa huo.

2 Wafalme 1:[2]Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.”

Hili ni jambo ambalo lilimchukiza Mungu pata muda soma kitabu cha 2 Wafalme kupata Ufahamu zaidi juu ya Habari hii!!,

Sasa Beelzebuli “Maana yake ni Mkuu wa Pepo”  Au Mkuu wa Mashetani.

Yesu alipokuwa akifanya Miujiza kama kuponya wagonjwa, kutoa mapepo kwa nguvu za Mungu Mafarisayo walisema kuwa anatoa Pepo kwa mkuu wa pepo yaani Beelzebuli.

Mathayo 12:22  “Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.

23  Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?

24  Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa BEELZEBULI MKUU WA PEPO”.

Sasa huyu mkuu wa Mashetani ni nani?

Biblia inataja wazi mkuu wa mapepo/Mashetani ni Ibilisi, yaani Shetani mwenyewe aliekuwa Lucifer. Ndio mkuu wa nguvu za Giza na mapepo wote aliowashawishi wakaasi. Yeye ndio mkuu wao.

Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.”

Biblia inasema “malaika zake wakatupwa pamoja naye” kuwa yeye ndio mkuu wao hao waliotupwa pamoja nae.

Hivyo Mafarisayo walipoona hivyo walisema Yesu anatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo(Shetani/ibilisi) jambo ambalo Yesu alilikanusha kwa kutoa sababu za Msingi kabisa.

Akisema Shetani hawezi kumtoa Shetani mwenzake vinginevyo huo ufalme utafitinika yaani hautasimama.

Hivyo waliingiwa na wivu na chuki na hasira kwa sababu wao hawakuwa na nguvu ya kufanya hivyo wakaona Yesu ndio anaaminika kuliko wao wakongwe ambao tangu mwanzo wao wanapenda kuheshimiwa Sasa walioja heshima waliokuwa wakiheshimiwa na kuogopwa na kusalimiwa na watu njiani inahamia kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Mathayo 12:26 “NA SHETANI AKIMTOA SHETANI, AMEFITINIKA JUU YA NAFSI YAKE; BASI UFALME WAKE UTASIMAMAJE?27  Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.28  Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia”

Hivyo kamwe Shetani hawezi kumtoa Shetani ikiwa hivyo basi ufalme wa nguvu za giza hautasimama kamwe.

Inatufundisha kumbe Shetani hawezi kuto Pepo maana mapepo yote yanafanya kazi katika maagizo yake hakuna hata pepo moja linafanya kazi nje na Amri yake.  Yote yanafata Order ya mkuu wao alivyoyapanga katika vitengo mbali mbali.

Lakini nguvu za Mungu pekee ndio zinaweza kutoa pepo na pepo likatii maana uweza wake MUNGU wetu ni mkuu sana.

Hivyo mtu anaeenda kwa Wachawi, waganga wa kienyeji kitu kinachofanyika hapo sio kwamba pepo linatolewa bali anawekewa mapepo mengine yenye nguvu zaidi na pemgine anabadilishiwa tatizo ikiwa ilikuwa ilikuwa ni kulipuka mapepo tu muda fulani ukifika atawekewa mapepo machafu mengine yatakayozalisha tabia zingine kama alikuwa sio mzinzi anakuwa ni mtu wa kuzini,nk.

Maana kama tulivyojifunza “Shetani hawezi kumtoa Shetani mwenzake ” Jiuluize huko ni kipi kinakwenda kutolewa!??.

Suluhisho la Mambo yote ni Bwana wetu YESU KRISTO tu.  Wala si kingine yeye ndie awezae kufanya hivyo ķumtoa pepo ndani ya mtu usidanganyike mganga wala mchawi hawawezi.

Ubarikiwe sana.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Je umeokoka ikiwa bado hujampa Yesu Kristo maisha yako bado hujachelewa mlango bado uko wazi. Epuka kwenda kwa waganga unakwenda kupoteza muda na kuongeza mapepo mengine ndani yako.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi

+255693036618/+2557890001312.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *