Nini maana ya Maziara? Je!, tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom.

Maziara. Ni sehemu ya juu ya kaburi pale mtu anapomaliza kuzikwa kile kinachokaa juu ya kaburi kama mfano wa kijumba,mnara,au hata msalaba kinachoashiria kuwa Kuna kaburi mahali pale.

Maziara ni mapambo ya ziada yanayoongezwa ili kulipamba kaburi lipendeze kama vile kaburi la mwalimu Julius K Nyerere Kuna kile kijumba kilichojengewa baada ya lile kaburi kumalizwa kujengwa sasa hicho kijumba kwa jina jingine ndio kinaitwa Ziara.

Na kusudi kubwa la kufanya hivyo ni kulipendezesha kaburi na  kumuenzi marehemu aliekufa.

Katika Agano la Kale manabii walipouwawa na Mafarisayo na Waandishi walikuwa wakiyajengea makaburi ya manabii Maziara kaa lenyo la kuwaenzi lakini walikuwa ni wanafiki maana ndio wao hao hao walikokuwa wanawaua.

Bwana Yesu aliwakemea Mafarisayo na Waandishi kwa unafiki huo waliokuwa wakiufanya.

Mathayo 23:29  Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 

30  na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.

31  Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.

32  Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.

33  Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

34  Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

35  hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

36  Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.

JE LILIKUWA NI KOSA KUFANYA HIVYO?.

Hapana halikuwa ni kosa ila Bwana Yesu aliwakemea kwa kile kilichokuwemo mioyoni mwao kilikuwa ni tofauti na kile walichokuwa wanakionyesha nje!, yaani walikuwa ni wanafiki walikuwa wanajionyesha kana kwamba wanawaenzi sana na wanawapenda sana lakini wao hao hao ndio waliokuwa wakiwaua wakifanya njama mpaka wanawaua.

Kama vile walivyowaua wakina Petro na Mitume wengine wengi.

NI SAHIHI KWA MKRISTO KUSAFISHA KABURI LA MAREHEMU WAKE/MFIWA?

Ndio ni sahihi kwani ni kulifanyia marekebisho na maboresho na kupalilia pale nyasi zinapokuwa nyingi sio kosa kabisa maana hata makaburi ya zamani vivyo hivyo yalikuwa anasafishwa na kutunzwa na kwa nje yalikuwa yamepandiwa bustani.

Yohana 20:15 “Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.”

hivyo ni vizuri kufanya hivyo lakini ukitambua kabisa jambo hilo haliongezi chochote kwa huyo marehemu.

NI SAHIHI KUFANYA IBADA HAPO?.

ikiwa ni ibada za kuwaombea marehemu waliokufa watoke kwenye mateso waende mbinguni (Toharani) si sahihi hizo ni ibada za wafu, yaani ibada za sanamu. Hivyo kama Mkristo hutakiwi kabisa kufanya hivyo ni machukizo makubwa sana Mbele. Maana wengine huenda na kuanza kuzungumza na kaburi na kuacha hela pale wakiamini yule mtu kweli yuko pale lakini sivyo.  Hizo ni ibda usishiriki kabisa wala kusogea.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *