HAPO NDIPO ULE MWISHO UTAKAPOKUJA.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Ukianza kusoma kitabu cha Mathayo 24:3 utaona wanafunzi wake Yesu walikuwa wakimuuliza Bwana Yesu mambo hayo aliowaambia yatakuwa lini maana yake yatatokea kipindi gani au wakati gani?,

lakini hatuoni wanaishia hapo tu wanamuuliza tena kuwa dalili ya kurudi kwake Bwana Yesu au kiashiria/viashiria cha kujua kuwa Yesu amekaribia kurudi ni vipi? Wanamalizia na kwa kumuuliza na dalili ya mwisho wa dunia itakuwaje?.

Kwa kulidhibitisha hilo tunaweza kusoma..


Mathayo 24.3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

Ili uweze kupata habari nyingi kutoka kwa Yesu lazima umwendee faragha kama wanafunzi wake walivyofanya, katika kuomba na kusoma neno na kutafakari.


Sasa Yesu alianza kuwambia ukweli wa mambo yote itakuwaje na akawapa dalili nyingi lakini karibia zote alizotaja alisema “msitishwe mwisho bado, hayo yote ndio mwanzo wa utungu” kauli alizo waambia baada ya kuwaelezea dalili Fulani.

Sasa leo tutakwenda kutazama dalili moja ambayo alisema mwenyewe Bwana Yesu kuwa tukiiona hiyo basi ule mwisho ndipo sasa utakapofika.

DALILI KUU AMBAYO NA MIFANO YA DALILI ZILIZOLETA MAANGAMIZI.

Mathayo 24.14 TENA HABARI NJEMA YA UFALME ITAHUBIRIWA KATIKA ULIMWENGU WOTE, KUWA USHUHUDA KWA MATAIFA YOTE; HAPO NDIPO ULE MWISHO UTAKAPOKUJA.

unaona hapo! Dalili za manabii wa uongo,matetesi ya vita,ufalme kwenda kupigana na ufalme,makristo wa uongo,kuongezeka kwa maasi,upendo wa wengi kupoa nk ni mwanzo wa utungu lakini sio ile ishara kuu kabisa.

Isahara kubwa sana ambayo inabidi tuiangalie tuiomwamini Yesu kwa kina ni hii katika huu mstari wa 14.

Anasema“…..habari njema ya ufalme itahuburiwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; HAPO NDIPO ULE MWISHO UTAKAPOFIKA.”

Sasa katika karne hii ya 21 injili karibu imehubiriwa ulimwengu mwote hakuna ambae hajalisikia jina la Yesu.

Kupitia Redio,TV,mitandao ya kijamii kiasi kwamba hata mtu alieko vijijini anaweza akasikiliza mahubiri katika vipindi vya redio nk. Waijilisti wengi kwa kiasi kikubwa wamefika vijijini haijalishi wengine ni wa uongo na bado wanalitumia jina la Yesu.

Wamejaa mastendi,masokoni,mitaani nk wanahubiri injili tunawaona kama wamekosa kazi ya kufanya wanapaza sauti kuwaita watu kwenye wokovu. Lakini inaonekana wanapiga kelele. jambo hili tunaliona kwa jinsi ya mfano kabisa ulio dhahiri kwa Lutu kule sodoma na Gomora.

Mwanzo 19:14 “Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, AKASEMA, ONDOKENI MTOKE KATIKA MAHALI HAPA KWA SABABU BWANA ATAUHARIBU MJI HUU. Lakini akawa kama ACHEZAYE MACHONI PA WAKWEZE

Unaona hapo? Alionekana kama anacheza tu hata hawakuwa na mpango wala muda wa kumsikiza kabisa lakini baada ya muda mchache sana baada ya Lutu kutoka Bwana alinyesha mvua ya moto sodoma na gomora na kuingamiza kabisa. Kwa hiyo miji huo haukuangamizwa pasipo unjiri kwanza kuhuburiwa kwa watu.

Sasa mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano na yaaandikwa ili kutuonya sisi kama maandiko yanavyosema….

1 Wakorintho 10:11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani”

Hivyo ndugu fanya hima simama vyema katika imani wala usiregee kabisa maana tuko mwishoni kabisa mwa safari yetu. Kaza mwendo tengeneza njia zako mapema. Maana mwisho umeshafika tayari bado kitambo kidogo sana maandiko yanaema…

1 Wakorintho 10:12 “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”

Angalia sana ndugu yangu tukaze mwendo tuko katika saa za mwisho kabisa mambo ya dunia hii na kawaida ya dunia hii isitupumbaze na sisi tukaishi kama wa dunia hii tukajisahau na siku ile ikatujia kama mwivi. Tufanyike bibi Arusi wa Kristo kweli kweli.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *