JE! UNAMUWAKILISHA KRISTO AU ULIMWENGU?

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya Mwokozi wetu.

 

Kama Mwamini uliyeokoka ukampa Yesu Kristo maisha yako ni muhimu sana kujua unamuwakilisha nani kwa watu wanaokutazama. Katika jamii inayokuzunguka wakikutazama wanamuona Kristo ndani yako au wanauona ulimwengu ndani yako?, ni jambo la kuwa makini sana na kuwa watu wa kujitazama kila siku na kutenegeza mahali palipo na mapungufu ili Ukristo wako usiwe na lawama kwa Mungu na kwa wanadamu pia.

 

Ukristo sio kwenda kanisani na kuonesha tabia njema tu ukiwa kanisani na watu unaosali nao bali Ukristo ni maisha. Ukristo ni kuwa tofauti kabisa na watu wa ulimwengu huu. Ukristo ni badiliko la akili,ufahamu,tabia na mwenendo na ndio maana maaandiko yanasema ukiwa katika Kristo unafanyika kuwa kiumbe kipya.

 

2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”

 

Hivyo Ukristo ni lazima kuwe na badiliko la ndani kabisa katika kila maeneo na katika kila eneo la maisha yako na maandiko yanasema

 

Wagalatia 2:20 “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; WALA SI MIMI TENA, BALI KRISTO YU HAI NDANI YANGU; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu”

 

Unaona hapo anasema “...wala si mimi tena, bali kristo yu hai ndani yangu…..”  kwa nini anasema “..wala si mimi tena..” kwa nini  hakusema “..bali ni mimi pamoja na Kristo ndani yangu…” maana yake ni kwamba ni lazima ukubali unapompokea Kristo yeye ndio aonekane na sio wewe tena. Kwa kukubali kuchukua sura halisi na tabia halisi ya Kristo ndani yako hapo unakuwa unamuwakilisha Kristo katika ulimwengu huu na watu wanaokuzunguka pia.

 

Note: “Ukristo ni badiliko la kifkra,kimwenendo,kimatendo,mtazamo wala sio kwenda kanisani tu na kuimba kwaya na kuuhubiri injili halafu maisha yako ni machafu bado.

 

SASA NI KWA NAMNA GANI UTAJUA UNAMUWAKILISHA KRISTO AU UNAUWAKILISHA ULIMWENGU(IBILISI NA MIFUMO YAKE)

Tutakwenda kuangalia mambo machache nay a Muhimu sana kwa Mkristo yeyote mwenye tumaini la uzima wa milele kweli kweli ndani yake lisilo na mashaka wala hofu.

 

  1. MAVAZI

Hili ni eneo ambalo wakristo wengi sana wanachukia na kukasirika wanapoambiwa. Nyuso zao zinabadilika na mioyo uyao ndani inaghadhabika sana. Ni kundi la wakristo wasiopenda kusikia ukweli hasa unaogusa kwenye badiliko lao juu ya mavazi.

 

Leo hii utakuta ni Mkristo ananguo za kanisani na nguo asizoweza kwenda nazo kanisani  maana ni aibu. Mkristo ananguo za heshima(akiwa kanisani tu) na zisizo za heshima(akiwa kazini au mtaani).NI UNAFIKI MKUBWA MBELE ZA MUNGU. Mkristo unaendana na fashion za kidunia, unavaa masuruali,nguo za kubana hata watu wakikutazama hawamuoni Kristo bali wanamuona mwanamke wa kidunia tu.

Watu wa kidunia wanakimbizana na fashion na wewe Mkristo unakimbizana na fashion tofauti yao na yako iko wapi? Unafahamu kuwa huo mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu?(1 wakorintho 3:16)unauvalisha nusu Uchi.

Ukiwa mkristo lazima ukubali katika ulimwengu huu hauna fungu lolote fungu lako ni katika ulimwengu ujao kubali kuishi kama mpitaji usitake kuwa kama mkaaji waache wenye dunia yao waishi kama wanavyotaka.

 

  1. MWENENDO.

Hili ni eneo muhimu sana kwa mkristo. Na limebeba mambo mengi ikiwemo hata la hapo juu lakini hapa tutaangalia mambo mengine kwa undani zaid.

Kama mwamini lazima mwenendo wako uwe kama wa mwokozi wako. Leo hii utakuta mkristo anatoa matusi mdomoni mwake kama watu wa kidunia, mtu wa kulipiza visasi na kutikusamehe. Mkristo unafatilia tamthilia za kidunia zenye maudhui ya kizinzi tu ndani yake, na ni tamthilia zisizokujenga kiroho bali zinakubomoa kiriho kabisa. Leo hii Mkristo umejaza nyimbo za kidunia kwenye simu yako(na kwenye akili yako pia) kuliko hata nyimbo za injili. Unasikiliza nyimbo za kidunia na unaziimba kabisa hadharani au kwa maficho unafikiri Yesu anapendezwa na hilo jambo? Leo uko kanisani lakini baadae uko baa na kwenye kumbi za starehe halafu unasema “si mimi tena bali Kristo ndani yangu” ndugu yangu hapo wala si Kristo ndani yako tena.

 

Unashabikia mipira na kubishana na watu wa kidunia na hata mwingine unatukananao, natoa maneno mabaya na mizaha mingi na kukasirishana unafika nyumbani huna hada hamu ya kula kisa mpira na unasema Kristo yuko ndani yako. julize ni Kristo yupi huyo?.

 

Usidanganywe na injili za uongo wanazokwambia ” ukiokolewa umeokolewa. Hata uendelee kuishi hivyo hivyo huwezi kwenda kuzimu wokovu ni wa milele. Mwamini hawezi kupoteza wokovu Mungu hakufanya kazi nusu nusu” usidanganyike na hizi injili ni potofu kabisa zinakufanya uendelee kusisinzia katika dhambi mwisho uangamie.

“fikiria unakubali kujisalimisha katika dhambi unaendelea kuangalia ponografia,unaangalia posti za picha chafu chafu tu huko twitter(X),instagram, umejiunga kwenye magroup ya whatsapp ya picha za uchi huko nk”  yote hayo unafanya unatofauti gani na mtu asiyemjua kabisa Kristo ambae hajaokolewa?

 

Unasema umeokolewa na unaishi maisha ya namna hiyo je! Umeokolewa kwa namna gani huko? Kama sio udanganyifu wa shetani? Kuwa makini sana katika nyakati hizi, usidanganyike INAWEZEKANA KUSHIDA DHAMBI KATIKA ROHO MTAKATIFU wala hakuna dhambi ngumu kuishinda/kuiacha.

 

Mwenendo wako Kristo anautzama sana na kuona je unalifanya jina la Mungu litukuzwe au litukanwe katikati ya mataifa? Maana anaefanya jina la Mungu litukuzwe au litukanwe ni sisi wenyewe waamini, watu wanajifunza kutoka kwetu, dunia inatutazama sisi.

 

Usishirikiane na matendo ya giza bali uyakemee…

 

Waefeso 5:8” Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,”

 

Hivyo ndugu angalia sana hayo unayoyang’ang’ania leo hayatakufaidia badilika ki mwendo,fikra,mtazamo, ufanane na Kristo

 

Kumbuka wewe ni barua ya wazi inayosomwa na watu wote, je wewe ni barua inayosomekaje? Katika uzuri au ubaya? Sisi pia ni manukato mabele za Kristo je wewe ni manukato yapi mbele za Mungu? Mabaya aumazuri?

 

2 Wakorintho 3:2-3 ” Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;

[3] mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.”

 

Matendo yako na mwenendo wako ndio barua tosha watu wanaisoma, kama matendo yako si mazuri nakushauri acha, mtake Roho Mtakatifu aingilie kati leo maisha yako.

 

Matanatha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *