Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Wakati fulani nikiwa nimekaa na watumishi wenzangu tukitafakari neno la Mungu. Roho Mtakatifu alitufundisha jambo kubwa sana. Ambalo hatukulifahamu hapo kabla.
Tukiwa katika kutafakari tukisoma maandiko Roho Mtakatifu alisema nami kwa njia ya ufahamu ndani yangu maneno haya “Baraka hazitafutwi,Baraka zinakufata/zinakutafuta wewe siyo wewe ndio unaezitafuta baraka”
Nilitafakari sana ni kwa namna gani Baraka zinanifata kivipi? Kadiri tulivyozidi kujifunza Roho Mtakatifu alizidi kutufundisha zaidi.
Sasa katika nyakati za Mwisho hizi Wakristo wengi sana wanapoteza Muda wao mwingi sana kutafuta Baraka kuliko hata kumtafuta Mungu. Yaani Baraka hizo zinatafutwa kuliko hata yule anaezitoa..
Sasa ni kwa namna gani..watu wanahudhuria sana katika ibada! Wanaomba sana,wanafunga sana ili Bwana awabariki katika mambo yao.. au Bwana awainue katika utumishi wao,Masomo yao nk yote haya ni mazuri lakini watu wengi wanakosea Shabaha.
Ndio hapo utakuta mtu analalamika na kunung’unika sana kuwa amejitoa katika kumtumikia Mungu,kumtolea Mungu lakini haoni Mungu akimbariki.. ndugu natamani ulifahamu hili na uliweke kwenye ufahamu wako Mtu yeyote aliejitoa kweli kumtumikia Mungu katika mazingira yoyote yale iwe kazini nk ni lazima Mungu atambariki tu.. Baraka zitamtafuta kokote aliko na zitamjilia.
Sasa ni kwa namna gani?
Kumbukumbu la Torati 28
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
Unaona hapo?. Soma vizuri huo mstari wa kwanza na wa pili 2. Anasema “utakaposikiza kwa Bidii na kuyatunza….”
Lakini anaendelea tena kwa kusema.. “…Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo Sauti ya Bwana….”
Hapo hasemi..”Baraka hizi zote utazijilia na kuzipata zilipo..”
Hivyo Baraka zetu zote zipo katika kumtii Mungu ama kuyashika yale anayotuamuru kuyafanya basi. Kama kweli tutakaa chini ya Roho Mtakatifu na kukubali kuongozwa na yeye basi tujue fika kabisa Baraka ni lazima zitatutafuta na kutufata mahali popote pale tulipo..
Roho Mtakatifu anapokuambia acha kitu fulani au toa kitu fulani au fanya jambo fulani kuwa mwepesi wa kufanya hivyo. Usiwe ni mgumu wa kuking’ang’ania .
Anza leo kumtii Roho Mtakatifu kufata kile anachokuambia.. fata Neno la Mungu linakutaka ufanye nini.. na hii ni kanuni ambayo Mungu ameiweka..
Baraka na mambo yote tunayapata kwa neema wala si kwamba tunastahili sana la! Kila unachokipata kizuri ni kwa neema zake na neema hiyo ndio inayokufundisha kukataa ubaya na kuchagua mema na kutembea katika njia ya haki na utauwa/utakatifu.
Hivyo ikiwa ikiwa unashika yote Yesu anayotaka na huoni chochote usikate tamaa wala usivunjike moyo wakati na majira vitakapofika Baraka zako zitakujiria kama mvua ya vuri ni lazima tu zitakupata.. hivyo endelea katika njia ya haki na kweli wakakati utakapofika zitakufikia tu.
Usihangaike kwenda kwa manabii,kununua maji,mafuta,kuwekewa mikono nk. Bali simama tu katika njia ya haki na kutii neno linasema nini. Wingu litakapojaa maji mvua haikosi kunyesha..
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.