Heri walio masikini wa roho.

Biblia kwa kina No Comments

Heri walio masikini wa roho.

Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Bwana Yesu anawaambia makutano pamoja na wanafunzi wake waliokubali kupanda/kumfata kule mlimani kwenda kumsikiliza katika hotuba yake na mambo mengi sana aliwafundisha.

Akiwaeleza mambo mbali mbali juu ya wao wanatakiwa kuwa ni watu wa namna gani kama hujapata nafasi ya kusoma sura yote ya tano ya kitabu cha Mathayo basi ni vyema ukaanza kuisoma sura nzima kisha ukatafakari utajifunza mambo mengi sana. Ni muhimu sana kuifahamu sura hiyo kwa yeyote anaesema yeye ni Mkristo.

Sasa Yesu Kristo anaanza kuwaambia/kuwafundisha wanafunzi wake na makutano kwa maneno mengi lakini leo tutatazama neno moja aliloanza kabisa kuwaambia “Heri waliomasikini wa roho;maana ufalme wa mbinguni ni wao

Neno “Heri” katika biblia maana yake ni “Kubarikiwa”  Hivyo anawaambia wamebarikiwa wote walio masikini wa roho maana kupitia umasikini huo wa roho walionao ufalme wa mbinguni ni wao?

Kwa namna gani sasa? Ni vizuri tutafahamu kwanza masikini katika Muktadha wa kawaida kabisa ni mtu wa namna gani ili tuweze kupata picha kamili ya jambo lipi linafunuliwa katika roho. Kumbuka mambo ya mwilini yanafunua mambo ya rohoni. Na ndio maana Bwana Yesu katika kuelezea ufalme wa mbinguni alitumia mifano ya dhahiri kabisa ya mambo ya mwilini ili kutoa taswira ya mambo ya rohoni.

Alitumia hekima za mambo ya mwilini kufunua kitu fulani katika roho.

Masikini ni mtu wa namna gani? Masikini ni mtu ambae ni muhitaji ambae hana uwezo wa kukidhi mahitaji yake ya msingi kama vile chakula,malazi,makazi, kutokana na ukosefu wa rasilimali za msingi kama vile fedha.

Na sifa ya masikini siku zote ni mtu asiekata tamaa katika kutafuta mahitaji yake ya msingi hawezi kukaa siku nzima lazima atakuwa ni mtu wa kuwaza leo atakula nini? Kama hana magazine atatafuta ni wapi atalala siku hiyo?, vivyo hivyo atatafuta tafuta hata nguo zilizotupwa na watu wengi ili kwa ajili ya kujistiri nk.

Sasa baada ya kuelewa juu ya masikini katika Muktadha wa kawaida kabisa sasa tutakwenda kuangalia masikini wa roho ni mtu wa namna gani na sifa zake ni zipi?.

Masikini wa roho. Hana tofauti sana na masikini wa Mwilini ni mtu ambae haridhiki kiroho anajiona kama vile hana chochote(hajajua chochote kuhusu Yesu Kristo) anaona kama ndio kwanza anahitaji sana kumjua Kristo hata kama ana miaka mingi katika wokovu. Anaona kama vile bado hajaimalisha mahusiano yake vizuri na Mungu.

Sasa Mtu wa namna hii kila siku ni lazima atakuwa ni mtu wa kupiga hatua zaidi katika kumuelewa zaidi Yesu Kristo na kuzidi kuimarisha zaidi mahusiano yake na Mungu.

Sasa Wakristo wengi sana katika nyakati hizi za Mwisho wanajiona sio masikini wa Roho kabisa maana kama wakristo wengi wangekuwa na roho hii ndani yao ya kujiona ni masikini basi muda mwingi sana tungeona idadi kubwa ya Wakristo wakihangaika huku na kule kutafuta kumjua zaidi Yesu Kristo kumfahamu zaidi na kumtumikia kwa moyo wote na kwa bidii sana.

Wakristo wengi wangekuwa na bidii ya kuomba,kufunga kukesha kusoma sana biblia nk. Maana roho hii inapokuwa ndani ya Mkristo anakuwa na sifa kadhaa..

Kama vile…

Kiu ya usomaji wa Biblia muda mrefu na kila siku na anakuwa ni mtu kila siku wa kujifunza jambo jipya, mtu huyu anakuwa ni muombaji tena wa maombi ya masafa marefu, kuwa na hofu ya mambo ya Ki-Mungu na kuyachukulia kwa uzito usio wa kawaida na kuliheshimu neno lake  wala anakuwa si mtu wa kulichukulia juu juu tu kama habari. 

Leo hii Wakristo wengi neno la Mungu hawalichukulii katika uzito wowote ule.  Linaonekana ni la kawaida tu yaani. Ni hatari kubwa mno.

Sasa katika nyakati hizi za Mwisho Wakristo wengi wanajiona wao kuwa ni matajiri sana rohoni. Na hii ndio sifa ya kanisa moja wapo ya kanisa hili la mwisho la Laodikia linajiona linajua mambo mengi kuhusu Mungu.

Leo hii Wakristo wengi sana wanajiona wanamfahamu sana Kristo kupitia mafundisho wanayofundishwa jumapili kwa jumapili kanisani na ibada za kati katikati ya wiki. Hawataki kukaa wao kuanza kuisoma biblia na kutafakari, wanaona biblia yote na mambo yote wanayajua.

Ikiwemo hata wachungaji nao vivyo hivyo wanaona hakuna mtu wa kuwafundisha wao ndio wanaelewa biblia yote wala hawataki kusikiliza na kujifunza kitu kipya kila siku yaani hakuna unyenyekevu kabisa ni watu ambao wanakosoa wengine na kuona wao hawajui kitu. Lakini kumbe hakuna kitu wanafahamu.

Ndio sifa hii imetajwa kwa kanisa letu hili la saba kwamba….

Ufunuo wa Yohana 3:17“Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.”

Unaona sifa ya kanisa hili? Lakini Yesu Kristo anasemaje? Kuwa kanisa hili ni wanyonge(hawajui kitu),tumejawa na mashaka (leo hii Wakristo wengi ukiwauliza wanauhakika wa kwenda Mbinguni? Watakwambia “Mungu mwenyewe ndio anajua au hilo ni jambo lingine” maana yake hakuna uhakika kabisa wakati tunapomuamini Yesu Kristo tunakuwa na hakikisho ndani yetu lililo imara kabisa.) Wakristo wengi wakisikia habari zinahubiriwa kuhusu siku za mwisho wanaogopa na kutetemeka mwisho wanasema “hizo ni habari za kutishana” wakati maandiko yametutaka tufarijiane kwa maneno hayo kuwa Kristo yu karibu kurudi

1 Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

Unaona katika huo mstari wa 18? Maisha tunayoyaishi katika Kristo Yesu ndio yanayotupa hakikisho haijalishi unaenda kanisani kila siku na kutoa sadaka likuki kama maisha yako hayaendani na kile unachokiamini bado ni mzinzi,mtu wa mambo ya duniani huko hutakuwa na hakikisho tengeneza njia zako mapema.

Lakini anaendelea kusema Masikini,Kipofu(hata nyakati tulizopo Wakristo wengi hawajui na wanatakiwa kufanya nini wapo wapo tu wao ni kanisani jumapili kwa jumapili,) anaendelea kusema tena  na ni uchi (yaani wanajiita ni Wakristo lakini matendo yao ni mafu kabisa).

Sasa ili kuwe ni masikini wa roho kubali kuwa ni mnyenyekevu,kiri wewe hujui chochote unahitaji kumjua zaidi Kristo usijitumainishe.. Anza kuwa muombaji, tengeneza maisha yako kaa mbali na dhambi na ubaya wa kila namna anaza kuweka shauku yako katika mambo ya Ki-Mungu utaanza kuoma mabadiliko na ndipo hapo utaanza kuona Roho Mtakatifu anakufundisha na kukutengeneza kwa namna nyingine..

Maandiko yanasema..

Wakorintho 8:2 “Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.”

Soma tena…

1 Wakorintho 3:18“Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.”

Nyenyekea!, Usijione mwenye hekima machoni pako mwenyewe mtake Bwana usiwe kama farisayo kubali kuongeza maarifa kila siku na ikiwa ulikiwa umefundishwa mafundisho yasiyopatana na biblia kubali kuyaacha usijifanye mjuaji kwa kuyatetea.. unatetea kuvaa suruali,kunywa pombe si dhambi,umesamehewa milele ishi utakavyo huwezi poteza wokovu.. ndugu yangu ukiendelea kukaa katika hayo utajiona kuwa ni tajiri ķumbe ni masikini na ni mnyonge tena kipofu na uko uchi kabisa.

Muombe sana Roho Mtakatifu akupe kujiona ni masikini wa roho kisha toa nafasi ya yeye kukufundisha zadi.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *