Ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu.

Biblia kwa kina No Comments

Ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu.

Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Kama vile mambo ya duniani hapa jinsi tunavyoyataabikia na kuyasumbukia ili tuyapate na mwisho tuwe na maisha mazuri.  Kama vile Fedha,Elimu,nk

Unatumia muda mwingi katika kuhakikisha unajiweka vizuri katika maswala ya kifedha, kuongeza elimu zaidi na kufanya kazi kwa bidii ili kile unachokitaka kipatikane unaamka saa12 kwenda kazini hata kama hujisikii au la! Unaamka asubuhi na mapema wakati bado unasoma unawahi shule na kukesha kujisomea nk.

Sasa mambo ya rohoni nayo ni hivyo hivyo ikiwa unataka kuuteka ufalme wa mbinguni ni lazima ukatae uvivu wa kiroho na uwe na bidii hapo utaanza kuona matokeo makubwa sana yanafanyika katika maisha yako Bwana Yesu alisema.

Mathayo 11:12“Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”

Kama unavyowaza na kufikiri mambo ya duniani vivyo vivyo fikiri na wafanyia kazi mambo ya rohoni.

Ufalme wa Mungu uko ndani yako pindi tu ulipomwamini Yesu Kristo ufalme wake unakaa ndani yako wote wala sio nusu nusu unafanyika mmoja wa wana wa ufalme lakini ili huo ufalme ulioko ndani yako uweze kutoa matokeo nje yaani uweze kukuhudumia kama mwana wa ufalme inahitajika nguvu za roho “na hazipatikani kama bahati na au kwa kusema ipo siku nitakuwa na nguvu nyingi rohoni bali zinapatiakana kwa mikakati au ni mchakato kubali kuanza mchakato huo”.

Vinginevyo ufalme utaendelea kuwa ndani yako lakini hutaona matokeo yoyote yaani hautakusaidia sana. Bwana Yesu anasema..

Luka 17:21“wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

Tukisoma kwenye maandiko tunaona baadhi ya watu waliofanikiwa kuuteka ufalme wa Mungu ni wengi na ukiangalia maisha waliokuwa wanayaishi ni tofauti sana na watu wengine tutawatazama watu wawili kwa leo na tutajifunza ni kwa namna gani tunaweza kuuteka ufalme wa Mungu?.

1.Bwana Yesu.

Bwana wetu Yesu Kristo alifanikiwa kuuteka ufalme wa Mungu hata ukawa tayari kumsikiliza na kumtii kwa chochote alichotaka! Haikuwa ni rahisi kama tunavyodhani.. Bwana Yesu alilazimika kuingia gharama kubwa ili jambo hilo lifanikiwe alijua siri hiyo nasi tunajifunza kutoka kwake.

Bwana Yesu alikuwa ni mtu wa kuomba sana, kujifunza sana(hata alipokuwa na umri wa miaka 12 alikuwa anakaa na watu wenye hekima akiwauliza maswali na wakamjibu pia nae akawafundisha mpaka wao wakashangaa) wengi wetu tunadhani Yesu alikuwa anajua kila kitu la! Alihitaji kujifuza hakuzaliwa anajua kuongea,kutembea nk.

Lakini alikuwa ni mtu wa kufunga kwa kipindi kirefu na ni mtu ambae alikuwa anaishi maisha matakatifu hata asitende dhambi hata moja!! Haleluya hakika huyu ndie MWOKOZI.

Alijaa nguvu nyingi sana rohoni kumbuka “kuwa na nguvu nyingi za rohoni haziji kwa bahati mbaya bali ni mchakato kwa wewe na mimi kuzitafuta

Baada ya Yesu kuondoka utaona hata mitume wake walimuangalia yeye alikuwa anafanya nini wakawa ni watu wa kwenda Hekaluni kusali kila ifikapo saa9 mchana.. lakini wakawa ni watu wa Mifungo mingi mpaka wakina Petro wanasikia njaa kiasi cha kuzimia alipokuwa kule Yafa.

2.Yohana Mbatizaji. 

Huyu vivyo hivyo alijaa nguvu nyingi rohoni na akafanikiwa kuuteka ufalme wa Mungu kanuni aliyoitumia ni ile ile kama ya mwokozi alikuwa ni mtu wa kukaa majangwani huko na cha ajabu Yohana hakuwa anawafata watu mijini ili awahubirie juu ya msamaha wa dhambi bali watu ndio waliokuwa wanamfata wao Soma(Mathayo 11:6-9)Haleluya.

Israeli yote ilimfahamu Yohana Mbatizaji majangwani huko hakuwa anakaa tu basi.. sivyo alikuwa ni mtu wa kufunga, kuomba, kusoma torati nk na alijiepusha na uovu/dhambi alipokuwa huko hivyo ikapelekea mpaka Yesu Kristo mwenyewe kusema maneno haya…

Mathayo 11:11 “Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.”

Unaona! Yaani hata manabii huko wote wakina Musa,Danieli,Yeremia,nk hawakuwa ni wa kuu kama huyu mtu alikuwa ni mtu mkuu sana katika ufalme wa mbinguni mamlaka yake katika roho haikuwa ya kawaida kabisa. Na cha kushangaza Yohana hakuwahi kufanya Muujiza wowote ule maisha yake yote alikuwa ni mtu wa kuhibiri tu lakini kile alichokuwa anakihubiri kilikuwa na nguvu kubwa sana ya kubadilisha watu.

Lakini Yesu Kristo anasema hapo hapo 11b “Walakini aliye mdogo ni mkuu kuliko yeyea”  habari njema ni kwamba tunaweza kuwa ni wakuu katika ufalme wa mbinguni kuliko Yohana Mbatizaji Haleluya…!

Ni kwa kufata kanuni tu na jinsi inavyotupasa kutembea latika Kristo Yesu. Kuwa ni mdogo katika ufalme wa mbinguni maana yake ni kuwa mnyeyekevu,mwaminifu unaethamini mambo ya rohoni (Ki-Mungu) unaejitoa kwa ajili ya wengine kwa kuifanya kazi ya Mungu pasi kuangalia maisha yako. Yaani kujikana nafsi kwa kuipoteza kwa ajili ya Kristo fanya kazi ya Mungu kwa moyo wako wote wahudumie watu..

Kuwa ni mtu wa maombi kwako yasikate,kusoma neno na kufanya uinjilisti kwako isiwe mwisho endelea ni kwa kitambo kidogo sana utaona jinsi unavyokuwa ni mtu mwingine.

Kuna siri moja kubwa sana ya sisi kuwa wakuu yaani kuuteka ufalme wa Mungu Bwana Yesu alitwaambia kupitia wanafunzi wake hata sasa sisi tulifikiliwa na miisho ya zamani hizi.

 

Mathayo 20

26Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;

27na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;

28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

Soma hiyo mistari kwa kurudia tena uone siri iliyopo hapo!! Unataka kuwa mkubwa katika ufalme wa Mungu? Kama jibu ni ndio Basi TUMIKA.

unataka kuwa wa kwanza? Kama jibu ni ndio KUWA MTUMWA.

Yesu hakuja ili sisi tumtumikie ingali ni mfalme na Bwana wa Yote wala pasipo yeye sisi hakikufanyika kitu yaani chanzo cha kila kitu anakuja kututumikia sisi, ni upendo wa namna gani huu? Hakutaka malipo kwetu wala hakujiinua! Toa nafsi yako kwa ajili ya wengine (kutoa nafsi yako si kufa tu mstari huo hautafsiriki hivyo)

Maana yake ni kujitoa kwa ajili ya wengine kuwahubiria neno la Mungu na kuwaokoa na hukumu ya milele huko ndio kutoa nafsi yako kwa ajili ya wengine ili nao wawe ni warithi pamoja na wewe. Kubali kupoteza muda wako kwa kuingia mtaani, mtandaoni kuwahubiria watu injili.

Naimani kuanzia sasa utaanza kuuteka ufalme wa Mungu ukuhudumie na kukusikiliza utaanza kutoa matokeo makubwa sana. NIMEKUOMBEA KATIKA JINA LA YESU.

ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *