Chamchela ni nini kama ilivyoandikwa na kutumika katika biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Chamchela ni upepo mkali unaovuma kwa Kasi kiasi cha kupeperusha na kuzoa kila kitu kwa muda mfupi yaani kisulisuli.

Tunaweza tukajifunza zaidi na kupata maana iliyo Bora zaidi katika neno la Mungu ambalo ni hili.

Zaburi 58:9 “Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipepeiliyorusha kama chamchela, Iliyo mibichi na  moto. ”

Isaya 29:5 “Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula

6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao”.

 

Chamchela ambayo ni kisulisuli ni njia mojawapo inayotumiwa na Bwana Mungu kujidhihirisha kwa watu wake kuwa yeye ni mkuu kuliko wote na pia hutumia njia hiyohiyo kudhihirisha hasira yake kwa wao watendao dhambi ambayo ni uasi mbele za Bwana pia katika hii njia huwarejeza wale wanaopotea katika njia mbaya na hata kuwaonya wale wanaofanya kinyume na mapenzi ya Mungu huku wakijua kuwa ni kosa lakini Bado wanakuwa wakiendelea kufanya uovu hivyo Bwana hutumia kisulisuli ili kuwajengea na kuwatengeneza zaidi.

Pia turejee maneno haya ya uzima tuone Bwana kile anachohitaji tujifunze kutoka kwake.

Ayubu 38:1 “Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema

2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa”?

Pia aliweza kunitumia njia hii kuonyesha ukuu wake kwa waovu na jinsi anavyoweza kuwaangamiza kwa mfano wa kisulisuli.

Isaya 41:16 “Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia Bwana, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli”.

Yeremia 23:19 “Tazama, tufani ya Bwana, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni dhoruba ya kisulisuli; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani. 20 Hasira ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa”.

Hivyo inatupasa tuuishi utakatifu na kumpendeza Mungu kwa kuwa watii mbele zake na kushika amri za Bwana Yesu huku tukiutunza utakatifu wetu kwa kutenda mema Kila wakati ili tuone Mungu akijifunua kwate kwa upole na kwa utulivu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *