Fahamu adui yako mkubwa ni nani?.
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Hili ni somo muhimu sana kwako tafadhari chukua muda wa kulisoma na kutafakari litakufungua mahali pakubwa sana usiwe mvivu.
Wengi wetu tunafahamu adui wetu mkubwa ni Shetani,miili yetu(haipatani na mambo ya rohoni). Au wanadamu wenzetu ambao wanatumiwa na ibilisi kwa namna moja au nyingine.
Lakini ukweli ni kwamba Shetani,miili yetu, wanadamu wenzetu sio maadui wako/ wakubwa sana kwa wewe uliyemwamini Yesu Kristo bali yuko adui ambae ni mkubwa sana na huna budi kuwa makini sana na kuchukua hatua dhidi yake.
Adui mkubwa wa Mwamini ni UJINGA. tutaona kwa namna gani. Ujinga ndio adui namba moja hebu tutafakari mstari huu..
Hosea 4:6“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”
Umewahi kuutafakari kwa kina mstari huu? Anasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa…” hasemi “WATU WANGU WANAANGAMIA”
Kumbe chanzo cha watu hao kuamgamizwa ni kwa sababu ya kukosa maarifa. Tafsiri ya kukosa maarifa ni ujinga. Ujinga unaweza kumpelekea mtu katika uangamivu mkubwa sana.
Shetani mara nyingi anawatesa watu waliomwamini Yesu Kristo kwa sababu ya wao wenyewe kukosa maarifa ndani yao ya kutosha kumhusu Mungu.
Utakuta Mkristo anapoanguka katika dhambi au kukosa katika eneo fulani na dhamiri yake inapomshitaki Shetani anatumia nafasi hiyo kuanza kumwambia.
“Mungu tayari ameshakuacha.. hawezi kukaa na wewe tena. Umekosa pakubwa sana na mara nyingi sana wewe Mungu ameshakuchoka hubadiliki nk”
Maneno mengi sana yatakuja kwenye akili zako na utajikuta unakata tamaa na anaona kweli Mungu hayuko pamoja nae anaanza kuhangaika na kukosa tumaini..
Wakati maandiko yanasema..
Yeremia 31:3“Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.”
Mungu ametupenda miele sio kwa ukamilifu wetu bali tukiwa na madhaifu yetu. Yeye siyekuwa na madhaifu ni yupi? Madhaifu yetu hayafanyi Mungu akatuacha ikiwa tuna nia ya kumpendeza yeye.. tutakosea na pale tunapotambua makosa yetu na kumrudia yeye anatusamehe bila ukomo tena pasipo kuchoka..
“Mungu hachoki kutusamehe” pale tunapomrudia na kutaka msaada wake.. nini sisi na fikra zetu ndio zinazotufanya tuone Mungu yupo mbali na sisi na hawezi kutusamehe.. siku zote liamini neno la Mungu usiamini hisia zako na mtazamo wako amini Neno limesema nii basi ishi nalo hilo kwa kuliamini.
Ujinga ndio unampelekea mwamini kutenda dhambi fulani kwa kutokujua madhara ya dhambi hiyo atakapoifanya ndio hapo anapofanya dhamiri itamshitaki ndani yake..
Dhamiri kukushtaki sio kukufanya uone hufai unatakiwa kwenda motoni la! Bali dhamiri inapokushitaki inakutaka ubadilike usiendelee kwenda katika njia hiyo. Lakini hapo hapo shetani kupitia fikra zako atakwambia wewe umeshafeli huwezi sikilizwa na Mungu tena.
“Elewa Mungu hajatupenda na ukamilifu wetu bali na udhaifu wetu ili ili tumuangalie yeye na kumtegemea yeye ili atufanye kuwa imara..”
Maandiko yanasema..
1 Yohana 1:9“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”
Katika Biblia ya Amplified inasema..
1 Yohana 1:9 [9]Ikiwa [kwa hiari] tunakiri kwamba tumetenda dhambi na kuziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki (kweli kwa asili yake na ahadi zake) na atatusamehe dhambi zetu na [kuendelea] kutusafisha na mambo yote. udhalimu [kila kitu kisichopatana na mapenzi yake katika kusudi, mawazo, na matendo].
Kwa hiari tunapokubali kukiri na kuungama dhambi zetu na kumaanisha kuacha kweli.. yaani kudhamiria kabisa kikamilifu basi yeye ni mwaminifu a aturehemu haijalishi tumefanya nini na na ataendelea kutuosha na udhalimu wetu wote sio siku moja bali ni mwendelezo..
Tunakosea kila siku(ikiwa inapita siku unasema leo hujatenda kosa basi kweliunajidanganya.. Bali kila siku tunamkosea Mungu pasipo kujua na kila siku Mungu anatusamehe Rehema zake hazikomi)
Lakini kwa kukosa maarifa tunaona Rehema za Mungu zina ukomo lakini sivyo..
Zaburi 103:11“Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.”
Ujinga ni kitu kibaya sana.. kuwa na maarifa ni wewe kila siku kuendelea kujifunza. Kusoma Biblia. Kusoma vitabu vya watumishi wa kweli mbali mbali utaona ujinga unaanza kutoweka na maarifa yanaanza kuingia ndani yako wala hutatikiswa na uongo wa adui kamwe.
Usihangaike kupigana na Shetani hangaika na kuingizà maarifa ya Mungu mengi zaidi ndani yako.
Paulo na kusoma kwake hata alipokuwa mzee bado alimuagiza Timotheo mwanae katika imani ammeter vitabu vyake vya ngozi ili aendelee kusoma na kujifunza zaidi.. Yesu Kristo mwenyewe alikkuwa na maarifa mengi kuliko mtu yeyote hapa dunia kabla yake yeye na baada yake yeye hakuna..
Si kwamba alizaliwa nayo. Nataka nikwambie Yesu Kristo alizaliwa kama watoto wengine hakuwa anajua kusoma wala kuandika yaani kichwani alikuwa hana kitu chochote lakini alikuwa ni mtu wa kusoma sana na kuuliza waalimu ili azidi kujifunza zaidi matokeo yake akawa mtu mwenye ufahamu mkubwa sana wala hakwenda kusoma shule kwa muda mrefu la.
Hivyo ndugu yangu Shetani anatumia ujinga kwa wewe kukosa maarifa ili aendelee kukutesa ikiwa utakuwa na maaeifa hataweza hata kidogo.
Ndio maana Bwana Yesu katika huduma yake hakuwa anahangaika na Shetani bali alikuwa anahangaika na wanafunzi wake kwa kuwafundisha ili kuhakikisha wanakuwa na maarifa ya kutosha ndani yao kuhusu Mungu.
Ujinga una gharama kubwa anza kuingiza maarifa. Soma sana biblia, vitabu,uliza maswali omba sana. Utaona unafunguka kwa sehemu kubwa sana tatizo letu ni wavivu wa kujifunza ndio maana hatumuelewi Mungu katika utimilifu wote anasema na sisi kutokana na kiwango cha maarifa tulichonacho.. haendi nje na hapo maana tutuwezi kuelewa.
Lakini tunapokuwa na maarifa mengi ndani yetu inampa nafasi na wigo mpana Roho Mtakatifu kusema na sisi katika kiwango cha juu zaidi kupitia maarifa tuliyonayo anajua namna ya kutufundisha zaidi.
Naimani kuanzia leo utaanza kuwekeza Muda wako Mwingi katika kuingiza maarifa yanayohusiana na Mungu zaidi.
Nimekuombea katika jina la Yesu Kristo adui huyu umeshakwisha kumshinda na Mungu wa Mbinguni atakujaza nguvu nyingi ili umelewe vyema hutatawaliwa tena na ujinga. Unapojifunza unaondoka ujinga na kupata ufahamu mpya.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.