Hamjui mfano huu basi mifano yote mtaitambuaje?.
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima!.
Bwana Yesu sehemu zote kama maandiko yanavyosema hakunena chochote pasipo mfano. Katika kila jambo alilokuwa anataka kuwafundisha makutano na wanafunzi wake alinena kwa mfano.
Hata sasa Yesu Kristo ananena nasi kwa mifano kupitia Roho Mtakatifu bahati mbaya watu wengi sana hatuelewi ni kwa namna gani ananena nasisi kwa mifano.
Na hii inatuonyesha ili tuweze kumuelewa Mungu kwa wepesi zaidi hatuna budi kuangalia vitu vya asili ili kumuelewa Mungu. Ili tuweze kumuelewa Bwana Yesu vizuri hatuna budi kutafakari sana mifano au kutafakari maisha ya kawaida kabisa na vitu vya asili ili tuwezeshe kuhusianisha na mambo ya rohoni.
Ni vigumu sana kuuelewa ufalme wa Mungu ukoje kama tutashindwa kuvitafakari vitu vya asili vinavyotuzunguka.
Ndio maana hapo Yesu anawaambia kama wanashindwa kuelewa mfano huo wataelewaje na mingine? Ikiwa na maana kuwa mazungumzo yake yote yameegemea kwenye mifano tu.
Mfano tunaona mtume Paulo anawaandikia Wakorintho kuhusu ufufuo wa wafu utakuwaje kwa sehemu walikuwa hawaamini kama mtu akishakufa atafufuka vipi? Haya ni maswali ama mashaka waliyokuwa nayo na mtume Paulo anawaandikia barua na kuwaelezea juu ya jambo hilo linakuwaje..
1 Wakorintho 15 35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;
37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
Pata muda naomba pitia hii sura yote ya 15 utajifunza mambo makubwa sana. Usiwe mvivu..
Mtume Paulo anawaelezea dhahiri kwa mfano wa mbegu kuwa mbegu inayopandwa Haichipuki isipooza kwanza (kufa) baada ya hapo ndio inachipua na kutoa mmea.
Hivyo mambo ya asili yanatupa picha kamili ya mambo ya rohoni.
Yohana 12:24“Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.”
Bwana Yesu anawaambia hapa kwa mfano wanafunzi wake ni sawa na mtu anaepanda mahindi katika shimo moja atapanda mbegu mbili au moja lakini ikishachipua na kuzaa haizai mbegu moja bali mbegu nyingi zitatoka pale.. ndio hivyo hata mfano huo ulikuwa ukifunua kuhusu yeye atakapokufa na kuondoka duniani hapa Roho Mtakatifu atakuja na atakuwa ndani ya kila mwamini. Kitu ambacho zamani kilikuwa hakipo.
Hata katika mfano wa wana wali 10 wapumbavu na welevu.. vivyo hivyo anazungumzia kwa njia ya mfano kuelezea kitu kilichohalisi.. Mungu atusaidie sana katika kizazi hiki.
Wako Wakristo ambao wao ni jumapili kwa jumapili kanisani.. si waombaji,hawataki kujazwa Roho ili waenende kwa Roho, hawana kiasi, wakujitenga tenga tu na wenzao hawana mafuta ya kutosha(Hawajajaa Roho Mtakatifu) pale Kristo atakaporudi hawataondoka nae(ni jambo linaloonekana kama masihara hivi lakini ni uhalisia huo uliopo) ukweli dhahiri umewekwa njia ya mifano ili tuelewe.
Hivyo ni vizuri sana tutumie Muda mwingi kutafakari mambo ya asili ipo injili kubwa sana ya Kristo nyuma yake ambayo itatupa picha kamili na namna ambavyo inatakiwa tubadilishe mitazamo yetu na kumfata yeye kwa nguvu zote.
Penda kutafakari mambo ya asili na imani Mungu atakufunulia ili uelewe katika kila kitu unachokiona ni injili gani ya Kristo iko nyuma yake.
Maana biblia kwa sehemu kubwa imeandikwa kwa mifano mifano kila mahali ili kutupa wepesi wa kuelewa vyema Bwana atusaidie tusiwe wavivu wa kutafakari na kukaa uweponi mwake..
Mwambie Roho Mtakatifu nahitaji unifundishe na uniongoze kwa imani kabisa yupo karibu yako na fungua moyo wako tu ili uweze kupokea neema na nguvu ya kumuelewa na kutembea katika mapenzi ya Baba.
Nimekuombea kwa jina la Yesu Kristo na Mungu atakupa neema ya kuelewa vizuri zaidi na kutembea katika mapenzi yake.
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.