Timiza wajibu wako.

Biblia kwa kina No Comments

Timiza wajibu wako.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Wakristo wengi wanataka kusaidiwa kutimiza wajibu wao..

Kama mwamini uliesamehewa deni la dhambi bure katika Kristo Yesu una wajibu wakufanya. Vivyo hivyo Mungu anawajibu wa kufanya kwa sehemu yake.

Mungu anawajibu wa kufanya katika maisha yako lakini pia wewe una wajibu wa kufanya kwa ajili yake na kwa ajili yako pia.

Wakristo wengi hawatimizi/kufanya wajibu wao.. wanataka kila kitu Mungu awafanyie jambo ambalo haliwezekani.. hata Mungu alipomuumba Adamu na kumuweka katika Bustani ya Edeni alimpa jukumu la kufanya.

nalo ni kuhakikisha anaitunza bustani ile. Lakini Adamu halikuwa jukumu lake kuidizaini iwe na muonekano gani lakini lilikuwa ni jukumu la Mungu.

Mungu ameshatimiliza majukumu makuu katika maisha yetu sisi kwa kumtuma mwanae Yesu Kristo kufa kwa ajili ya dhambi zetu(Yohana 3:16) na si hivyo tu hata kabla hatujazaliwa Mungu ameshakwisha kutujua. Lakini hakuishia kutujua tu lakini pia jukumu lake/wajibu wake ni kututakasa katika Kristo Yesu(Yeremia 1:5).

Sasa wajibu wako ni nini unaotakiwa kuufanya? 

Kama mtu uliezaliwa mara ya pili una wajibu wa kufanya kwa ajiri yako na kwa ajiri ya Mungu.  Tutatazama baadhi ya majukumu ambayo unatakiwa kuyafanya.

Mathayo 7:7“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;”

Bwana Yesu anawaambia wanafunzi wake pamoja na makutano wajibu wao ni nini au wanatakiwa kufanya nini!.

1.kuomba.

Huu ni wajibu Wangu mimi na wewe.. ni jambo ambalo sio la kufanya kwa hiari la!. Bali ni la lazima kulifanya kama ilivyo kwa chakula mwili ni suala la lazima sio hiari usipokula utakufa. Vivyo hivyo usipokuwa muombaji utakufa kiroho ni lazima uwe ni muombaji.. maombi ni chakula cha mtu wa rohoni kama akikikosa ni lazima atakufa kama vile mwili usipokula lazima utakufa.

Kula sio chaguo/hiari ndio maana maandiko yanazidi kutusisitiza..

1 Wathesalonike 5:17“ombeni bila kukoma;”

Maandiko yanasema pia..

Luka 18:1“Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.”

Katika kuomba ndio unapokea pasipo kuomba hutapokea kitu chochote maombi ni nguzo muhimu katika Ukristo wako wala huwezi kusimama na kuifanya kazi ya Mungu.

Anaendelea kutoa ufafanuzi..

Mathayo 7:8“kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”

Kila anaeomba anapokea unaona kama hupokei kwa sababu unataka kitokee ulichoomba kwa jinsi ulivyokitengeneza katika akili yako kitatokeaje..

2.Kutafuta.

Ni wajibu wako kutafuta, wala hakuna ataekusaidia kutafuta ni wewe.. kama ilivyowajibu wako kutafuta fedha ndivyo wajibu wako pia sana katika kumtafuta Mungu.

Kama ulivyona bidii katika kutafuta fedha ndivyo inatakiwa uwe na bidii zaidi katika kutafuta mambo ya rohoni na ahadi ni hii ukitafuta utapata HALELUYA.!

Unatafuta hupati kwa sababu unatafuta kwa nia yako Mwenyewe uvitumie katika ubatili na hutafuti katika nia ya Kristo kama maandiko yanavyosema..

Yakobo 4:3“Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.”

Lakini pia ni jukumu lako kwenda kuwatafuta kondoo waliopotea na kuwaleta katika zizi(Wokovu waefahamu Yesu Kristo).

Hili jambo limekuwa mzigo na gumu kwa Wakristo wengi wanaona ni wajibu es mchungaji,Shemasi,wazee wa kanisa nk lakini ukweli ni jukumu la kila mmoja mmoja.

Mathayo 28:19“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”

Ni jukumu lako kuwavuta watu kwa Kristo na kuwafundisha wamjue Kristo nataka nikwambie kutafuta Pesa sio jukumu kubwa ulilonalo hilo ni jukumu la kawaida sana lakini wajibu mkubwa ulionao ni kuhubiri injili na kupitia injili basi Bwana atakupa hata mahitaji yako maana hayo Bwana anayaita ni mengineyo.

3.Bisha.

Ni wajibu wako kubisha mpaka mlango ufunguliwe na ukweli ni kwamba ukibisha utafunguliwa.

Kuna mambo hayatafunguka kwa kuyaombea mara moja tu.. Kuna mambo yanahitaji nguvu ya ziada kukaa zaidi mlango huku ukiendelea kubisha mpaka alieko ndani afungue(kaa katika maombi kwa muda mrefu unapoomba jambo unaona halitokei usiondoke magotini fanya kuwa ni maombi endelevu na hakika utaona yatatokea tu).

Kuna mambo hayapatikani kwa wepesi yanahitaji udumu katika kuyaombea mfano uamsho, wokovu kwa watu wote kama vile Familia nk.. wakati mwingine ni mambo yako binafsi nk.

Kila aombae atapewa,abishae atafunguliwa na atafutae ataona.. ni uhakika tumepewa na neno la Mungu ni hakika wala halidanganyi.

Ndugu usisubili kuombewa omba Kristo yuko ndani yako una nguvu (sijamaanisha usiombewe na wengine ila hiyo iwe ziada), usisubili kutafutiwa tafuta utapata, usisubili mtu akusaidie kubisha.. bisha utafunguliwa unaembishia mlango akufungulie si kwamba anaweza kuwa hayupo la! Lakini yupo muda wote/siku zote..

Nimekuombea kwa jina la Yesu Kristo neema ya kutimiliza wajibu wako katika mwili wa Kristo ili ujengwe.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *