SEHEMU YA NNE(04).
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele karibu katika mwendelezo wa somo hili.
Ikiwa hukupata sehemu ya kwanza na ya pili na ya tatu, basi wasiliana nasi kwa ajiri ya kupata sehemu zilizopita.
NB: unapomaliza kusoma omba.
Leo tutakwenda kutazama kanuni ya nne (04).
4.kanuni ya kujidhabihu.
Kama tunavyofahamu dhabihu ni sadaka zilizokuwa zinateketezwa kwa moto mpaka ziishie kabisa.
“Utoaji unaomgusa Mungu uaambatana na kuteketea kwa sadaka” tutafahamu ni kwa namna gani.
Siku zote unapotoa sadaka kwanza unakuwa umefanya uamuzi wa kuitoa sadaka hiyo(kanuni ya kuchagua) na hapo unakuwa umefanya kuhamisha umiliki wa hicho kitu kukipeleka kwa mtu mwingine(Mungu au mtu uliekusudia kumpa) maana yake hicho kitu kinakuwa sio mali yako tena.
Sasa mchakato huu huo ni mgumu sana kwa watu wengi na ndio hapo sadaka za watu wengi zinapoteza mguso kwa Mungu kwa sababu hawajajidhabihu japokuwa wamaonekana wametoa. Sasa hapa tutajifunza jambo dogo ambalo naimani litakusaidia..
Nini maana ya kujidhabihu? Ni kukubali kwa hiari kuhamisha umiliki wa kile ulichonacho kuwa mali ya mtu yule unaempa. Ni hari ya kutoa kitu chako unachokipenda kwa hiari kwa ajiri ya mtu mwingine akimiliki kiwe chake na akifanye atakavyo pasipo wewe kuwa na uamuzi juu ya hicho..
Sadaka hii inaanza kuwa na mvuto pale tu inapoteketea kweli katika moyo wa mtoaji.
Maandiko yanasema…
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza, Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
Unaona hapo anasema “….iwe dhabihu iliyo hai, Takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibada yenu yenye maana..” kwa nini mwandishi asiseme tu “itoeni miili yenu iwe dhabihu ndiyo ibada yenu yenye maana.”
Lakini anasema iliyo hai maana yake kuna dhabihu zisizo hai na zisizompendeza Mungu na bado sio Takatifu mbele za Mungu. Roho Mtakatifu akupe kulifahamu hili tutaendelea kujifunza zaidi..
Neno dhabihu lililotumika hapa katika lugha ya kiingereza ni sacrifice yaani kutekeza au sadaka iliyotolewa kuchinjwa. Anaposema tuitoe miili yetu kuwa dhabihu iliyo hai alikuwa na maana waifanye miili yao kuwa kama sadaka iliyochinjwa japo inaishi kwa ajiri ya Mungu, Haleluya.
Hiki ni kiwango cha juu sana kukubali kuuteketeza mwili(kwenda kinyume na mapenzi yote ya mwili uasherati, wivu,husuda,nk) ili uweze kumpendeza Mungu.
“Sadaka inaanza kuwa na mguso pale tu inapoteketea katika moyo wa mtoaji”
Tukianza kumuangalia Mungu mwenyewe alifanya nini juu ya mwili wake kwa ajiri yetu sisi.
Warumi 8:32 “Yeye [Mungu] ambaye hakumhurumia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote…”
Unaona hapo anasema “hakumhurumia…” Lakini anaendelea kusema tena..
Isaya 53:4, 5, 10 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa makosa yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona… Lakini BWANA aliridhia kumchubua; amemhuzunisha; …”
Kwa sababu Mungu alikuwa amedhamiria kumfanya Yesu Kristo kuwa dhabihu hakujali kufanya lolote kwake kwa ajiri yetu sisi ni upendo mkuu sana huu.
Hivyo ili bidi Mungu amfanye Yesu Kristo kuwa sadaka iliyoteketezwa ili aukomboe ulimwengu.
Mungu alikubari kumtekeza Bwana Yesu na kumuacha kabisa kama Yesu Mwenyewe anaposema pale msalabani..
Mathayo 27:46 “…Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Hapa sasa Yesu akawa ametengwa kabisa na Mungu. Na mwisho biblia inasema Yesu “akaitoa roho” yaani akakubali kuwa mbali na Uungu. Jaribu kufikiria kidogo, hivi unafikiri jambo hili lilikuwa jepesi, HAPANA.
Nini nataka ujifunze hapa, ilimbidi Mungu amfanye Yesu kuwa dhabihu iliyoteketea ili akamilishe lengo lake la kuukomboa ulimwengu. Kama asingefanya hivyo mpaka leo ulimwengu ungekuwa haujaokolewa hata kama Yesu alishatolewa sadaka.
Ili sadaka iwe na matokeo lazima wewe unayeitoa uitoe na kuisahau kabisa. Na hili si jambo rahisi kwa watu wengi.. ni kweli wanatoa lakini bado wanakuwa na maswali mengi juu ya kile walichokitoa.
Mfano leo hii utamsikia mtu anasema “tunatoa zaka kwani hizo zaka zinaenda wapi? Au zinatumikaje?” Au “yule mtu nimempa nguo anaivaa tu hata haifui, sitarudia kumpa kitu changu nguo nimempa juzi juzi tu kashaipausha nk”
Maana yake ametoa kile kitu mwilini Kweli lakini bado anacho moyoni mwake.
Nataka nikwambie “ kama hutakubali kuiondoa sadaka moyoni mwako hata ukiitoa ni sawa na kazi Bure”
Nataka kusema hivi, si vibaya kuwa na maswali kama haya. Lakini kama kile utakachotoa kitakuwa kinapiga kelele ndani yako baada ya kutoa, hiyo ni dalili kwamba kile kitu kipo bado kwako.
Umekitoa tu katika hali ya mwili lakini kipo bado moyoni mwako. Mungu anataka vitu ambavyo tunavitoa kuanzia moyoni, vitu ambavyo tukivitoa tunavisahau kabisa.
Utoaji lazima kwanza uanzie moyoni si kwa mhemko lakini kwa kudhamiria wewe mwenyewe bila kusukumwa na mtu tujifunze jambo moja hapa..
Mwanzo 22
9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.
11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Maswali yangu ni, kwa nini Mungu asingemwita baada tu ya kuonyesha utii wa kukubali kumtoa Isaka? Au baada ya kusafiri hata siku mbili basi? Au baada ya Isaka kumwuliza yu wapi mwanakondoo? Au baada tu ya kujenga madhabahu na kuweka kuni juu yake, na kumwambia maneno haya?
Kwa nini Mungu asubiri mpaka Ibrahimu aonyeshe hatua ya mwisho kabisa yaani kuchinja ndipo amwite? Unafikiri kwa nini Mungu alichagua kufanya hivi?
ni kwa nini Mungu alichagua kufanya hivi? “Mungu hana shida na sadaka ikiwa mkononi mwako, ana shida na sadaka hiyo ikiwa moyoni mwako.”
Nilipoendelea kujifunza nilipata majibu haya; Mungu alitaka katika Moyo wa Ibrahimu kusiwe na mtu anaitwa Isaka. Naam, kwa hatua ile ya kukubali kumchinja ni dhairi kabisa kwamba Isaka alikuwa ameteketea kabisa moyoni mwa Ibrahimu.
Nimejifunza pia jambo, kwamba Mungu hakuwa na shida na Isaka kwa maana ya mwili wake, alikuwa na shida na Isaka aliyekuwa moyoni mwa Ibrahimu.
Mungu hana shida na sadaka yako ikiwa mkononi mwako, ana shida na sadaka hiyo ikiwa moyoni mwako. Kama Ibrahimu asingemteketeza Isaka moyoni mwake asingekuwa na ujasiri kabisa wa kumchinja. Ni baba gani anaweza kumchinja mtoto wake wa pekee? Huku ni kujidhabihu kwa kiwango cha juu sana.
Na kwako ni vivyo hivyo, kama hutokuwa tayari kuiondoa sadaka moyoni mwako hata ukiitoa ni sawa na bure, kwa sababu itabaki moyoni mwako. Na hiyo haitakuwa sadaka yenye mguso. Mungu akusaidie.
Naimani katika kanuni hii umejifunza jambo jipya tena.. nimekuombea kwa Jina la Yesu Kristo moyo wa kujidhabihu kwa Bwana.
Uwe na utekelezaji mwema kusoma tu na kuelewa haitoshi. Soma,elewa,tenda. Mungu anakupenda sana.
Ubarikiwe sana.
Mawasiliano 0613079530.
@Nuru ya Upendo.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.