USIVAE MAVAZI YA KIGENI

Biblia kwa kina No Comments

 

USIVAE MAVAZI YA KIGENI

Sefania 1:8 “Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa MAVAZI YA KIGENI.”

Katika ukiristo mavazi ya kigeni ni yapi?

Neno la Mungu linasema..

Mathayo12:33 “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, KWA MAANA KWA MATUNDA YAKE MTI HUTAMBULIKANA.”

Mavazi yampasayo mkristo ni mavazi yote ya heshima na adabu yanayoakisi ukiristo wake;

Huwezi kuvaa mavazi ya kihuni na mitindo ya wasanii wa kidunia kama crazy, modo, n.k halafu ukatambulika  kama mkristo, hapana utatambukika tu kama msanii fulani wa nyimbo za kidunia.

Mavazi ya kigeni ambayo hayamtukuzi Mungu bali yanatukuza mambo ya dunia hii mkristo hapaswi kuvaa, kama mkristo fahamu kuwa wewe ni taifa teule la Mungu, hupaswi kuiga na kufuata desturi za kipagani.

1Petro2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”

Katika siku hizi za mwisho shetani ameyaleta mitindo mingi (fashion) ya mavazi ya kigeni, ambazo zinatangaza na kuhubiri injili yake ya kuwavuta watu wengi katika himaya yake.

Mkristo kuvaa mavazi yanayoacha mwili wake wazi, au kuchora maungo yake ni machukizo kwa Mungu. Fashion ambazo zinajulikana kama mgongo wazi, mipasuko, mavazi ya juu-chini, mavazi ya Peplum, Bardot, na mengineyo..hayo ni mavazi ya kigeni ambayo mkristo hapaswi kuvaa.

Biblia inasema…

Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

Kama mkristo je! unavaa nini??

Kumbuka kila mtu atatambulika kwa mavazi yake, dakitari anatambulika kwa mavazi ya udaktari, askari vivyo hivyo, mwanamziki vivyo hivyo na mkristo pia anatambulika kwa mavazi aliyoyavaa. Kwa matunda yake mti hutambulikana.

Kama mkristo usivae mavazi ya kigeni!!

Fahamu tunaishi katika muda wa nyongeza..hizi ni siku za mwisho kweli kweli na Bwana anasema..

Sefania1:8 “Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, NA WATU WOTE WALIOVAA MAVAZI YA KIGENI.

9 Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganifu.

10 Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka mlimani.

14 Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana;..”

Je umempokea Yesu Kristo? Kama bado unasubiri nini mpaka sasa?

Fahamu kuwa umechelewa sana, hivyo usiendelee kukawia kawia, tubu dhambi zako na mpe Yesu maisha yako kabla mlango wa neema haujafungwa.

Maran atha.

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *