CHANZO CHA MATATIZO
Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa iongozayo njia zetu. Biblia inasema “Mjue sana Mungu ili uwe na Amani (Ayubu 22:21)”..Siku zote ukijua sababu ya jambo Fulani basi unapata amani. Amani inakuja baada ya kujua sababu ya jambo Fulani.
Leo tutajifunza juu ya vyanzo vya matatizo, na namna ya kuyatatua. Kama tunavyojua wengi wetu vyanzo vya matatizo mengi ni shetani..huo ni ukweli usiopingika. Lakini je! Shetani analetaje matatizo?.
Ni vizuri ieleweke kuwa shetani hawezi kujiamuria tu kufanya kila kitu ndani ya mtu kama atakavyo, isipokuwa kwanza amepata ithini au mlango wa kukuletea hayo matatizo.
Na mlango peke ambao unamuruhusu shetani alete matatizo kadha wa kadha kwa mtu ni DHAMBI ndani ya mtu basi, wala hakuna kingine…ni hicho tu.
Hivyo ikiwa dhambi haijaondolewa ndani yako, wala usianze hata kuangaika huku na huku kutafuta chanzo cha matatizo unayoyapitia, wala usibaki kumsingizia shetani kuwa yeye ndiye kasababisha, ni kweli yamkini ni yeye, lakini tatizo lipo kwako, wewe Ndio umempa ithini, umemfungulia mlango kupitia dhambi iliyo ndani yako.
Na shetani huwa ana njia kuu mbili za kuwashambulia watu.
1) Anatumia mapepo…Katika njia hii mtu atajikuta tu ameingia matatizoni pasipo kujua chanzo ni nini. Kumbe ni majeshi ya mapepo wabaya yamemvamia.
2) Na njia ya pili anatumia watu..(Na watu atakaowatumia ni aidha watumishi wake wa uongo wanaovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni mbwa-mwitu wakali…au atatumia wachawi na waganga)….atatumia watumishi wa uongo kuwajaribu wale wanaomjua Mungu, na atatumia wachawi na waganga kuwajaribu wale wasiomjua Mungu…au wakati mwingine atatumia vyote viwili kuwajaribu wale watu wanaomjua Mungu.
Yamkini watu wanaotumiwa na shetani kukuharibu, ni wachawi au waganga…na unashindwa kuelewa chanzo cha mambo yote ni nini? Lakini leo fahamu chanzo cha mambo yote sio watu kukuonea wivu, au wachawi kukuchukia hapana!..chanzo cha matatizo yote ni dhambi ndani ya maisha yako.
Dhambi ikiwa ndani yako ulinzi wa kiMungu unakaa mbali na wewe, hivyo usianze kupambana na watu wanaokuchukia, anza kutafuta mzizi wa tatizo ni wapi.
Ukiwa mwasherati magonjwa yatakusumbua na wachawi watakusumbua sana, mapepo yatakusumbua sana hakuna namna utaweza kuwashinda, hata uombewe kiasi gani hakuna namna utaweza kuchomoka mikononi mwao…ukiwa mtazamaji wa pornography na mfanyaji wa masturbation ni hivyo hivyo…ukiwa ni mzinzi, ni mlevie, ni msagaji ni hivyo hivyo, watakusumbua na hakuna namna utaweza kuwashinda…Usidanganywe kuwa kuna mchungaji yeyote duniani mwenye uwezo wa kukuombea wachawi au mapepo yasikufikie wala kukudhuru, wala usidanganyike kuwa kuna maji yoyote au mafuta yoyote ya upako yanayowazuia wachawi wasiweze kufika nyumbani kwako…Usidanganyike kabisa ndugu…
Kitu pekee kinachoweza kufukuza na kuzishinda nguvu za giza juu ya maisha yako ni MAISHA YA UTAKATIFU katika Kristo Yesu, Uhusiano wako na Mungu ni wa kiwango gani, hicho tu! Wala hakuna kingine….Maisha unayoishi ndio yanayoamua ulinzi wa kiMungu uwe juu yako au uondoke.
Fanya uamuzi sahihi leo, usitazame wachawi, wala waganga, kama ndio chanzo cha matatizo yako…wala usiende kutafuta suluhisho kwa kuombewa, wala kupakwa mafuta..Suluhisho lipo kwako ambalo ndio chanzo cha mambo yote…suluhisho ni KUBADILIKA na kuishi maisha ya utakatifu, ambayo hayo yanakuja kwa kutubu kwanza dhambi zako zote, na kudhamiria kuziacha kabisa kuanzia sasa na kuendelea na kwenda kubatizwa na kisha kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye atakusaidia kushinda dhambi.
Ukifanya hivyo, ulinzi wa kiMungu utakuwa juu yako, haihitaji wewe kwenda kuombewa wala kupakwa mafuta, wala kuwaogopa wachawi…Utaishi kwa Amani sana, na wala hakuna chochote kitakachokugusa. Kwasababu nguvu iliyopo ndani yako ni kubwa kuliko ya kwao..Bwana Yesu alisema..
Luka 6.17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;…… watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;…”
Bwana akubariki sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.