
WALA MIOYO YA WATU BADO HAIJAKAZWA KWA MUNGU WA BABA ZAO.
2Mambo ya Nyakati 20:31-33 ”Yehoshafati akatawala juu ya Yuda; alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala, akatawala miaka ishirini na mitano huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Azuba binti Shilhi.
[32]Akaiendea njia ya Asa babaye, wala hakuiacha, akifanya yaliyo mema machoni pa BWANA.
[33]Lakini mahali pa juu hapakuondolewa; WALA MIOYO YA WATU BADO HAIJAKAZWA KWA MUNGU WA BABA ZAO.”
Yehoshafati alikuwa ni miongoni wa wafalme wachache waliofanya mema katika Yuda, yeye aliweka tumaini lake lote kwa Mungu wa Israeli, maadui walipokuja kupigana naye…hakukimbilia kuomba msaada kwa mataifa mengine kama walivyofanya baadhi ya wafalme wengine, yeye alimlilia Mungu na Mungu akamsaidia. Tunasoma
2Mambo ya Nyakati 20:1-4 “Ikawa baadaye, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni,
wakaja juu ya Yehoshafati vitani.
[2]Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng’ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi).
[3]Yehoshafati akaogopa, AKAUELEKEZA USO WAKE AMTAFUTE BWANA; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.
[4]Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA”.
Unaona hapo, Yehoshafati alipopata taarifa kuwa jeshi kubwa la maadui, wanakuja kupigana nao..alielekeza uso wake kumtafuta Bwana wa Majeshi Mungu wa Israeli, alipiga mbiu ya watu kufunga na kuomba Bwana aingilie kati..kwa kuwa alijua ushindi wao upo kwa BWANA WA MAJESHI.
5]Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya;
[6]akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.
[7]Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele?
[8]Nao walikaa humo, wamekujengea patakatifu pa jina lako humo, wakisema,
[9]Yakitujia mabaya, upanga, hukumu, au tauni, au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako, (maana jina lako limo katika nyumba hii), na kukulilia katika shida yetu, nawe utasikia na kuokoa.
[10]Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;
[11]tazama, jinsi wanavyotulipa, wakija kututupa toka milki yako, uliyoturithisha.
[12]Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? MAANA SISI HATUNA UWEZO JUU YA JAMII KUBWA HII, WANAOTUJIA JUU YETU; WALA HATUJUI TUFANYEJE; LAKINI MACHO YETU YANATAZAMA KWAKO.
Yehoshafati alitambua msaada wao upo kwa BWANA; alitambua kuwa wao wenyewe hawawezi pasipo Bwana. Hivyo wakajinyenyekeza mbele za Bwana.
[13]Wakasimama Yuda wote mbele za BWANA, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.
[14]Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya BWANA, katikati ya kusanyiko;
[15]akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; BWANA AWAAMBIA HIVI, MSIOGOPE, WALA MSIFADHAIKE KWA AJILI YA JESHI KUBWA HILI; KWANI VITA SI YENU BALI NI YA MUNGU.
[16]Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli.
[17]Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yu pamoja nanyi.
[18]Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za BWANA Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia BWANA.
[19]Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu BWANA, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.
[20]Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
[21]Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.
[22] NAO WALIPOANZA KUIMBA NA KUSIFU, BWANA AKAWEKA WAVIZIAO JUU YA WANA WA AMONI, NA MOABU, NA WA MLIMA SEIRI, WALIOKUJA JUU YA YUDA; NAO WAKAPIGWA.
[23]Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe.
[24]Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.”
Umeona jinsi ushindi ulipopatikana, kwa kumsifu tu Bwana basi. Wakati mwingine hatuhitaji kukemea sana ni kumsifu tu Bwana wa Majeshi, ndipo ngome za adui zinaporomoka.
Sasa pamoja na kuwa Yehoshafati alijitahidi kumtafuta Bwana na kumtumainia lakini MAHALI PA JUU hapakuondolewa wala mioyo ya watu bado haijakazwa kwa Mungu kikamilifu.
Maana yake watu waliendelea kuvukiza uvumba katika mahali pa juu na kutoa sadaka kwa miungu, jambo ambalo ni machukizo makubwa.
Hata leo hii, habari hizi hazijaandikwa iwe historia ya wana wa Yuda tu, hapana! Biblia inasema mambo hayo yaliandikwa ili kutuonya na kutufundisha sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani (1Wakorintho 10:11).
Ni kweli tunaweza tukawa tunamtegemea Mungu kwa kila kitu, na Mungu anatupigania, lakini mioyo yetu iko nusu kwake na nusu kwingineko.
Tunaweza tukawa tunaomba na kulia, tunahudhuria ibadani kila wiki, tunamtolea Bwana, tunafanya kazi yake n.k n.k lakini hutujakaza mioyo yetu kwake na hivyo hatuwezi kumuona siku ya mwisho. Haijalishi tumemtumikia kwa namna gani, mapenzi ya Bwana sio kwenda tu kanisani kila siku na kumtolea basi, sio kumwimbia tu basi, sio kufanya miujiza kwa jina lake au kusaidia mayatima tu..kwa ufupi mapenzi ya Bwana ni sisi kumpenda yeye kwa mioyo yetu yote na kujitoa kwake kikamilifu, hiyo ndiyo amri kuu na ya kwanza na pasipo hiyo hatuwezi kumuona yeye kamwe.
Mathayo 22:35 ”Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
[36]Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
[38]Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
[39]Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
[40]Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.”
Kumbuka hiyo ni amri sio ombi.
Ukimpenda Bwana kwa moyo wako wote hautamchukia adui yako, utamwombea kwasababu sifa ya upendo hauhesabu mabaya wala hauoni uchungu (1Wakorintho13).
Halikadhalika ukimpenda Bwana kwa moyo wako wote huatavaa mavazi ya aibu wala kuzungumza mazungumzo mabaya kama kusengenya, kutukuana n.k kwasababu upendo haukosi kuwa na adabu.
Ukikaza moyo wako kumpenda Bwana kweli kweli hauwezi kuufurahia uovu bali utakemea na kuwahubiria watendao maovu watubu wamgeukie Yesu.. kwasababu upendo wa kweli haufurahii udhalimu. Na sifa zingine zote kama kuvumilia, kufadhili, kutojivuna, n.k kwa ufupi mambo yote mema yapo ndani ya upendo na huo ndio utakatifu, pasipo huo hakuna atakayemwona Mungu (Waebrania 12:14).
Je! unatii kweli hiyo amri ya Bwana? umetoa moyo wako wote kwa Bwana kweli? Au umetoa nusu tu?
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.