
ASILI YA KUJIPAMBA KWA WANAWAKE
Asili ya mapambo kwa wanawake ni kutoka kwa MAMA WA MAKAHABA, ndiye alionekana akiwa amejipamba kwa dhahabu na lulu, sasa huyu mama wa makahaba ni nani?
Turejee..
Ufunuo wa Yohana 17:1 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
[2]ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
[3]Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
[4] NA MWANAMKE YULE ALIKUWA AMEVIKWA NGUO YA RANGI YA ZAMBARAU, NA NYEKUNDU, AMEPABWA KWA DHAHABU, NA KITO CHA THAMANI, NA LULU, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
[5]Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
[6]Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
Umeona, huyu mwanamke alikuwa amepabwa kwa dhahabu, huyu ndiye chanzo cha wanawake kujipamba katika kanisa, na kanisa limemridhia.
Ufunuo 2: 18 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika;
Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
[19]Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
[20]Lakini nina neno juu yako, ya kwamba WAMRIDHIA YULE MWANAMKE YEZEBELI, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
[21]Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
[22]Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
[23]nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Hapa tunazidi kumjua vizuri huyu mwanamke, ambaye ni mama wa mapambo, machukizo ya nchi. Kumbe! ndiye YEZEBELI ambaye tunamsoma katika Agano la kale, huyu ndiye chanzo cha wanawake kujipamba katika kanisa.
2Wafalme 9:30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; AKATIA UWANJA MACHONI MWAKE, AKAPAMBA KICHWA CHAKE, akachungulia dirishani.
Na hapa, Bwana Yesu anasema kanisa limemridhia huyu mwanamke.
Maana yake, wewe mwanamke unayesema umeokoka na huku umejipamba kwa mapambo ya Yezebeli, umemridhia!!
Wewe dada unayetia uwanja, unayepaka makeups, lipusticks, rangi kucha, na kuvaa hereni, vipini, bangili, pamoja na kupamba kichwa yaani KUSUKA NYWELE, kuweka rangi, wigi n.k na huku unasema umeokoka na unampenda Yesu, fahamu kuwa hukumu imeshatolewa kwa Yezebeli na wafuasi wake wote yaani wanaojipamba kama yeye na kufanya ukahaba kupitia hayo mapambo.
Hivyo leo amua kuvua hayo mapambo na mavazi yote ya kikahaba (suruali, vimini, kaptula, na magauni ya kubana), tafuta sketi ndefu inayostiri mwili wako vizuri, na halikadhalika tafuta mapambo ya ndani yaani utu wema, upole, unyenyekevu, utii maana ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu.
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
Kwahiyo wanawake wa kikiristo wanao ukiri uchaji wa Mungu wanapaswa kujipamba kwa mavazi ya kujistiri na sio mapambo ya makahaba. (1Timotheo2:9)
Huwenda matendo yako kweli ni mazuri, unahudhuria ibadani vizuri, unatoa sadaka, tena pengine we ni mtumishi, una huduma kanisani pengine ni kiongozi wa kwaya, au ni mama mchungaji, lakini kosa tu ambalo unafanya ni kumridhia huyu mwanamke Yezebeli kwa kukubaliana naye na mapambo yake. Lakini Bwana YESU ameshatuonya.
Ufunuo2:19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
[20] LAKINI NINA NENO JUU YAKO, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
Roho ya Yezebeli inawafundisha watu “Kuzini”.. Inawafundishaje?.. si kwa njia nyingine isipokuwa kwa injili ya kwamba “Mungu haangalii mwili anaangalia roho”… Injili hii, inawafanya watu wavae watakavyo..ili lile neno Bwana YESU alilolisema kuwa “amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake” litimie juu yao kupitia yale mavazi ya kikahaba wavaayo.
Dada/mama fahamu kuwa uvaapo mavazi ya kikahaba kama Yezebeli halafu mwanaume akikutamani tayari umekwisha kuzini naye, hata kama hajakushika mkono. (wewe na yeye wote mmezini, na si yeye tu!.. bali hata na wewe, ambaye hujui kama umetamaniwa kwa mavazi yako). Sasa jiulize unapotembea mtaani umevaa nguo hizo za nusu uchi, umezini na wanaume wangapi!
Hivyo jihadhari na injili hiyo ya adui, isemayo “Mungu anaangalia roho na haangalii mwili”.. Ulinde mwili wako usiwe chanzo cha kuipoteza roho yako moja kwa moja jehanumu.
Fahamu kuwa ukishaokoka, mwili wako unakuwa ni hekalu la Mungu (1Wakorintho 3:16-17 & 6:19)
Hivyo jivue roho ya UYEZEBELI.. Mvae BWANA YESU (Warumi 13:14). Hizi ni siku za Mwisho na Bwana YESU anarudi.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.