Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima?.
Kabla ya kufahamu dhambi ni nini inachotaka tuangalie dhambi ni nini?
Dhambi ni nini?
Ni uvunjaji wa sheria/maagizo ya Mungu yaani kutokumtii Mungu.
Pale tunaposhindwa kumtii Mungu hapo tayari hiyo ni dhambi na dhambi inatendeka kupitia Fikra(mawazo mabaya) kutenda nk.
Na dhambi ilipata nguvu(kuingia ulimwenguni) baada ya Adamu na Hawa kukosa kwa kushindwa kuntii Mungu. Ndio kikawa chanzo cha magonjwa,kifo,na matendo yote mabaya chanzo chake ni dhambi.
Sasa ni nini dhambi inachotaka kwako?
Maandiko yanasema dhambi inataka/inadai mauti juu yako yaani uangamie kabisa milele katika ziwa la moto.
Warumi 6:23“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Unaona hapo? “Mshahara wa dhambi ni mauti;…” hivyo mtu anapotenda dhambi maana yake anafanya kazi namalizo atayapata nayo ni mauti ya mwili na ya roho. Hivyo dhambi si lafiki kabisa kwa mwanadamu.
Na dhambi kitu inachofanya mtu ni kumtumikisha yaani mtu anaetenda dhambi huyo mtu ni mtumwa wa dhambi.
Yohana 8:34“Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.”
Hivyo mtu anaevuta Sigara,kunywa pombe,kuzini,anaishi na mke asiewake au mume asiye wake, anakaa na boyfriend na girlfriend na wanashiriki tendo la ndoa ni dhambi na dhambi ndio inayomtumikisha(utumwa wa dhambi ni mbaya sana fikiria mtu anakwenda kununua mwanamke anaeuza mwili wake anaenda kuzini nae hajui ana nini na mwanamke anakubali kulala na mwanamume ambae pia hamjui nk nikitu cha kutisha sana).
Hivyo dhambi inataka mauti ikiwa hujaokoka jua kabisa ukifa ni Lazima utakwenda kuzimu wala hakuna msamaha baada ya kufa msamaha unapatikana ukiwa hai..
Lakini Mungu anachotaka wewe usife atika dhambi bali upate uzima wa milele kupitia Yesu Kristo..
Yaani unapomuamini Yesu Kristo unapata ondoleo la dhambi. Dhambi haiondoki ndani ya mtu kwa kutenda matendo mema bila Yesu Kristo, haitoki kwa kuli sana lakini inatoka kwa kumwamini Yesu Kristo.
Na Yesu Kristo ndio dawa pekee ya kushinda dhambi. Bila Yesu Kristo hakuna awezae kushinda dhambi. Hata kidogo hivyo Mungu anataka uwe na uzima wa milele.
Lengo na kusudi la Mungu la kumuumba Mwanadamu kwa sura na mfano wake si kwamba Mwanadamu aishi miaka 80 au 1000 bali aishi milele ila dhambi ndio iliyoleta mauti.
Ndugu fahamu huo uzinzi,wizi,uchawi,uganga,utapeli,kujichubua na kujichua,kuuza mwili wako ili upate fedha kumbuka vina mwisho wake..
Jiulize ukifa katika hali hiyo utakwenda wapi? Kumbuka moto wa miele upo na ukienda katika moto wa milele kamwe utapata mateso huko miaka yote wala mateso hayo hayatakuwa na mwisho.
Lakini ya nini yote hayo ikiwa Mungu ameshatupa neema ni sisi tu kumwamini Yesu Kristo kupokea msamaha wa dhambi na tunapewa Roho Mtakatifu ndani yetu ili atusaidie kuishi maisha matakatifu. Bado hutaki..
Unaendelea kupenda giza ndugu siku tulizonazo hizi zinahesabika na kifo ni kufumba na kufumbua yathamini maisha yako jitafakari. Ziangalie njia zako je zinakupa hakikisho la wewe kwenda Mbinguni? ikiwa hamna huchachelewa bado mpe Yesu Kristo maisha yako leo hii.
Kumbuka ukimwamini Yesu Kristo unafanyika kuwa mtoto wa Mungu na unapewa nguvu ya Kushinda dhambi ndani yako.
Unawekwa huru mbali na dhambi.. ni nini unachosubilia? Je siku ile utasema nini mbele za Mungu? Kwamba hukusikia injili? Usiufanye moyo wako kuwa mgumu amini leo. Tengeneza njia zako mapema leo.
Maisha haya ni mafupi sana ndugu yangu chukua hatua leo.. jua Mungu hachanganywi kabisa wala hadanganywi..
Leo unaenda kwa mganga kesho kanisani kesho disco . Uko bar nk halafu unasema unamwabudu Mungu ndugu sivyo. Unajidanganya tu mwenyewe hapo wala Mungu hadanganyiki wala siku ile hutafunua kinywa chako kujitetea hutakuwa na neno lolote la kusema badilika siku mbaya zinakuja.
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.