Je kuna tofauti kati kushuhudia na kuhubiri ?

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe, nakukaribisha katika wakati mwingine tena wa kujifunza neno la Mungu.

Swali: Je haya maneno mawili Kushuhudia na Kuhubiri yapo na utofauti

Jibu: Ndiyo kuna tofauti katika maneno haya japo yanategemeana, tuangalie maana ya kushuhudia ni nini, kushuhudia limetokana na neno shuhuda, mfano mtu aone jinsi mtoto mdogo alivyo dondoka katika shimo la maji ikasababisha kifo chake, kisha akatoka pale na kwenda kuwaeleza watu jinsi ilivyo tokea hadi mtoto yule akadondoka katika shimo hapo ni sawa na kusema huyo mtu ametoa ushuhuda ameshudia namna jambo lile lilivyo kuwa

Lakini maana ya kuhubiri inabeba vitu vingi, ni pamoja na kuonya, kutoa maoni, kushuhudia nk..

Kwahiyo mtu anayehubiri kuhubiri anazama ndani zaidi, mfano labda mtu kashuhudia tukio kisha akaenda kuwashuhudia mwanzo hadi mwisho kisha akamalizia kwa kutoa maoni nini kifanyike ili kuzuia lile jambo lisitokea tena, au kuonya mambo yanapaswa kuzingatia ili kuepukana na majanga kama hayo, sasa huyu mtu anakuwa ameenda mbele zaidi kuliko yule alisema tu namna tukio lilivyokuwa kisha akaondoka, lakini huyu wa pili yeye ameshudia na ametoa elimu nini kifanyike

Vivyo hivyo nasi tunapotoka kuwashudia watu tusiichie tu kuwaeleza uzuri wa Yesu tukaacha pale pale bali pale tunapomaliza kuwaelezea jinsi anavyonya, au kuonya watu, kinachofuta ni kuwaeleza umuhimu wa Yesu Kristo maishani mwao pale wanapompokea, na hasara za kutompokea, kwa kufanya hivyo tunakuwa tumesaidia zaidi huyo mtu tumemshuhudia na kumhubiria pia

Marko 16:15-16
[15]Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
[16]Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *