Fahamu wajibu wako kama kuhani wa Mungu

Biblia kwa kina No Comments

Fahamu wajibu wako kama kuhani wa Mungu

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu.

Katika agano jipya kila mtu amefanyika kuwa ni kuhani, na Yesu Kristo ndio kuhani wetu wetu mkuu kama jinsi maandiko yanavyo sema.

1 Petro 2:9-10 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.”

Na ukweli ni kwamba ufalme wa mbinguni sio kwa ajili ya nabii,mtume,Mwalimu,mchungaji,au mwilijilisti. Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya makuhani. Kuhani ni nafasi kubwana naya juu zaidi katika ufalme wa Mungu na lazima kama Mkristo ulewe na kutambua kazi ya kuhani ni ipi unatakiwa kufanya nini.

Kila mtu aliezaliwa mara ya pili ni kuhani lakini kwa Bahati mbaya watu hawatambui wao ni wakina nani na nini wanachokufanya.

Sasa kulielewa hili tutasoma maandiko machache tu kisha twende kuangalia mambo machache kwa ufupi.

Ufunuo 5:9-10 “Nao wakaimba wimbo mpya wakisema, Ustahili wewe kukitwa kitabu, na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa uliuwawa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila, na lugha, na jamaa, na taifa; ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

Unaona hapo anasema “…….ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”

Tumefanywa kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu sasa anasema mwisho hapo kwamba “…nao wanamiliki juu ya nchi

Unaona hapo watu ambao wanamiliki na kutawala juu ya nchi ni wafalme na makuhani ndio walio na  uwezo. Maandiko hayasemi kwamba tumekafanywa kuwa manabii,mitume nk hizi ni huduma tu ambazo zipo lakini kusudi kubwa la Yesu kunwaga damu yake ni sisi mwisho wa kusiku kufanywa kuwa ni wafalme na makuhani.

Sasa kama kuhani kuna kazi maalumu za yeye anazotakiwa kuzifanya na kama ukiona zimepunguka ndani yako basi jua kabisa bado hujafanyika kuwa kuhani na huna uwezo wa kumiliki kwa sababu katika ufalme bado unonekana kuwa ni  mtoto na ufalme/ukuhani siku zote haukabidhiwi mtoto aongoze.

1.Kuombea wengine.

Hili sio ombi bali ni wajibu wa kuhani kuombea wengine zaidi kuliko kujiombea yeye kama yeye hii ni hatua ya juu sana ple unapoona kuwa napaswa kuwaombea wengine sana kuliko hata mimi mwenyewe si kwamba hutakiwi kujiombea la! Lakini kuwekeza muda mwingi na kujitoa katika maombi kwa ajili ya wengine.

Angalia huduma ya Yesu Kristo duniani katika vitabu vya njili sehemu nyingi Yesu Kristo katika maombi yake juu ya watu wengine na sio kwa ajili yake tu.

Lakini kama sivyo unaweza kusema huyo alikuwa ni Yesu angalia mitume katika nyaraka zao sehemu nyingi sana wanasema maneno mengi kama haya “tukiwaombea,nk”

Usifikiri kuwaombea wengine unapoteza Muda au hujijengi mwenyewe kuwaombea wengine ndio jia ya kujengwa zaidi na Mungu kuliko hata kujiombea wewe kama wewe.

Angalia watu waliokuwa na tabia ya kuwaombea wengine kama wamewahi kurudi nyuma kiimani utagundua ni watu wenye maendeleo makubwa sana Rohoni na ndio wanazidi kuimarika zaidi angalia mitume kwenye kitabu cha matendo hakuna alierudi nyuma hata mmoja. Ukitaka kuwa imara wekeza muda kuwaombea wengine kwa kumaanisha kabisa sio kutimiza wajibu kwa kuzama ndani sana rohoni.

Warumi 1:9-10 “Maana Mungu, ambaye nimemtumikia kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ndiye shahidi wangu jinsi nisivyokoma kuwataja ninyi katika maombi yangu sikuzote; nikimuomba Mungu kwa mapenzi yake nipate sasa kufunguliwa njia ya kuja kwenu.”

Kwa muda wako soma Waefeso 1:15-16, Wafilipi 1:3-4, Wakolosai 1:9, 1 Wathesalonike 1:2-3

Yako maandiko ambayo ni mengi sana yanayoonyesha maombi ya mitume haya yalikuwa yameegemea wapi.

Je wewe unafanya kazi ya kuwekeza muda mwingim kuwaombea watu wengine? Au maombi yako mengi ni kujiombea mwenyewe ya ubinafsi huwezi ombea wengine kwa kuugua kabisa ninaposema wengine sio watu wa nyumbani mwako la bali ndugu zako katika Kristo wakimemo na maadui zako pia.

Ikiwa hushulutishwi kufanya hivi basi unafanya kazi ya kikuhani ambayo wanafanya watu  waliokomaa katika wokovu wao sio Watoto wachanga tena.

2.upatanisho.

Huu ni wajibu wa kuhani sio ombi kwake ukishajitambua kuwa wewe ni kuhani ni lazima utaanza kuwapatanisha watu na Mungu kama vile Kristo alivyotupatanisha sisi na Mungu. Huu ni mzigo ambao ulikuwa ndani ya Yesu Kristo kama kuhani mkuu na ikapelekea hata kutoa maisha yake kwa ajili ya upatanisho kati yetu sisi na Mungu vivyo hivyo hata sisi kama makuhani inatupasa hata kuhatalisha maisha yetu kwa ajili ya upatanisho.

Kwenda kuipeleka injili kila mahali pasipo kuangalia changamoto kwa sababu mzigo haswa ulioko ndani yako unakusukuma kufanya hivyo. Je wewe kama Mkristo unajitoa kwa muda wako,fedha zako, akili zako, nguvu zako nk kwa ajili ya kuwahubiria wengine injili? Je unaifanya kazi ya Mungu katika mazingira hayo hayo uliyonayo? Ikiwa Hapana jua bado katika nafasi hii hau fit na hutaweza kutawala na kumiliki juu ya falme za giza.

2 Wakorintho 5:18–19Lakini vyote vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi naye kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

Ziko kazi nyingi za kikuhni kwa kadili Bwana atakavyozidi kutupa neema tutazidi kujifunza.

Lakini jambo la Muhimu na la kuzingatia sana sana kuwa msomaji wa maandiko soma Bwana Yesu alikuwa mtu wa namna gani mitume walikuwa watu wa namna gani na kisha anza kuuonyesha shauku yako ya kutaka kubadilika na kuwa ni mtu mwingine hii itakusaidia sana.

Mungu akubariki sana,

@Nuru ya upendo.

Mawasiliano: 0613079530

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *