IKO HATUA MOJA TU KATI YA MIMI NA MAUTI

Biblia kwa kina No Comments

IKO HATUA MOJA TU KATI YA MIMI NA MAUTI

1Samweli 20:3 “Daudi akaapa, akasema, Baba yako anajua sana ya kuwa nimeona kibali machoni pako, naye asema, Yonathani asilijue neno hili, asije akahuzunika; lakini ni kweli, aishivyo BWANA, na iishivyo roho yako, IKO HATUA MOJA TU KATI YA MIMI NA MAUTI”.

Ujumbe huu unakuhusu wewe ambaye maji yamekufikia shingoni na unaona unaenda kuzama, pengine umebakiza tu hatua moja kati yako na mauti, lakini habari njema ni kwamba bado kuna matumaini ya wokovu ndani ya Yesu. Ndiye aliyeandikiwa haya maneno..

Isaya 42:1 “Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.

[2]Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu.

[3]MWANZI ULIOPONDEKA HAUTAVUNJA, WALA UTAMBI UTOKAO MOSHI HAUTAZIMA; atatokeza hukumu kwa kweli.

[4]Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.” (Mathayo 12:20)

Hapo anasema mwanzi ulipondeka hautavunja, wala utambi utokao moshi hautazima; unaelewa maana yake?

Mwanzi, ni shina lolote la mmea, inaweza ikawa ni mti, mchicha, mgonga n.k. Lakini anasema ukipondeka huo, hata kufikia hatua ya kukosa matumaini kabisa yeye anasema hatamalizia kuuvunja..Utambi utoao moshi ni kama umeshazima, yaani utambi ukishafikia hatua ya kutoa moshi tu, ni wazi kuwa huo tayari umeshazima huo, lakini yeye anasema hataumalizia kuuzima, moyo ambao wewe huwezi kuwa nao, huwezi kuwa na tumaini na utambi ambao unatoa moshi tu, tena kikubwa utakachofanya hapo ni kuuzima haraka usiendelee kukotelea moshi. Lakini kwa YESU haikuwa hivyo, yeye bado aliutazama, na kuuhangaikia..Na utambi huo ni sisi, mwanzi huo ni mimi na wewe!

Inawezekana maisha yako ni sawa na mwanzi uliopondeka, umefika hatua, unaona kabisa tayari ulishakosea njia, na hakuna matumaini tena ya kumrudia Mungu, umekuwa mlevi wa kupindukia, unatumia madawa ya kulevya mpaka yamesha kauthiri huwezi tena kuacha.,Umekuwa mwasherati mpaka imefikia hatua umepata UKIMWI, na wewe bado ni kijana mdogo tu na hivyo umekata tamaa ya kuishi, unaona kama jamii haiwezi kuwa na wewe tena, wala Mungu kukupokea kwa mambo uliyoyafanya. Umekuwa katika magonjwa yasiyoponyeka, huna tumaini tena kilichobakia ni kufa tu, Nataka nikuambie, YESU yupo, sio marehemu, kutaka kukusimamisha tena, na kukunyanyua tena uwe mwana Mungu BUREEE!!.

Yeye ndiye aliyetabiriwa maneno haya

Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA AMENITIA MAFUTA niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.

Unaona? Unaweza ukawa ni mdhaifu wa Imani, imefikia wakati unataka kusema Mungu hayupo umekuwa utambi unaotoa moshi, ni hatua moja tu imebaki ya wewe na kukata tamaa ya maisha, umekuwa katika vifungo vya giza, umeingia katika ushirikina, na uchawi, maisha yako unaona kabisa yapo hatarini kutoweka, hujui kama hata kesho utaishi kwa jinsi ulivyo katika vifungo vya hofu, wewe ni utambi unaotoa moshi, pengine unaweza ukawa ulianza vizuri na Kristo huko nyuma ulikuwa moto kweli kweli utambi wako ulikuwa unawaka vizuri huna shida yoyote , lakini wakati ukafika shughuli za dunia na udanganyifu wa mali na anasa vikakusonga, sasa umepoa huna tofauti na watenda dhambi wengine..Yesu ni wa rehema bado anatamani kukuwasha tena uangaze upya. Ametiwa mafuta kwa kazi hiyo.

Ulimwengu utakukatia tamaa, lakini Kristo anakutazama haijalishi umedondoka mara ngapi, Upo katika masononeko ya roho, upo katika tabu na maumivu mbali mbali, Njoo kwa Yesu. Leo hii sema ni mwisho naanza tena na Bwana naye atakupokea, yeye mwenyewe anasema..

Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Ndugu ni nani awezaye kukuahidi mambo mema kama haya kama sio YESU peke yake.?Kwanini kila siku unasikia YESU ni rafiki wa wengine, Na asiwe rafiki yako? Hata sisi tulipokuwa walevi, na wazinzi, na watukanaji, wa endaji disco, watazamaji pornography, tulikuwa katika hofu, japo mbele za watu tulijifanya wenye furaha siku zote, na wenye ujasiri..Lakini siku YESU alipotupa raha nafsini mwetu ndipo tulipojua hakika raha halisi ipo wapi?..Kwahiyo tunafahamu vizuri hali unayopitia wewe uliye katika dhambi, kwasababu na sisi tulikuwa huko, lakini tumeonja huku, na tumejua hakika Bwana ni mwema.

Njoo! Kwa mwokozi wako ambaye ni mwokozi wetu pia, muda unazidi kwenda, moja ya siku hizi UNYAKUO utapita, au kama hautapita basi KIFO kitakukuta, sasa huko uendako ni nani atakuwa mtetezi wako? Kama umemkataa mtetezi wako angani u hai?..Ukimpokea leo atakuwa ni rafiki mwema kwako.

Bwana akuangazie rehema zake.

Ubarikiwe na Bwana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *