Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?.

Biblia kwa kina No Comments

Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?.

SEHEMU YA PILI 02.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.. karibu katika mwendelezo wa somo hili Muhimu sana kwa Mkristo yeyote ulimwenguni.

Katika sehemu ya kwanza tulijifunza kanuni moja ambayo ni kanuni ya umiliki.. “Mungu hawezi akakwambia utoe kitu ikiwa humiliki kitu” yaani hakuna umiliki hakuna utoaji. Sasa leo tutaendelea na kanuni ya pili ikiwa hujasoma sehemu ya kwanza basi nakusihi upitie..

2. Kanuni ya upendo.

nyuma ya utoaji wowote wa kweli upo upendo wa Kweli.” Upendo unamsukuma kitu cha thamani alicho nacho kwa ajiri ya yule ampendae. Hivyo tunaweza kusema.. “ikiwa unampenda mtu ni lazima utampa kitu unachokipenda” yaani maan yake ni lazima kile kitu kwanza ukipende kabla hujampa mtu unaempenda au unaetaka kumpa.. utanielewa baadae nini namaanisha hapa.

Haijalishi utakuwa na vitu vingi kiasi gani lakini kama hautakuwa na upendo ni dhahiri huwezi kuwa na utoaji unaomgusa Mungu. Kuwa na vitu vingi vya kutoa hakukufanyi uwe bingwa wa kutoa.

Unahitaji kuuelewa upendo (sio katika maneno tu) ili uweze kuwa na utoaji unaomgusa Mungu. Zingatia hili…

Hatuwi watoaji kwa sababu tuna vitu vingi vya kutoa bali kwa sababu tuna upendo.”

Upendo wa Mungu kwetu sisi.

Huu ni upendo wenye matokeo makubwa na mguso mkubwa kwa Mungu mwenyewe..

Yohana 3:16.“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Hili ni andiko ambalo Wakristo wengi sana wanalifahamu lakini si wote wanaolielewa kwa undani zaidi.. tutataangalia kwa ufupi.

Kanuni zote tutakazojifunza zimefichwa katika andiko hili Yohana 3:16.. Mungu akupe neema ya kuelewa vizuri kanuni hii.

Kama tulivyojifunza hapo mwanzo kwamba “nyuma ya utoaji wowote wa kweli upo upendo wa kweli.”

Ukisoma kwa makini mstari huo unaanza na UPENDO unamalizia na KUTOA. maana yake pasipo upendo hakuna utoaji wa kweli. Roho Mtakatifu akufunulie hili..

Ikiwa na maana kwa Mungu upendo wake kwetu lilikuwa ni jambo la maana sana kuliko chochote alichokuwa nacho(uumbaji wote) hata uungu wake haukuwa chochote kwake ukilinganisha na upendo wake kwetu. HALELUYA… (rudia tena utapata kitu kikubwa sana na tafakari pia)..

Na ndio maana ikamlazimu kuacha mbingu(kutoa uungu wake) ili iwe fidia kwa ulimwengu wote Glory to God.

Kama ulivyonavyo vina thamani zaidi ya upendo ulionao kamwe huwezi kuwa na utoaji wenye mguso”.

Thamani ya upendo.

Upendo unapaswa kuwa na thamani ya juu zaidi ya thamani ya vile unavyovimiliki. Ukifikia katika hatua hii ndio unaanza kuwa na utoaji hasa unaomgusa Mungu.

Mungu haguswi na wingi wa vitu ulivyonavyo bali anaguswa na upendo ulionao.. upendo ulionao ukizidi hata kutoa vitu vyako vya thamani haitakusumbua.

Utoaji wowote unaomgusa Mungu ni lazima unaongozwa na upendo. Maana yake kitu kinachotakiwa kutusukuma kutoa si wingi/ubora  wa vitu tulivyonavyo/ tunavyovitoa bali inapaswa kuwa ni upendo.

Upendo ninaotaka kuuzungumzia hapa ni lazima uguse katika maeneo makuu matatu..

1.Upendo kwa Mungu. 

2.Upendo kwa unachokitoa.

3.Upendo kwa unayempa kile unachotoa.

1.Upendo kwa Mungu. 

Jambo unalotakiwa kuliweka akili kuanzia leo ni hili.. “ Mungu Mungu havutiwi na wingi wa vitu ulivyonavyo bali anaguswa na upendo ulionao hasa kwake” unaweza kujiuliza ni kwa namna gani? Jibu ni rahis sana..

Jibu ni kwa sababu yeye ndie mmiliki wa vyote yeye ndiye ampaye mtu kwa jinsi apendavyo. HALELUYA..

Unaweza kutoa sadaka nyingi za kila namna zaidi hata ya Sulemani kama utapeleka pasipo upendo ni kazi ya kuchosha na kujilisha upepo tu.

hebu tujifunze jambo moja hapa..

Mwanzo 22

1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

Andiko hili tunalifahamu wengi Lakini umeshawahi kujiuliza ni jambo gani hasa Mungu alikuwa anamjaribu Ibrahimu? Ni nini Mungu alikuwa anataka kukipata?

Jaribu la kumtaka Ibrahimu amtoe Isaka mwanae wa pekee tena wa ahadi aliemgoja kwa kipindi cha miaka 25 tafakari kama ungelikuwa ni wewe..

Hapa Mungu alichokuwa anakitafuta hasa ilikuwa ni kuupima upendo wa Ibrahimu kwa Mungu. Ni kwa kiasi gani Ibrahimu anampenda Mungu? Je! Ibrahimu bado anampenda Mungu kama alivyokuwa hana mtoto? Au upendo wake umehamia kwa kile alichokitarajia kwa miaka mingi? Hili ndio jambo Mungu anamjaribu Ibrahimu..

Je? Bado unampenda Mungu kama kipindi haujapata kazi? Au upendo wako umehamia katika kazi yako?, Mumeo?mke au?

Wakati wote Mungu anataka kuhakikisha katika mioyo yetu tunampenda yeye zaidi ya vile alivyotupa maana tukimpenda yeye aweza kutupa zaidi ya hivyo.”

Kama kweli tunampenda Mungu utoaji halitakuwa jambo gumu kwetu hata kidogo haijalishi Mungu atatutaka tuoe nini.

Tunaona kilichokuwa ndani ya Ibrahimu tunaona upendo wake kwa Mungu ulizidi kuliko upendo wake kwa Isaka. Na tunaona mbele kidogo matokeo yake ni nini tusome…

Mwanzo 22:

12“Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.”

Kwa Ibrahimu Mungu ndio alikuwa nafasi ya kwanza kisha mke,mtoto na mali zake mpaka Mungu anamshuhudia je! Unataka Mungu akushuhudie hivi? Dhamiria ndani yako inawezekana nimekuombea katika jina la Yesu.

Kama tunampenda Mungu kutoa kwetu halitakuwa jambo gumu. Na huu ndio upendo wa kweli kwa Mungu hatuwezi  kusema tunamcha Mungu tusiyempenda(hatuwezi kutoa vitu vya thamani kwa ajiri yake).

2. Upendo kwa unachokitoa.

Jambo hili nililigusia kidogo huko juu hapa tutaamgalia kwa undani kidogo.

Mungu ataguswa tu pale tunapokua tayari kutoa kitu tambacho sisi wenyewe tunakipenda” sio nadharia hili ni jambo la kweli kabisa.. kama unatoa kitu usichokipenda, ambacho unakiona ni cha kawaida tu kwako usitegemee kamwe kumgusa Mungu sahau.

Ukirudi katika Yohana 3:16 maandiko yanasema “ akamtoa mwanae wa pekee.” Maana yake mbinguni na duniani hakuona kilicho na thamani ikamgharimu yeye mwenyewe kujitoa.

Tunachokipenda sana ndicho anachokitaka Mungu.

Tunajifunza jambo kwa Ibrahimu Mungu anamwambia ni nini anachotaka amtolee..

Mwanzo 22:

2.”Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

Hebu tutafakari kwa kina huu mstari angalia maagizo hayo.. anasema Umchukue mwanao haishii hapo anasema mwana wa pekee, lakini haishii mwana wa pekee tu anamalizia na kusema umpendaye anamtaja na jina Isaka. Maana yake Ibrahimu hakuwa na namna ya kuanza kujiuliza ni yupi bali maelekezo yalikuwa wazi kabisa.

Ibrahimu alikuwa na mke mzuri aliyempenda Mungu hakumtaka amtoe huyo, alikuwa na Ishmael hakumtaka pia wote alikuwa anawapenda Ibrahimu lakini Ibrahimu alikuwa anampenda Isaka kuliko vyote.. hapa tunajifunza jambo kumbe Mungu kile tunachokipenda ndio anachotaka tukitoe.

Ukisma Waebrania 11:4 tunaona Habili anatoa sadaka nzuri aliyoipenda kutoka Moyoni hata akamgusa Mungu moyo wake kuliko kaini ambae alitoa ilimradi sadaka tu.

Mwanamke yule alietoa senti mbili pia Soma Luka 7:36-50 alitoa kilichomgusa Yesu mwenyewe mpaka anamshuhudia na tunamsoma hivi leo. Sadaka ya mwanakr yule ilitoka moyoni na kwa upendo kabisa.

Mara nyingi Mungu anatupa maelekezo ya wazi kabisa kama kwa Ibrahimu lakini sisi kwa nia zetu tunakaidi na kupishana na baraka nyingi.. tii kile Mungu anakwambia utaona miujiza mikubwa wala usiwe mzito.

3.upendo kwa yule unayempa kile unachotoa.

Vizurii kufahamu hili.. hakuna sadaka yoyote unayoitoa inafika moja kwa moja kwa Mungu (hapa ndio watu wengi wanapata shida). Unapotoa zaka  unatoa kwa mchungaji wako unapotoa sadaka yoyote ile yule anaezipokea anamuwakilisha Mungu katika kuzipokea si jukumu lako kuchunguza sadaka zako unatoa zunaenda wapi..Jukumu lako wewe ni kutoa na weka akilini umeweka hazina isiyoharibika katika ulimwengu ule ujao..

Kama utampa mhitaji utakuwa umempa Mungu kupitia mhitaji huyo. Na Kama utatoa kwa yeyote yule au sehemu yoyote basi jua yupo anaewajibika kupokea kama muwakilishi wa Mungu.

Kumbuka mahali unapoitoa sadaka yako ni pa muhimu sana kuliko sadaka yenyewe.

Mungu alimtoa Yesu Kristo kwa sababu alitupenda sisi sana kuliko chochote.  Kama Mungu asingetupenda wala asingemtoa Kristo afe kwa ajiri yetu na utoaji wake usingekuwa na nguvu yoyote kwetu lakini sasa utoaji huo una nguvu hata sasa damu ya Kristo inanena mema..

Nimekuombea kwa Mungu upokee moyo wa upendo sawa sawa na watakatifu waliokuwa Filipi kama maandiko yanavyosema…

Wafilipi 4

14 Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.

15 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.

16 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.

 

Usisubiri kuwa na Vingi unahitaji kuwa na upendo na mambo haya si magumu.. amua leo ndani yako..

Pasipo kufanya uamuzi hakuna kitu kitafanyika amua kuingia zaidi katika ulimwengu mwingine wa utoaji unaomgusa Mungu utabadilisha maisha yako ya rohoni na mwilini..

Usikose kujifunza mwendelezo wa somo hili katika kanuni ya tatu ni ya muhimu sana kuifahamu na kuiishi..

Nimekubea kwa jina la Yesu Bwana akufanikishe kukupa na kukupa neema ya kukifanyia kazi hiki ulichojifunza.

Maranatha.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *