Usiishie kujua tu bali jua na kutenda.
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu.
Wakristo wengi sana tunafahau mambo mengi kumhusu Mungu jinsi alivyo na anatutaka tufanye nini!? Lakini bahati mbaya idadi kubwa ya Wakristo wanaishia kujua tu na hawatendi kile wanachokifahamu.. ama hawafanyi vile inavyowapasa kufanya.
Ingawa wanafahamu wajibu wao ni nini. Na hii ni hatari kubwa sana wala si jambo la kawaida maandiko yanasema..
Luka 12:47“Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.”
Wakristo wengi wapo katika kundi hili wanafahamu ni nini kinachowapasa kufanya lakini hawafanyi. Siku ile itakuwa ni kilio na kusaga meno Mungu atusaidie sana tujiweke tayari kuyatenda mapenzi yake.
Siku ile hakutakuwa na namna yoyote ya kujitetea kabisa ikiwa ulifahamu yakupasayo kufanya lakini hukufanya.
Unajua unatakiwa kuwa ni Mtakatifu kama yeye uliyemwamini alivyo Mtakatifu lakini haufanyi hivyo.. unaendeleajee na uzinzi,kujichua,kuangalia picha za uchi, huna kiasi wala hujizuii, unatakiwa uhubiri injili lakini hutaki umekaa tu nyumbani umewaachia wengine wakati na wewe ni jukumu lako kwenda shambani kuvuna roho za watu.
Unatakiwa kuwaombea wengine wasimame,kuliombea kanisa,kuwapenda adui zako na kuwaombea..kuwa mnyenyekevu, kuwarehemu wengine, utende haki usipokee rushwa,wala usiwe msingiziaji,mseng’enyaji,uwe mtu wa haki mwenye kuutafuta kwa bidii kuwa mtaua nk.
Yote haya unafahamu na mengine zaidi ya haya lakini unayapuuzia na kuyaona ni mambo ya kawaida tu na unajitumainisha kuwa uko salama katika Kristo Yesu ndugu hauko salama.
Jitahidi sana kukua na dhamiria ndani yako kila siku kupiga hatua na kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu Kristo na jinyenyekeze chini yake Bwana akupe nguvu ya kusonga mbele na kushinda majaribu na kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Na nguvu hizi tunazipata kwenye maombi na kuwa watu wa kufunga na kuomba.. nataka nikwambie hata ukiwa msomaji wa neno vipi pasipo kuomba utaanguka tu..
Omba sana usipitishe siku bila kuomba utakuwa salama katika Kristo utaanza kupiga hatua nyingine.
Tusijidanganye tumeokolewa kwa neema na tusitake kuwa watu wa haki tutapotea kabisa maandiko yanasema..
1 Yohana 2:29“Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.”
Unaona hapo anasema kama tukijua yeye ni mwenye haki je tuishie kujua tu? Maana yake hata wapagani wanajua kwa namna fulani Mungu ni mwenye haki ni mtakatifu lakini je wanatenda kama Yesu anavyowataka? La sasa ukirudi hapo juu anasema kila atendaye haki!, amezaliwa na yeye..
Hivyo si kusema tu nimemwamini Yesu Kristo halafu bado unaendelea kuishi unavyotaka hutaki kubadirika inakupasa sasa ubadilike.
Kumbuka mbegu ukiyoipokea ndani yako ina asili ya kukua haibaki vile kama ulivyokuwa toka mwanzo bali inakua siku baada ya siku na ni mbegu isiyoharibika. Hivyo jitahidi sana kukua na kuongezeka kwa wewe binafsi kuwa muombaji,msomaji wa neno na kujaa Roho kila siku.
Maama usipojaa Roho itakuwa ni ngumu kutembea katika Roho ni lazima utatembea katika mwili tu. Ambao ni uharibifu.
Nimekumbea na nitamanio langu katika jina la Yesu Kristo usiishie kujua tu bali ukawe ni mtendaji kama maandiko yanavyotaka tusiwe wasikiaji tu bali watendaji..
Amini umelipokea hili katika jina la Yesu Kristo sema Amina kwa imani kabisa.
@Nuru ya Upendo.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.