Kuna umuhimu wowote wa kunena kwa Luga?

Biblia kwa kina No Comments

Kuna umuhimu wowote wa kunena kwa Luga?.

Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe Karibu tuyatafakari meneno ya uzima.

Nini maana ya kunena kwa Lugha?.
Ni kuongea au kuomba kwa Lugha ya kipekee ya rohoni, ambayo haieleweki kwa akili ya kawaida . Lugha hii si Lugha ya kawaida ya binadamu bali ni Lugha ya Rohoni inayoweza kutumika kwa ajili ya Maombi,Sifa(chants), au unabii.

Je? Kuna umuhimu wowote wa kunena kwa Lugha?.

Ndio kuna umuhimu mkubwa sana wa mtu kunena kwa Lugha,  na mtu asiyenena kwa lugha basi kuna mambo ambayo anayakosa katika kujengwa na Roho Mtakatifu.

Kuna faida kubwa sana ikiwa mtu hatafanya hivyo kwa mazoea yaani kuvuta muda wa kumaliza kuomba.

Kuna faida nyingi sana za Mtu kunena kwa lugha na kama mtu akipuuza katika eneo hili kutakuwa na mambo fulani ambayo yanaweza kumchukua muda kidogo kujengwa/kutengenezwa.

Maandiko yanasema…

1 Wakorintho 14:2
“Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.”

Unaona hapo? Anasema “..Mambo ya siri katika roho yake ” ukweli ni kwamba hata mambo hayo ya siri yaliyo katika roho yako huyajui kabisa lakini Roho anayafahamu na anakusaidia kuyaombea kwa kuzama sana ndani.

Umuhimu wa kunena kwa Lugha katika maombi .

Ziko faida nyingi sana katika kunena kwa Lugha. Lakini tutaangazia sababu chache sana ambazo nitazielezea kwa kina kwa msaada wa Bwana.

1.Roho hutusaidia mahali tusipoweza kuomba.

Kuna mahali ufahamu wako hauwezi kabisa kuomba hususani katika hayo mambo ya siri ndani ya roho yako.

Unapoomba kwa kunena kwa Lugha Roho Mtakatifu anatusaidia mahali ambapo fahamu zetu haziwezi kuomba.

Kuna mahali ambapo ufahamu wetu hauwezi kufika wala kuelewa mambo yaliyopo ndani yetu namna ya kuyaombea. Na ni mambo ya Muhimu ambayo tunatakiwa kuyaombea. Ili kujengwa sasa sehemu kama hiyo hata tufanyeje hatuwezi kupafikia isipokuwa Roho Mtakatifu tu.

Ni sawa na mtoto mdogo ambae yeye anapumua tu na hajui hasa ni kwa namna gani anapumua na ni vitu gani vinasababisha apumue halafu unaanza kumwambia aelezee mfumo wa upumuaji jinsi unavyofanya kazi.

Ni wazi kuwa Hataweza japokuwa mfumo wote wa upumuaji upo ndani yake.

Warumi 8

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Unaona hapo? Anasema “..huwaombea watakatifu kam Mungu apendavyo. ” Roho Mtakatifu hutuombea kama vile Mungu anavyotaka na anafanya hivyo pasipo kukosea akiwa na ufahamu wote maana yake maombi yanakuwa na nguvu kubwa sana.

Kwa kiingereza maandiko yansema.

Romans 8:26
[26]So too the [Holy] Spirit comes to our aid and bears us up in our weakness; for we do not know what prayer to offer nor how to offer it worthily as we ought, but the Spirit Himself goes to meet our supplication and pleads in our behalf with unspeakable yearnings and groanings too deep for utterance.

Maana yake…

Vivyo hivyo, Roho Mtakatifu hutusaidia katika udhaifu wetu; kwa sababu hatujui jinsi ya kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe huombea kwa ajili yetu kwa maombolezo na matamanio ya ndani mno—maombi yaliyo ya kina sana kiasi kwamba hayawezi kutamkwa kwa maneno ya kawaida.

Sasa hapo kuna maneno matatu ambayo tutayatazama kwa ufupi yatakayozidi kutupa uelewa zaidi wa ndani

Unspeakable yearnings-Matamanio ya ndani sana yasiyoweza kusemeka. Mfano unapokuwa na matamanio fulani ambayo kwa namna fulani unashindwa hata kuyaelezea.

Groanings – kuugua au maombolezo ya rohoni ya ndani sana.

To deep for utterance -mambo yaliyo ya kina sana kiasi kwamba hayawezi kutamkika kwa maneno ya kawaida.

Unaweza kuona kwamba ufahamu wetu hauwezi kuhimili wala kuelewa inahitajika Roho Mtakatifu.

Lakini maandiko pia yanasema mtu anenaye kwa Lugha hujijenga mwenyewe! Kwa namna gani kupitia kunena kwa lugha unajijenga mwenyewe?

Hili ni tendo la kuwasiliana na Mungu kwa lugha ya rohoni moja kwa moja..

Linamjenga mtu kiroho kwa sababu linaimalisha imani na roho yake ya ndani.

Ni tendo ambalo linajenga sana roho na hasa imani ya mtu. Na mtu ikiwa imani yake itashambuliwa na ni mtu anaena kwa lugha katika maombi kwa Roho basi imani yake itabaki kuwa dhabiti.

Na watu wengi wameegea katika kuomba kwa kunena kwa lugha tu lakini sio katika kuomba pia kwa ufahamu Paulo anasema…

1 Wakorintho 14:15
“Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.”

Unaona hapo Paulo anasema ataomba kwa roho (kuomba kwa lugha ya rohoni ambayo yeye mwenyewe haelewi katika fahamu zake) lakini anasema ataomba kwa akili pia maana yake ni kuomba kwa ufahamu ambapo akili yako inaelewa kile unachokiomba.

Anasema pia ataimba kwa roho(Spirit Chants) Bwana akitujalia tutajifunza nini maana ya kuimba kwa roho?” Maana yake kuna kuimba kwa roho ambapo kuna wakati hajui hasa ni kipi anachokiimba na mara nyingi huwa ni maneno machache yanayojirudia rudia..

Ikiwa unataka kufahamu ni nyimbo za namna gani basi sikiliza nyimbo hizi..

Wimbo “ Spirit chants “ mwimbaji- Victoria Orenze. Pia Dr Ipyana wimbo: Messiah “_ ni aina za kuimba kwa roho.

Lakini anasema nitaomba kwa akili maana yake ni nyimbo kama hizi tunazoimba Tenzi nk ambazo unaelewa kile kinaimbwa/unachokiimba.

Na kunena kwa Lugha hakuhitaji mpaka msukomo wa roho Mtakatifu la! Kuna wakati itakuwa hivyo lakini si mara zote ni muhimu kunena.

Paulo anaposema “….nitaomba kwa roho pia kwa akili, nitaimba kwa roho pia kwa akili..”

Inamaanisha hivi vitu anaweza kuvifanya kwa wakati wowote atao yeye anapokuwa kwenye maombi yaani viko ndani ya uwezo wake kutokana na ufahamu alionao katika Kristo.

Hivyo kuomba kwa roho na kwa akili vyote changanya kwa pamoja usiegemee upande mmoja tu fanya vyote.

Hivyo ni muhimu sana kunena kwa lugha maana ni kwa faida yako unapokuwa kwenye maombi yako binafsi tumia hata masaa2 au limoja kuomba maombi ya aina hiyo yatakujenga na kukuweka katika sehemu nzuri sana ya ukuaji wako kiroho maana utakuwa unajenga imani yako pia n mambo mengine mengi zaidi.

Usinene kwa kutaka kuonekana la! Lakini fanya ukiwa na lengo na nia ya kujengwa na fahamu zako elekeza huko kuwa Mungu anakujenga na kukuimalisha.

Ubarikiwe sana.

Maranatha. .

Mawasiliano 0613079530.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *