KUWA MAKINI TUNAPIMWA KATIKA MIZANI

Biblia kwa kina No Comments

KUWA MAKINI TUNAPIMWA KATIKA MIZANI

2 Samweli 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, NA MATENDO HUPIMWA NA YEYE KWA MIZANI”.

Ndugu matendo yetu yanapimwa katika mizani kila siku yakilinganishwa na ya wengine kama sisi…kizazi chetu kinapimwa katika mizani kikilinganishwa na vizaza vilivyotangulia..

Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”.

Mahali tunapoishi, tunapofanyia kazi tunapimwa…kila tunalolifanya linapimwa linalinganishwa na la wengine. Hata maisha tunayoishi sisi kama wakristo yanapimwa ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”.

Unapovaa suruali binti wa Mungu ambaye umezaliwa katika mazingira ya kikristo, pengine hata baba yako ni mchungaji…na unasema unakwenda mbinguni…ukumbuke kuna mwingine kama wewe mwenye umri kama wa kwako mahali fulani ambaye ni mzuri kuliko wewe na mwenye umbo zuri kuliko lako lakini havai hizo suruali wala vimini, ingawa mazingira yote yanamruhusu kufanya hivyo…yeye ameshinda katika mazingira magumu ya vishawishi vingi lakini wewe umeshindwa katika mazingira marahisi..Jua upendo wako kwa Mungu unapimwa!.

Unaposhindwa kumtafuta Mungu kwa kazi yako unayofanya masaa 8 tu kwa siku, na kusema upo bize sana…kumbuka kuna mwingine aliye bize kuliko wewe mwenye kufanya kazi masaa 10 mahali pengine lakini hakosi ibada, wala hakosi muda wa kusali na kuomba na kusoma Neno…ingawa anachoka kulko wewe…Fahamu kuwa upendo wako unapimwa!

Mfalme Belshaza alipimwa akaonekana amepunguka na hivyo akaondolewa. Si ajabu leo watu wanaondoka katika mazingira yakutatanisha, huwenda wamepimwa wakaonekana kuwa wamepunguka.

Danieli 5:27 “TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka”.

Neema Mungu aliyokupa na ukaichezea, fahamu kuwa unapimwa katika mizani, unapoendelea kuichezea muda sio mrefu utaondolewa, na waweza kuondolewa ukabaki tu kutembea mfu.

Hivyo ndugu huu ni wakati wa kujipima kabla ya kupimwa!…na kujitathimini upya…

Kumbuka siku zote, usilisahau hili Neno utembeapo, uishipo…matendo yako yanapimwa katika mizani.

Ayubu 31:4 “Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote?

[5]Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;

[6](Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);

[7]Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;”

Bwana akubariki.

Je! Umempokea Yesu?

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *