Kwanini wengi leo wanashindwa na dhambi ya uasherati?
Fahamu mambo manne yanayochochea uzinzi/uasherati ndani ya mtu.
Kwanza ni vizuri kufahamu kuwa shetani hana amri au mamlaka ya kumlazimisha mtu afanye uasherati na dhambi zingine kwa ulazima, kama ingekuwa hivyo, basi shetani angehukumiwa mwenyewe katika ziwa la moto,…lakini shetani anachokifanya ni kumshawishi tu mtu aingie mkataba na dhambi..ndio maana biblia inasema “mtu anayefanya zinaa anatenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe” maana yake ni yeye mwenyewe kakusudia kutenda jambo hilo baya juu mwili wake na wala hajapitiwa na sio shetani ni yeye mwenyewe.
Kwahiyo mtu anayekwenda kufanya uasherati leo, ni yeye mwenyewe amechagua uovu kwa ushawishi wa nguvu za shetani…zingati hili (Ni huyo mtu kafanya na sio shetani kafanya kwa niaba yake)…Kwahiyo hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza ni huyo mtu, kwasababu kachagua kufanya mabaya
Na hizi ni baadhi ya njia anazotumia shetani kuwatumikisha watu kwenye dhambi hii ya zinaa.
1) Picha na Video za kizinzi (Pornography).
Hii ni nyenzo kubwa sana shetani ameitumia kwa kizazi hiki kukiangamiza, Hii ni njia yenye ushawishi mkubwa kuliko zote, kiasi kwamba mtu akijiingiza huko uasherati hawezi akaukwepa kwa namna yoyote iwe ni ameshaingia kwenye ndoa au hajaingia, iwe ni kijana, au mzee haikwepeki, mtu huyo atabakia kuwa mwasherati au mzinzi daima. Na hapo shetani hajahusika kukufanya ukafanye uasherati hapana ni wewe mwenyewe kwa ufahamu wako kabisa na kwa miguu yako umeamua kuwa hivyo. Kama ingekuwa ni shetani kakuvaa ufanye hivyo, siku ile ya hukumu Mungu asingekuhukumu wewe angemuhukumu shetani.Lakini biblia inasema waasherati watahukumiwa… Na mtu anayetazama hivi vitu kama hatadondokea kwenye uasherati moja kwa moja basi ataishia kwenye masturbation/kujichua ambayo nayo ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu.
2) Njia ya pili ni ‘Mazungumzo mabaya’ ;
Biblia inasema..”1Wakoritho 15: 33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema . ”
Haya ni mahubiri ambayo utakuta shetani anamuhubiria mtu pasipo hata yeye mwenyewe kujua, utakuta vijana au wazee kutwa kuchwa wanazungumza habari za wanawake, na wanawake vivyo hivyo utawakuta wana jadili habari za wanaume muda wote, lakini muda wa kutafakari mambo ya muhimu ya Mungu hakuna, sasa hapo watu kama hao ni rahisi sana kutawaliwa na roho za tamaa, kwasababu vichwa vyao wakati wote vimejazwa hayo mafundisho ya zinaa. Biblia inasema “hata uasherati usitamkwe kati yenu.”Utakuta kijana muda wote anaumalizia mtandaoni..ukitazama ni kitu gani anafanya, utagundua kuwa anachati katika magroup ambayo misingi yake ni uasherati, sasa kwa tabia hiyo haiwezekani wewe kuushinda uasherati hata uombeweje ni wewe tu kuamua kuacha hivyo vitu na kuanza kutii mahubiri ya Roho Mtakatifu ndani yako.
3) Mavazi:
Vimini, suruali, kaptura, nguo zinazobana na zinazoonyesha vifua na migongo wazi kwa wanawake n.k., hivi vyote ni vichecheo vya uasherati, mavazi hayo yalibuniwa kwa kazi hizo, kuwavuta wazinzi wasogee karibu na wewe, hivyo mtu anayejiita mkristo na kuanza kuzivaa moja kwa moja anakaribisha uwepo wa uzinzi ndani yake.
4) Mziki na filamu za kidunia:
Kusikiliza miziki ya kidunia hii pamoja na filamu za kimapenzi ni kichecheo kikubwa cha kubebwa na roho hizi, asilimia 99 ya miziki yote ya kidunia zina mahudhui ya kiasherati ndani yake unategemea vipi uepukane na tabia hizo?. Na ndio maana utakuta mtu analalamika hawezi kuacha kuwa mzinzi/mwasherati wakati muda wote anaumalizia kwenye vitabu, filamu na tamthilia za kimapenzi. Viache hivi vitu kwanza na ndipo utakapoanza kuona wepesi.
Na mambo hayo yakishakaa ndani yako sana, sasa yanakuwa yakijirudia rudia yenyewe tu kwenye akili yako, mpaka inakuwa ngumu kuyakwepa kwasababu ndio yaliyoujaza moyo wako,
Hivyo ndugu ukitaka kuushinda uasherati usitafute kuombewa, dawa ipo ndani yako mwenyewe kwanza ni kuchukua uamuzi wa kukataa kutii mahubiri yote ya shetani, na kuanza kumtii Roho Mtakatifu anapougua ndani ya moyo wako, ukifahamu kuwa mtu atendaye mambo hayo mwisho wake ni kuzimu… kwa kufanya hivyo utampa Roho Wa Mungu nafasi ya kukutengeneza upya mpaka mwisho wa siku unajikuta ile tamaa imezikwa kabisa, na kuweza kuishi maisha pasipo kutamani uasherati kabisa..Hivyo kataa hayo mahubiri yote ya shetani anayokuletea kupitia mtandao,(Pornography) na picha za uchafu, kwa kupitia kuchat katika mambo yasiyofaa, kwa kupitia mazungumzo mabovu, na kampani zisizo za ki-Mungu, kwa kupitia filamu, vitabu, tamthilia na miziki ya kidunia pamoja na mavazi ya kikahaba, Anza kukaa mbali kwanza na hivyo vitu vyote, na ndipo utakapoanza kuitawala mapenzi yako.
Na pia mawazo machafu yanapokujia kichwani kwako ni kuyakataa kwa kutafakari NENO LA MUNGU badala yake, ukizingatia hayo kidogo kidogo Roho Mtakatifu anaanza kuyazika ndani yako, mpaka kufikia hatua ya kutoweka kabisa na kuwa na uwezo wa kujitawala. Kwasababu biblia inasema
(Mithali 26: 20a, “MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI”)….Hivyo uasherati pia hufa kwa kukosa vichochezi. Unapojitenga na vichocheo vyote hivyo hata ile tamaa ya kufanya uasherati inakuwa haipo. Roho Mtakatifu anaizika mpaka inafikia hatua watu watakushangaa unawezaje kuishi muda wote huo pasipo kuwa mwasherati?.
Lakini kama hutaki kuweka chini hivyo vitendea kazi vya uasherati kamwe hutaweza kumshinda shetani.
Na mwisho wa siku utakufa katika hali hiyo na kwenda jehanumu… kwasababu biblia inasema WAASHERATI WOTE sehemu yao ni katika lile ziwa la Moto(Ufunuo 21:8)
Hivyo ndugu iogope hukumu ya Mungu, anza kubadilika sasa kimbia uasherati. Mwili wako ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na mtu auharibuye Mungu kasema atamuharibu mtu huyo.
Kama hujaokoka, amua leo kumpa Yesu maisha yako kwa kumaanisha kutubu kabisa na kuacha dhambi zote…kabla mlango wa neema haujafungwa kwako.
Maran atha(Bwana Yesu anarudi)
Ikiwa unahitaji msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.