MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 07)

  Siku za Mwisho, Uncategorized

Huu ni mwendelezo wa makala inayoangizia makanisa na mafundisho ya uongo yanayopotosha watu wengi nyakati hizi za mwisho, kama ulipitwa na sehemu za nyuma za makala hii unaweza tutumia ujumbe kwa namba zinazoonekana mwishoni mwa makala hii, au tembelea tovoti ya www.rejeabiblia.com ili uweze kuzipata makala hizo.


Hii ni sahemu ya saba (07) ya makala yetu, karibu!


MAKANISA YOTE YANAYOBATIZA KWA JINA LA BABA, NA LA MWANA, NA LA ROHO MTAKATIFU. 

Kanisa lolote lile linalofundisha na kubatiza kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (iwe kwa kunyunyuzia au katika maji tele), sio kanisa sahihi, haijalishi ni kubwa na zuri kiasi gani, au linawafuasi wengi kiasi gani, au ni la muda mrefu kiasi gani, au linatenda miujiza na ishara za ajabu kiasi gani, hilo ni la uongo, kwa sababu katika maandiko matakatifu hakuna mkristo yoyote yule aliyebatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, hakuna hata mmoja. Wakristo wote walibatizwa kwa jina la YESU KRISTO.

Matendo 8:16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ILA WAMEBATIZWA TU KWA JINA LAKE BWANA YESU.

Soma tena

Matendo 10:48 Akaamuru WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. 

Soma na tena

Matendo 19:5 Waliposikia haya wakabatizwa KWA JINA LA BWANA YESU. 

Swali la kujiuliza ni hili, Inamaana mitume wote hawa waliobatiza kwa jina la Yesu Kristo walikuwa ni wakosaji kwa kupinga agizo la Bwana Wao alipowaambia wakabatize kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu? 

Matayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

Kwa sababu hakuna mtume wala mwanafunzi yoyote yule aliyebatizwa au kubatiza hivyo, bali wote walibatiza na kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo.

Jibu ni kwamba, mitume walikuwa na uelewa wa kutosha sana kuhusu ubatizo, kwani wao hawakuanza kubatiza baada ya Yesu Kristo kupaa, hapana! Bali toka kipindi walipokuwa duniani wakitembea na Bwana walikuwa wakibatiza.

Yohana 4:1 Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, 

2 (LAKINI YESU MWENYEWE HAKUBATIZA, BALI WANAFUNZI WAKE,) 

Hivyo, wakati Bwana anawapa agizo hilo la kubatiza hakikuwa ni kitu kigeni kwao, kwa sababu walishakifanya sana wakati walipokuwa na Bwana. Na pia isitoshe, mitume hao hao walishaambiwa zamani sana jina la Baba ni nani kwani Bwana Mwenyewe aliwajulisha hilo.

Yohana 17:25 BABA mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.

26 NAMI NALIWAJULISHA JINA LAKO, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao. 

Soma tena 

Waebrania 1:4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri JINA ALILOLIRITHI lilivyo tukufu kuliko lao. 

Jina la Baba ni Yesu Kristo ambalo Mwana wa Adamu alilirithi, na Baba huyo huyo ndiye Roho (Yohana 4:24), huu ni ufunuo waliokuwa nao mitume

Wapo baadhi ya viongozi vipofu wanaosema hatupaswi kuwasikiliza mitume bali Yesu Kristo kwani mtume si mkubwa kuliko Bwana wake, ndugu, huo ni uongo wa ibilisi, Bwana Yesu aliwaambia mitume wake kuwa, mtu Yoyote atakayewasikiliza wao wamemsikiliza Yeye (Luka 10:16), na mtume Petro siku ya pentekoste alisema hivi..

Matendo 2:38 PETEO AKAWAAMBIA, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Ikiwa na maana kwamba, usipomsikiliza Petro hapo katika kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo ni sawa na umekataa kumsikiliza Yesu Kristo Mwenyewe, wewe, huyo kiongozi wako kipofu, na hilo kanisa lako la uongo. Na pia andiko hilo la mtumwa si mkuu kuliko Bwana wake halina uhusiano wowote ule na ubatizo, hivyo toka katika hilo kanisa la uongo na tafuta kanisa lolote la kiroho kwa ajili ya ubatizo sahihi wa kimaandiko (ambao ni wa maji tele na kwa Jina la Yesu Kristo).

Kama ulibatizwa Angrikana, Lutherani, Katoliki, Orthodoxy, kwa wasabato, Pentekoste, Morovian, jeshi la wokovu, mashahidi wa yehova, na kanisa lingine lolote lile kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, ulibatizwa kimakosa (ubatizo usio sahih), rekebisha ubatizo wako. Na pia kama ulibatizwa ukiwa mtoto mchanga tambua kuwa, ulibatizwa ubatizo bandia, watoto wachanga hawabatizwi, hivyo rekebisha ubatizo wako kwa kutubu dhambi zako zote na kisha kwenda kuzamisha katika maji tele na kwa jina la Yesu Kristo kama maandiko yanavyosema

Matendo 2:38 PETEO AKAWAAMBIA, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Kumbuka: hizi ni siku za mwisho na shetani anapambana juu chini ili kuwapotosha watu mbali na maagizo ya Mungu, kama ibilisi hakupati kwenye night clubs, au bar, miziki ya kidunia n.k, basi atakufuata huko huko kwenye biblia yako na kukupoteza kama usipotaka kujifunza.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada nyinginezo:

MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 03)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 02)


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)


Tabia moja ya unafiki unayopaswa kuiepuka.


UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?


Makuhani wa Mungu ni watu gani katika biblia?

6 thoughts on - MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 07)

LEAVE A COMMENT