Mambo yanayoweza kuzuia Mungu kutembea na wewe.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima..

Mungu anatamani sana kutembea na sisi na kujifunua zaidi kwetu,  na anataka wakati mwingi sana tuhisi uwepo wake katika maisha yetu..

Lakini kuna mambo baadhi ambayo yanaweza kuwa kikwazo kwa sisi kushindwa kutembea na Mungu vizuri.

Sasa ni muhimu sana kuyafahamu mambo hayo ni yapi na sio kufahamu tu lakini pia kufanya juhudi kuepukana nayo ili tumpe Roho Mtakatifu nafasi vizuri ya kutembea na sisi.

 

Mambo makuu manne yanayozuia Mungu kutembea na Wakristo wengi. 

 

1.Hasira/kutokuachilia.

Katika maisha ya Kikristo uchungu moyoni dhidi ya mtu fulani ni kizuizi namba moja kikubwa kinachozuia Roho Mtakatifu kutembea na wewe..

Ikiwa wewe huwezi kuachilia/kumsahehe mtu aliekukosea au aliekufanyia mabaya kama usipokuwa mtu wa kusamehe kutoka ndani unasema tu “nimemsaheme “ILA”….” hutakiwi kuwa mtu wa kuweka ILA katika kusamehe.  Same here na kuwa tayari kuanza upya..

NB Yesu hakusema “wasamehe hawajui walitendalo ILA”

Siku zote “msamaha sio kwa ajiri ya yule unaemsamehe bali ni kwa ajiri yako wewe “ unapokaa na uchungu Roho Mtakatifu hawezi kutembea na wewe japokuwa yupo ndani yako.

Unapokuwa mzito katika kusamehe au usipokuwa mtu wa kusamehe ni mambo mengi sana unayazuia amabayo Mungu anataka Kuyafanya kupitia wewe. Maandiko yanasema..

Mathayo 6:15“Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”

Hapa Bwana Yesu anaongea na wanafunzi wake wala si wapagani.. ni muhimu kufahamu msamaha wa dhambi tunaupokea bure bila kuwasamehe wengine ni kwa neema. Lakini tunapooshwa makosa yetu na Kristo kuwa ndani yetu tabia ya Kristo ndio inatakiwa ionekane kwetu kama yeye alivyotusamehe anataka kuona na sisi tukiwasamehe wengine vinginevyo mambo mengi hayatafunguka

Kwa sababu ya uchungu ulioruhusu ukae ndani yako. Hivyo kuwa mtu wa kuomba na kusoma neno kama huwezi kusamehe taratibu utaanza kuona Roho Mtakatifu anakupa nguvu ya kufanya hivyo.

2.Hofu.

Kuruhusu hofu itawale ndani yako kiasi kwamba unaona unaliona tatizo ni kubwa kuliko Mungu.  Wakati mwingine unasema “kwa hili sizani kama Mungu atanisaidia au ataweza..” Wakati huo maandiko yanasema “Mimi ni Mungu wa wote wenye mwilo je kuna jambo lolote gumu nisiloliweza?”.

 

Kadiri Mungu unavyomshusha chini ndio tatizo linavyozidi kuongezeka ukubwa, na Kadiri unavyomuweka juu ndio tatizo linazidi kuwa dogo”

Wewe ndio unaamua Mungu awe mkubwa kwako au awe mdogo kwako ukichagua awe mdogo kwako atakuwa.. na ukichagua awe mkubwa kwako ndivyo itakavyokuwa..

Mungu ni mmoja na mwenye uweza wote na yupo kwa kila mwamini ijapokuwa anauweza wote anapokuja kwetu anaacha sisi tuamue awe na uwezo gani kwetu..

Ni vigumu Mungu kutembea na wewe ukiwa una hali ya mashaka mashaka na hofu ndani yako na ndio maana Mungu anamwambia Yoshua awe jasiri

Yoshua 1:9“Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”

Maana yake Yoshua asingekuwa na moyo wa ushuja na akawa na hofu ndani yake asingewafikisha kaanani wana wa Israeli.  Yoshua asingeweza kwenda kata kuiagusha Yeriko..

Ujasiri katika Kristo pale tunapofahamu sisi ni wakina na nani na Kristo amefanya nini kwetu basi tunapokuwa na ujasiri mwingi wa namna hiyo Roho Mtakatifu ni rahisi kutembea na sisi.  Soma sana biblia na omba ufahamu umuelewe Kristo na upate kujifahamu kwa udani wewe ni nani.

3.kujiona duni(uduni).

Pale unapojiona wewe ni wa kishindwa tu hawezi unatafuta kazi hupati,unafungua biashara inakufa haiendi, unaanguka katika dhambi mara kwa mara ndugu yangu nataka nikwambie jambo moja ukiendelea kujiona hivyo ndivyo utakavyokuwa hivyo milele.

Mpaka pale utakapobadilisha mtazamo wako nje na hapo utaendelea kuwa hivyo hivyo na kama umeshajiona hivyo Roho Mtakatifu hawezi kufanya chochote kwako kwasababu ndani unajiona wewe ni dhaifu.

Ndugu yangu amua leo na kataa kabisa hali ya unyonge hata kama unaona mambo hayaendi muamini Mungu na tamka kwa imani “sitakuwa hivi siku zote na mimi sio wa hivi”

Unapopita katika magumu usijione huwezi au wewe ndio umeandikiwa hivyo HAPANA hujaandikiwa hivyo unaposhindwa usijione wewe ni wa kushindwa wewe ni mshindi katika Kristo Yesu na umebarikiwa kwa baraka zote kwa nini ukubali kuwa mnyonge..

Kataa hiyo hali sema “mimi ni mshindi na nitamdhirisha Mungu wangu maana atanitoa hapa” 

Kiri maneno ya ushindi hiyo hali ya kitambo kisha Songa mbele ukijiona hivyo Roho Mtakatifu ni rahisi sana kukutia nguvu. Maandiko yanasema “ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo…” 

Hivyo wewe ndio unaamua kuwa nani kuwa mnyonge au  la! Hujaandikiwa matatizo wala mikosi wewe umebarikiwa kwa baraka zote katika Kristo haijasaria hata baraka moja bali zote umbarikiwa sema AMINA kwa ujasiri wote.

4. Kujihukumu.

Unapokuwa mtu wa kujihukumu juu ya jambo fulani hata unapokosea unaona huwezi kusamehewa tena na Mungu,  unaon kosa ulilofanya ni kubwa sana Mungu hawezi kukusamehe..

Unajiona hufai tena mbele za Mungu, hata mawazo mabaya yanapokuja basi unaona Mungu hawezi kukuvumilia kwa hayo mawazo mabaya yanayokuja.. ndugu fahamu kabisa shetani atautumia mlango huo kuendelea kukunyanyasa kwa sababu umeshindwa kuielewa vizuri damu ya Yesu Kristo inafanya nini na ilifanya nini juu yako.

Utazame msalaba umefanya nini kwako, badala ya kuangalia sana dhambi na makosa unayokosea mara kwa mara uangalia mara kwa mara msalaba hata nguvu ya kuendelea mbele na kuishi maisha matakatifu itakuja ndani yako “

Maana unapouangalia msalaba unaamini kwamba yupo aliekutoa katika utumwa na yeye ndio anahusika kuhakikisha unakuwa salama mpaka wakati wa kuja kwake.

Usiwe mtu wa kujihukumu na kuona wewe si kitu na Mungu hawezi kukusamehe.. kama kukosea unakosea katika Mengi Mungu anakurehemu na bado ataendelea kukurehemu maana rehema zake ni nyingi kwa wamchao.

Zaburi 103:11“Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.”

Maana yake rehema za Mungu kwako hazina ukomo wowote kabisa labda wewe mwenyewe uamue kutoka mbele za Uso wa Mungu,  yaani kuachana na habari za Kristo na kurudi duniani ijapokuwa sio rahisi Mungu atafanya namna nyingi usiende katika uangamivu. 

Hivyo ndugu mambo haya kama yako ndani yako shughulika nayo na hitaji msaada wa Mungu ukusaidiee..

Nimekuombea katika jina la Yesu Kristo ukawe mtu wa viwango vingine Zaidi.

Ubarikiwe sana,

Mawasiliano 0613079530

Maranatha.

@Nuru ya Upendo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *