
NAWE UTAWAAMBIA MANENO YANGU, KWAMBA WATASIKIA, AU KWAMBA HAWATAKI KUSIKIA;
Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe.
Upo umuhimu wa kuhubiri injili mahali popote na katika mazingira yoyote kwasababu ni agizo la Bwana mwenyewe bila kuangalia watu wanapokeaje; wanataka kusikia au hawataki kusikia.
Wapo watu wenye mioyo migumu..ambao wanajiziba masikio yao wasitake kusikia habari za kuacha maovu na kumgeukia MUNGU wa kweli. Lakini Nabii Ezekieli aliambiwa..
“Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana”.(Ezekieli 2:7
Umeona, watasikia tu kwa ulazima, kwamba wanataka au hawataki kusikia… maana wataokolewaje sasa wasipohubiriwa wakasikia?
Warumi 10:13-14 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
[14]Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
Ni lazima tu wahubiriwe, wasikie kisha waamue kuokoka, hakuna njia nyingine ambayo ilikuwepo au itakuja kuwepo.
Hivyo wewe dada/kaka unayesoma ujumbe huu, huwenda ni wewe ambaye una moyo mgumu hutaki kuelewa na kusikia habari za wokovu wa roho yako, lakini leo umepata neema ya kufikiwa na habari hizi mahali hapa..ili uamue kufanya uamuzi wa kuokoka na kuacha njia zako mbaya.
Amua kuacha ulevi wako, acha uzinzi na uasherati unaoufanya kila wakati, acha kujichua, acha ukahaba, acha kujipodoa, acha kiburi, acha usengenyaji, acha kusikiliza miziki na michezo ya kidunia, acha udunia kabisa na amua kuokoka kweli kweli acha kumchanganya Mungu na dunia.
Hizi ni nyakati za mwisho kabisa, Yesu anarudi muda wowote.
Acha kujitia ganzi, fungua moyo wako leo na amua kuokoka leo leo ingali bado neema ipo.
Maran atha.
Ikiwa unahitaji msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.